CHANANJA THE BIG DYNASTY
JF-Expert Member
- Sep 14, 2024
- 1,272
- 1,873
hata Mshua wangu Kai$ari angekuwa hai hii leo, angekuita MSENGEnyaji tu kwa uk*ma ulioandika hapa.
Kwani hujasoma mateso aliyoyapata Yesu baada ya kupigwa shavu la kulia? Alivishwa taji ya miiba, alipigwa mijeredi, Alisulibiwa, alichomwa mkuki. Hayo ni nini kama sio kuwageuza shavu la piliHivi unafahamu kwamba hata yeye alipopigwa hilo shavu la kulia hakugeuza la kushoto badala yake alihoji sababu ya kuchapwa kofi?
Yohana 18:23
[23]Yesu akamjibu, Kama nimesema vibaya, ushuhudie ule ubaya; bali kama nimesema vema, wanipigia nini?
Biblia haisomwi kama magazeti yenu ya udaku.
ni Yesu sio yesuKumbe yesu hakuwa mtawala?
Hapa unakosea mtumishi. Nani amemtukana mkuu wa nchi? lini, wapiKwani sheria za nchi yako zinasemaje. Zinakuruhusu kumtukana Mkuu wa nchi?
Nadhani huwa husomi comments zote. Soma post #8Nani amemtukana mkuu wa nchi? lini, wapi
Mbona mara nyingi aliwaita "uzao wa nyoka"? Kwani hiyo ni sifa?Katikati ya Watawala hao wa kisiasa, Yesu hakuwahi kuwatukana wala kutumia lugha ya dhihaka dhidi yao.
Alimwita Herode MbwehaYesu alipokuwa duniani, nchi aliyokuwa akiishi ilikuwa chini ya utawala wa Dola ya Kirumi. Wakati Yesu anazaliwa, Herod the Great, ndiye aliyekuwa Mtawala. Huyo ndiye aliyeamuru watoto wa Bethlehemu wauawe ili Yesu aangamie. Baadaye alitawala Herod Antipas, Mwana wa Herod the Great. Huyu alitawala wakati wa huduma ya Yesu na alikuwa pia na nafasi katika hukumu ya Yesu (Luka 23:7-11). Huyu ndiye aliyeamuru Yohana Mbatizaji auawe (Marko 6:17-28). Pontius Pilate, alikuwa liwali wa Kirumi (gavana) wa Yudea kutoka mwaka 26 hadi 36 BK. Huyu alikuwa na mamlaka ya mwisho ya kisiasa na kisheria katika Yudea. Huyu ndiye aliyemhukumu Yesu atundikwe msalabani, ingawa hakuona kosa lolote kwa Yesu (Mathayo 27, Yohana 18–19).
Katikati ya Watawala hao wa kisiasa, Yesu hakuwahi kuwatukana wala kutumia lugha ya dhihaka dhidi yao.
Katika Yohana 18:36-37 tunaona Yesu akizungumza kwa heshima, hata alipokuwa anapewa hukumu ya kifo.
Katika mafundisho yake, Yesu alionyesha kwamba hata watawala wa kidunia wana nafasi waliyopewa na Mungu kwa sababu fulani. Kwa mfano, watu walipomjaribu kuhusu kulipa kodi kwa Kaisari, Yesu alisema: "Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na ya Mungu mpeni Mungu." (Mathayo 22:21). Hapa Yesu anaonesha kwamba hata mamlaka za kisiasa zinastahili kuheshimiwa.
Viongozi aliowakemea Yesu ni wa kidini(Mafarisayo, Masadukayo na Waandishi) kwa sababu walikuwa wanawapotosha watu kwa mafundisho yaliyo kinyume na mapenzi ya Mungu.
Yesu aliwatahadharisha wanafunzi wake kuwa watachukiwa na kuonewa na watu, lakini hakuwahamasisha wafanye uasi au 'kukinukisha.'
Katika Mathayo 10:16-20 Yesu anawaambia wanafunzi wake wakipelekwa mahakamani au mbele ya watawala wa Kirumi, wawe na busara kama nyoka na wapole kama njiwa.
Katika lile tukio la askari na kundi lililoenda 'kumteka' Yesu, Petro alitoa upanga na kumkata sikio mtumishi wa Kuhani mkuu. Yesu alimuonya Petro na kumwambia arudishe upanga alani mwake, kisha akamponya huyo aliyekatwa sikio!
