Askofu Gwajima omba msamaha, siku ya mahubiri yako kanisani juu ya utekaji ulimkosea Mungu na Rais

Askofu Gwajima omba msamaha, siku ya mahubiri yako kanisani juu ya utekaji ulimkosea Mungu na Rais

Mimi nakupenda sana tangia kipindi cha covid 19. Misimamo yako naipenda sana ikiwa unasema ukweli. Siku unahubiri kanisani kuhusu utekaji nilikuwa nakufuatilisa vizuri. Tangia unaingika kanisani nilikufuatilitia vizuri.

Lakini mh Askofu niliingiwa na hofu kuu sana nikajiuliza hiki nini kimetokea. Kuhubiri juu ya utekaji siyo mbaya, lakini namna ulivyoanza mahubiri yako siyo heshima kwa Mungu na kwa taratibu za kanisa lenye kuwalisha kondoo neno la uzima. Unaanza kuhubiri kabla ya kusoma neno la MUNGU? Pale kanisani tunaenda kusikiliza neno la Mungu kwanza. Leo Mungu wetu ametuandalia nini watoto wake, kama chakula cha uzima?

Neno la Mungu ndiyo chakula cha uzima, mengine pale ulikuwa unapiga blablaa tu. Yale maneno yako ya siku ile hayawezi kuwapa watu uzima na kuwapeleka watu mbinguni. Kama ni kuhubiri kuhusu utekaji, ulitakiwa utafute kifungu kwenye Biblia KINACHOENDANA NA MAHALIFU KATIKA jamii, ukifananue vizuri, ndiposa uchomekee maneno kuhusu utekaji unaotokea nchini.

Kosa lingine ni kumtaji mkuu wa nchi japo indirectly kwamba anahusika na utekaji. Kwa kweli ulipotamka kwamba anayekupinga tujiulize anahusikaje kwenye utekaji, moyo uliniuma sana kwa sababu niliona sasa umekwea kwengine ambako kutoka huko itakuwa shida. Mh Rais kwenye chama alikujibu kiimani, wewe ukatafsiri amekupinga.

Lakini hata kama angekuwa amekupinga, wewe kama askofu uchungaye kondoo hukutakiwa kuwaonyesha waumini wako tena kanisani kwamba sasa inajulikana anayeagiza watu watekwe ni huyu, maana bado huna ushahidi. Na hata kama una ushahidi bado huna uwezo wa kupambana na taasisi ya uraisi. Na kwa nini wewe kama mchungaji wa kondoo uwe chanzo cha machafuko? Hatufanyagi hivyo mzee.

Unakumbuka lile neno YESU KRISTO alilowambia wanafunzi wake wakati anawatuma ulimwenguni? Au wewe siyo mwanafunzi wa YESU kwa sababu ni askofu?

Mt 10:16 ​


Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.

sasa wewe unakuwa mkali badala ya kuwa mpole .unategemea nini ?

unakumbuka kisa cha cha jogoo wa wili jasiri na mwoga?

nakushauri uombe msamaha kwa mkuu wa nchi na pia kwa MUNGU na kwa waumini.umesababisha kondoo kutawanyika sasa hawana mchungaji? umesababisha uitwe mtumishi wa shetani na siyo wa Mungu.Hii ni kosa lako kubwa.Nakuomba ukatubu

jifunze kwa YESU .yeye ni mpole na mnyenyekevu

Mt 11:29 ​

Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu

wakati mwingini upole ni mhimu sana.ache wengine waongee wewe baki katika kuwaombea waongeaji wapate hekima na busara katika kuongea.

Kwa hivyo ulipenda amshukuru maza kwenye lindi la utekwaji, ukabwaji, ubakwaji na uf*rwaji?

Yaani kuwa zuzu tu kama kina Lukasi na nduguye nduguye?
 
Kuna siku utafikiwa tu wewe au ndugu zako usifikiri uko salama sana wewe mwanalumumba.

Yaani anayekemea utekaji ndio awe kisababishi cha machafuko na sio mtekaji na boss wao?