Yesu hakushabikia matumizi ya nguvu au mashambulizi dhidi ya viongozi, hata wakati huo wa kukamatwa kwake. Hili ni fundisho la wazi kwamba Yesu alipinga ghasia na vurugu dhidi ya wenye mamlaka.
Kumbuka pale msalabani, jinsi Yesu alivyowaombea waliomsulibisha, Mungu awasamehe. Msimamo wa Yesu ulikuwa ni kuhubiri mabadiliko ya moyo(heart reform), na sio mapinduzi ya kisiasa. Alijua kuwa mioyo ya watu ikibadilika, wataacha uovu. Sauli alikuwa mbaya sana, na alifurahia kuona watu wa Mungu wakiuawa, lakini moyo wake ulipofanyiwa reform, alibadilika na kuwa mtu mwema.
Wanaohubiri Injili kwa maslahi ya matumbo yao waliishafichuliwa. Kama huwajui soma uzi huuHuna nondo za kunilisha zaidi unatumia maandiko kufanya upotoshaji kwa maslahi ya tumbo lako
Umechambua na kunena vyema mkuu,Mifano hii inaonyesha jukumu muhimu la manabii katika nyakati za kale.Manabii hawa walitumika kama sauti ya Mungu ya kupinga na kurekebisha kasoro za kimaadili,Kiutawala na kiimani za wafalme mbali mbali
Katika masimulizi kadhaa ya Biblia, manabii walitumika kama wajumbe wa Mungu, mara nyingi waliopewa jukumu la kuogofya na la kukabiliana na uovu wa wafalme. Manabii hawa waliteuliwa na Mungu ili kutangaza ukosefu wa haki, ibada ya sanamu, na upotovu wa maadili, wakiwahimiza watawala kurudi kwenye uaminifu na Kusimamia haki.Jumbe za Manabii hao hazikuwa maonyo tu bali pia wito wa kutubu, zikikazia matokeo ya kutotii na adhabu ya Mungu juu ya Wafalme hao.
Nathani na Mfalme Daudi
Mojawapo ya Kisa maarufu zaidi cha nabii kumkabili mfalme kinapatikana katika simulizi la Nathani na Mfalme Daudi. Baada ya dhambi nzito za Daudi za uzinzi na Bathsheba na kifo kilichopangwa cha mume wake Uria, Mungu alimtuma Nathani kutoa mfano uliofichua kosa la Daudi. Nathani alisema kwa ujasiri, "Wewe ndiye mtu huyo!" ( 2 Samweli 12:7 ), ikimwongoza Daudi kwenye toba. Ujumbe huu wa Nabii Nadhani kwa Mfalme Daudi ulikazia Jukumu la nabii huyo katika kuwawajibisha hata wale walio na nguvu zaidi kwa viwango vya Mungu.
Eliya na Mfalme Ahabu
Huduma ya Eliya wakati wa utawala wa Mfalme Ahabu ni mfano mwingine mkubwa. Ahabu, kwa kusukumwa na mke wake Yezebeli, aliongoza Israeli katika ibada ya sanamu na ibada ya Baali. Eliya alimkabili Ahabu, akisema, “Kama BWANA, Mungu wa Israeli, aishivyo, ambaye ninasimama mbele zake, hakutakuwa na umande wala mvua katika miaka hii, isipokuwa kwa neno langu” (1 Wafalme 17:1). Changamoto ya Eliya juu ya Mlima Karmeli, ambapo Mungu alionyesha uwezo wake juu ya miungu ya uongo, ilikuwa kemeo la moja kwa moja la uasi wa Ahabu na wito wa kurudi kwenye
Nafasi yake kama Mfalme
Isaya na Mfalme Hezekia
Nabii Isaya alitumikia wakati wa utawala wa wafalme kadhaa, kutia ndani Hezekia. Ingawa kwa ujumla Hezekia alikuwa mfalme mwadilifu, aliyumbayumba katika nyakati za kiburi na kutegemea mashirikiano ya kigeni. Isaya alimwonya juu ya matokeo ya matendo yake, hasa utekwa wa Babeli uliokuwa ukija (Isaya 39:5-7). Huduma ya Isaya yakazia Jukumu la nabii katika kutoa mwongozo na marekebisho, hata kwa wale ambao kwa sehemu kubwa ni waaminifu.