Kutoka maktaba miaka 8 iliyopita jionee

Kutoka Bungeni DODOMA, leo April 10, 2017 Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe alisimama kuomba kutoa taarifa kwa Naibu Spika wa Bunge akitaka Bunge lisimamishe shughuli za kawaida na kuanza kujadili matukio ya utekaji watu yanayoendelea nchini.Bashe amesema yeye pia ameshatumiwa ujumbe wa vitisho wakimwambia kuna watu 11 akiwemo yeye watafanyiwa vitendo vibaya popote watakapokuwa, hivyo analiomba Bunge lijadili suala hilo kwa dharula kwasababu sio sawa kukaa kimya.


View: https://youtu.be/Y0Y24wdT9OI?si=KR5hx9Y7psY5kOqd

mbunge bora kabisa katika bunge la AWAMU YA SITA.Hata GWAJIMA agesemea yale bungeni wala asingeingia matatani.BUNGENI ni uwanja wa siasa na kutoa hoja,kukemea maovu ,kuwasema wanasiasa na viongozi wengine.siyo kanisani wala mskititini
 

Warumi 13:1​


Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu.
Tangu zamani mamlaka zikikengeuka hufurushwa hata na Mungu mwenyewe..

1 Samweli 15:26
Samweli akasema, Sitarudi pamoja nawe; kwa sababu umelikataa neno la BWANA, BWANA naye amekukataa wewe, usiwe mfalme wa Israeli.

1 Samweli 15:28
Basi Samweli akamwambia, Leo BWANA amekurarulia ufalme wa Israeli, naye amempa jirani yako, aliye mwema kuliko wewe.
 
Ukweli upo pale pale - CCM na washirika wake wanapoteza watu tunasimama na Askofu Gwajima.

No Reforms......
 
Tangu zamani mamlaka zikikengeuka hufurushwa hata na Mungu mwenyewe..

1 Samweli 15:26
Samweli akasema, Sitarudi pamoja nawe; kwa sababu umelikataa neno la BWANA, BWANA naye amekukataa wewe, usiwe mfalme wa Israeli.

1 Samweli 15:28
Basi Samweli akamwambia, Leo BWANA amekurarulia ufalme wa Israeli, naye amempa jirani yako, aliye mwema kuliko wewe.
Biblia au Quran ni sawa na kichaka.ukishika njia moja ( neno moja ) unaweza kujikuta uko shimoni ukabaki unalilia na MUNGU akakushangaa umeingiaje humo:
 
mbunge bora kabisa katika bunge la AWAMU YA SITA.Hata GWAJIMA agesemea yale bungeni wala asingeingia matatani.BUNGENI ni uwanja wa siasa na kutoa hoja,kukemea maovu ,kuwasema wanasiasa na viongozi wengine.siyo kanisani wala mskititini
Wee chawa,
Tulia alishakataza kujadili utekaji na mauaji bungeni
 
Tangu zamani mamlaka zikikengeuka hufurushwa hata na Mungu mwenyewe..

1 Samweli 15:26
Samweli akasema, Sitarudi pamoja nawe; kwa sababu umelikataa neno la BWANA, BWANA naye amekukataa wewe, usiwe mfalme wa Israeli.

1 Samweli 15:28
Basi Samweli akamwambia, Leo BWANA amekurarulia ufalme wa Israeli, naye amempa jirani yako, aliye mwema kuliko wewe.
lakini usisahau kuwa mfalme hashiki upanga bure
 
Biblia au Quran ni sawa na kichaka.ukishika njia moja ( neno moja ) unaweza kujikuta uko shimoni ukabaki unalilia na MUNGU akakushangaa umeingiaje humo:
Ndiyo sababu tunakushangaa unavyojaribu kutumia maandiko kupamba watawala mafisadi, wezi wa uchaguzi, watekaji, wafiraji, wauaji 🚮

NO REFORMS NO ELECTION 📌
 
Ndiyo sababu tunakushangaa unavyojaribu kutumia maandiko kupamba watawala mafisadi, wezi wa uchaguzi, watekaji, wafiraji, wauaji 🚮

NO REFORMS NO ELECTION 📌
ndo maana nasema kuna sehemu nzuri unaweza ukawakemea ukawa salama zaidi lakini bsiyo kanisani wala msikitini
 
ndo maana nasema kuna sehemu nzuri unaweza ukawakemea ukawa salama zaidi lakini bsiyo kanisani wala msikitini
CHAWA,
Wacha upotoshaji.
Vitabu vya dini zote vinakataza dhambi za wizi, ufiraji, mauaji, nk
Ni jukumu la watumishi wa Mungu kukemea watawala wanapokengeuka kwa kutenda maovu na kuwarejesha kwenye njia sahihi.
 
mbunge bora kabisa katika bunge la AWAMU YA SITA.Hata GWAJIMA agesemea yale bungeni wala asingeingia matatani.BUNGENI ni uwanja wa siasa na kutoa hoja,kukemea maovu ,kuwasema wanasiasa na viongozi wengine.siyo kanisani wala mskititini
Subiri muda utatupa majibu.

Nakukumbusha tu watekaji wakija hawaulizi wewe ni chama gani wala hawaangalii rangi wala huulizwi dini.

Pengine bila watu kuwepo pale 2017 ndio ungekuwa mwisho wa Nape kuishi , tunaongelea Nape ambaye alifanya mbinu zake zote chafu kuhakikisha waliotaka kumuua wanaingia madarakani 2015.

Kama hujajifunza basi kuna siku utaelewa.
 
ndo maana nasema kuna sehemu nzuri unaweza ukawakemea ukawa salama zaidi lakini bsiyo kanisani wala msikitini
Em pitia haya madini hapa...
👇
Mifano hii inaonyesha jukumu muhimu la manabii katika nyakati za kale.Manabii hawa walitumika kama sauti ya Mungu ya kupinga na kurekebisha kasoro za kimaadili,Kiutawala na kiimani za wafalme mbali mbali

Katika masimulizi kadhaa ya Biblia, manabii walitumika kama wajumbe wa Mungu, mara nyingi waliopewa jukumu la kuogofya na la kukabiliana na uovu wa wafalme. Manabii hawa waliteuliwa na Mungu ili kutangaza ukosefu wa haki, ibada ya sanamu, na upotovu wa maadili, wakiwahimiza watawala kurudi kwenye uaminifu na Kusimamia haki.Jumbe za Manabii hao hazikuwa maonyo tu bali pia wito wa kutubu, zikikazia matokeo ya kutotii na adhabu ya Mungu juu ya Wafalme hao.

Nathani na Mfalme Daudi

Mojawapo ya Kisa maarufu zaidi cha nabii kumkabili mfalme kinapatikana katika simulizi la Nathani na Mfalme Daudi. Baada ya dhambi nzito za Daudi za uzinzi na Bathsheba na kifo kilichopangwa cha mume wake Uria, Mungu alimtuma Nathani kutoa mfano uliofichua kosa la Daudi. Nathani alisema kwa ujasiri, "Wewe ndiye mtu huyo!" ( 2 Samweli 12:7 ), ikimwongoza Daudi kwenye toba. Ujumbe huu wa Nabii Nadhani kwa Mfalme Daudi ulikazia Jukumu la nabii huyo katika kuwawajibisha hata wale walio na nguvu zaidi kwa viwango vya Mungu.

Eliya na Mfalme Ahabu

Huduma ya Eliya wakati wa utawala wa Mfalme Ahabu ni mfano mwingine mkubwa. Ahabu, kwa kusukumwa na mke wake Yezebeli, aliongoza Israeli katika ibada ya sanamu na ibada ya Baali. Eliya alimkabili Ahabu, akisema, “Kama BWANA, Mungu wa Israeli, aishivyo, ambaye ninasimama mbele zake, hakutakuwa na umande wala mvua katika miaka hii, isipokuwa kwa neno langu” (1 Wafalme 17:1). Changamoto ya Eliya juu ya Mlima Karmeli, ambapo Mungu alionyesha uwezo wake juu ya miungu ya uongo, ilikuwa kemeo la moja kwa moja la uasi wa Ahabu na wito wa kurudi kwenye
Nafasi yake kama Mfalme

Isaya na Mfalme Hezekia

Nabii Isaya alitumikia wakati wa utawala wa wafalme kadhaa, kutia ndani Hezekia. Ingawa kwa ujumla Hezekia alikuwa mfalme mwadilifu, aliyumbayumba katika nyakati za kiburi na kutegemea mashirikiano ya kigeni. Isaya alimwonya juu ya matokeo ya matendo yake, hasa utekwa wa Babeli uliokuwa ukija (Isaya 39:5-7). Huduma ya Isaya yakazia Jukumu la nabii katika kutoa mwongozo na marekebisho, hata kwa wale ambao kwa sehemu kubwa ni waaminifu.

Yeremia na Wafalme wa Yuda

Huduma ya kinabii ya Yeremia ilitiwa alama na maonyo yake ya kuendelea kwa wafalme wa Yuda kuhusu uhamisho wa Babeli uliokuwa ukija kwa sababu ya kuendelea kuabudu sanamu na ukosefu wa haki. Licha ya kuteswa na kufungwa, Yeremia alitoa ujumbe wa Mungu kwa uaminifu, akihimiza watubu na kurudi kwenye uaminifu wa agano. Mwingiliano wake na wafalme kama Yehoyakimu na Sedekia unaonyesha kujitolea kwa nabii kwa ukweli, bila kujali gharama ya kibinafsi (Yeremia 22:1-5).

Amosi na Ufalme wa Kaskazini

Amosi, ingawa alikuwa mchungaji kutoka Yuda, aliitwa kutoa unabii dhidi ya Ufalme wa Kaskazini wa Israeli wakati wa ufanisi na uharibifu wa maadili. Alishutumu ukosefu wa haki wa kijamii na unafiki wa kidini wa tabaka tawala, akisema, “Kwa maana najua makosa yenu ni mengi na dhambi zenu ni nyingi” ( Amosi 5:12 ). Ujumbe wa Amosi ulikuwa ukumbusho kamili kwamba haki ya Mungu inavuka mipaka ya kitaifa na kwamba ufanisi si ishara ya kibali cha kimungu unapoambatana na ukosefu wa uadilifu.

Yohana Mbatizaji na Herode Antipa

Katika Agano Jipya, Yohana Mbatizaji anatoa mfano wa mapokeo ya kinabii ya kuwakabili watawala. Kwa ujasiri alimkemea Herode Antipa kwa kumwoa Herodia, mke wa ndugu yake kinyume cha sheria, akisema, “Si halali kwako kuwa naye” ( Mathayo 14:4 ). Utangazaji wa kweli wa Yohana bila woga hatimaye uliongoza kwenye kufungwa kwake na kuuawa kishahidi, ikionyesha gharama ya ushahidi wa kinabii mbele ya mamlaka ya kisiasa.

Kulingana na Mifano hii tunaona kwamba sio wafalme wote walioweza kupokea au kukubaliana na maonyo,ukosoaji au ujumbe wa kuwashauri uliotoka kwa Viongozi wa kidini walipowaendea hao wafalme.
Wengi kwa kukutumia madaraka yao ya kiutawala waliwaudhi au hata kuwadhuru Manabii hao.
 
KWANI ANGEENDA BUNGENI ASINGEWEZA KUKEMEA WATEKAJI?
HAHAHAAHAH
Tuache kutafuta kichaka cha kijifichia.Hamas imejenga mahandaki chi ya hospital ,miskiti na shule kwa sababu sheria za kivita zinatambua maeneo hayo kwamba hayatakiwi kushambuliwa.NETANYAHU akasema washenzi wa kubwa kabisa ,nitawafuata huko huko.sasa na sisi tusifaanye misikiti na makanisa kuwa sehemu ya siasa na kuwakemea viongozi wa nchi.iko siku atakuja kiongozi kichaa atakufuata huko huko
Ni kwamba tu huna akili. Masuala ya utekaji hayajaongelewa kanisani tu kwa taarifa Yako mtaani, misikitini, kwenye bunge , taasisi binafsi mpaka nchi za nje yameongelewa kwahiyo huna hoja
 
Mimi nakupenda sana tangia kipindi cha covid 19. Misimamo yako naipenda sana ikiwa unasema ukweli. Siku unahubiri kanisani kuhusu utekaji nilikuwa nakufuatilisa vizuri. Tangia unaingika kanisani nilikufuatilitia vizuri.

Lakini mh Askofu niliingiwa na hofu kuu sana nikajiuliza hiki nini kimetokea. Kuhubiri juu ya utekaji siyo mbaya, lakini namna ulivyoanza mahubiri yako siyo heshima kwa Mungu na kwa taratibu za kanisa lenye kuwalisha kondoo neno la uzima. Unaanza kuhubiri kabla ya kusoma neno la MUNGU? Pale kanisani tunaenda kusikiliza neno la Mungu kwanza. Leo Mungu wetu ametuandalia nini watoto wake, kama chakula cha uzima?

Neno la Mungu ndiyo chakula cha uzima, mengine pale ulikuwa unapiga blablaa tu. Yale maneno yako ya siku ile hayawezi kuwapa watu uzima na kuwapeleka watu mbinguni. Kama ni kuhubiri kuhusu utekaji, ulitakiwa utafute kifungu kwenye Biblia KINACHOENDANA NA MAHALIFU KATIKA jamii, ukifananue vizuri, ndiposa uchomekee maneno kuhusu utekaji unaotokea nchini.

Kosa lingine ni kumtaji mkuu wa nchi japo indirectly kwamba anahusika na utekaji. Kwa kweli ulipotamka kwamba anayekupinga tujiulize anahusikaje kwenye utekaji, moyo uliniuma sana kwa sababu niliona sasa umekwea kwengine ambako kutoka huko itakuwa shida. Mh Rais kwenye chama alikujibu kiimani, wewe ukatafsiri amekupinga.

Lakini hata kama angekuwa amekupinga, wewe kama askofu uchungaye kondoo hukutakiwa kuwaonyesha waumini wako tena kanisani kwamba sasa inajulikana anayeagiza watu watekwe ni huyu, maana bado huna ushahidi. Na hata kama una ushahidi bado huna uwezo wa kupambana na taasisi ya uraisi. Na kwa nini wewe kama mchungaji wa kondoo uwe chanzo cha machafuko? Hatufanyagi hivyo mzee.

Unakumbuka lile neno YESU KRISTO alilowambia wanafunzi wake wakati anawatuma ulimwenguni? Au wewe siyo mwanafunzi wa YESU kwa sababu ni askofu?

Mt 10:16 ​


Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.

sasa wewe unakuwa mkali badala ya kuwa mpole .unategemea nini ?

unakumbuka kisa cha cha jogoo wa wili jasiri na mwoga?

nakushauri uombe msamaha kwa mkuu wa nchi na pia kwa MUNGU na kwa waumini.umesababisha kondoo kutawanyika sasa hawana mchungaji? umesababisha uitwe mtumishi wa shetani na siyo wa Mungu.Hii ni kosa lako kubwa.Nakuomba ukatubu

jifunze kwa YESU .yeye ni mpole na mnyenyekevu

Mt 11:29 ​

Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu

wakati mwingini upole ni mhimu sana.ache wengine waongee wewe baki katika kuwaombea waongeaji wapate hekima na busara katika kuongea.
"UTTER NONSENSE" - PAUL KAGAME
 
CHAWA,
Wacha upotoshaji.
Vitabu vya dini zote vinakataza dhambi za wizi, ufiraji, mauaji, nk
Ni jukumu la watumishi wa Mungu kukemea watawala wanapokengeuka kwa kutenda maovu na kuwarejesha kwenye njia sahihi.
NI SAHIHI ,LAKINI KUNA NAMNA YA KUWAKEMEA INDIRECTLY BILA KUONEKANA UMEWATAJA MAJINA YAO
 
Back
Top Bottom