Yeremia na Wafalme wa Yuda
Huduma ya kinabii ya Yeremia ilitiwa alama na maonyo yake ya kuendelea kwa wafalme wa Yuda kuhusu uhamisho wa Babeli uliokuwa ukija kwa sababu ya kuendelea kuabudu sanamu na ukosefu wa haki. Licha ya kuteswa na kufungwa, Yeremia alitoa ujumbe wa Mungu kwa uaminifu, akihimiza watubu na kurudi kwenye uaminifu wa agano. Mwingiliano wake na wafalme kama Yehoyakimu na Sedekia unaonyesha kujitolea kwa nabii kwa ukweli, bila kujali gharama ya kibinafsi (Yeremia 22:1-5).
Amosi na Ufalme wa Kaskazini
Amosi, ingawa alikuwa mchungaji kutoka Yuda, aliitwa kutoa unabii dhidi ya Ufalme wa Kaskazini wa Israeli wakati wa ufanisi na uharibifu wa maadili. Alishutumu ukosefu wa haki wa kijamii na unafiki wa kidini wa tabaka tawala, akisema, “Kwa maana najua makosa yenu ni mengi na dhambi zenu ni nyingi” ( Amosi 5:12 ). Ujumbe wa Amosi ulikuwa ukumbusho kamili kwamba haki ya Mungu inavuka mipaka ya kitaifa na kwamba ufanisi si ishara ya kibali cha kimungu unapoambatana na ukosefu wa uadilifu.
Yohana Mbatizaji na Herode Antipa
Katika Agano Jipya, Yohana Mbatizaji anatoa mfano wa mapokeo ya kinabii ya kuwakabili watawala. Kwa ujasiri alimkemea Herode Antipa kwa kumwoa Herodia, mke wa ndugu yake kinyume cha sheria, akisema, “Si halali kwako kuwa naye” ( Mathayo 14:4 ). Utangazaji wa kweli wa Yohana bila woga hatimaye uliongoza kwenye kufungwa kwake na kuuawa kishahidi, ikionyesha gharama ya ushahidi wa kinabii mbele ya mamlaka ya kisiasa.
Kulingana na Mifano hii tunaona kwamba sio wafalme wote walioweza kupokea au kukubaliana na maonyo,ukosoaji au ujumbe wa kuwashauri uliotoka kwa Viongozi wa kidini walipowaendea hao wafalme.
Wengi kwa kukutumia madaraka yao ya kiutawala waliwaudhi au hata kuwadhuru Manabii hao.
Nadhani umeelewa.... jitahidi kuwa na huruma na damu zinazomwagika nchini mwako...naomba ukumbuke hili siku unayokufa...ulishindwa kuwatetea ulijali tumbo lako kwa hongo unazopewa.Upendo mkuu,upendo mama,kuwa na upendo.Loo, wewe mwenye akili nyingi nioneshe kwenye uzi wangu nimeandika wapi neno "mhubiri"
Ona sasa umeshindwa kuthibitisha. Wewe unafikiri JamiiForums inasomwa katika nchi yako tu. Ujumbe wa mada hii unawahusu watu wa nchi zote.Nadhani umeelewa.... jitahidi kuwa na huruma na damu zinazomwagika nchini mwako...naomba ukumbuke hili siku unayokufa...ulishindwa kuwatetea ulijali tumbo lako kwa hongo unazopewa.Upendo mkuu,upendo mama,kuwa na upendo.
Kampa jina bila kujua sioKwahiyo samia aitwe mbweha?
Mwambie kiongozi yeyote leo kuwa yeye ni mbweha tuone kama sio tusi. Rahisi tu. 🤣🤣🤣.Kuna watu wanadai Yesu alitukana au alimkosea heshima Herod Antipas kwa kumuita “mbweha.” aliposema “Mwambieni yule Mbweha...”
Wananukuu Andiko la Luka 13:32, Yesu aliposema:
“...Nendeni, mkamwambie yule mbweha, Tazama, leo na kesho natoa pepo na kuponya wagonjwa, siku ya tatu nakamilisha kazi yangu.”
Ukichunguza vizuri utaona kuwa hilo halikuwa tusi. Katika tamaduni za Wayahudi, "mbweha" ni mfano wa mtu asiye na nguvu kama simba. Kwa mfano huo alikuwa akiwafundisha wanafunzi wake kuwa Herod Antipas hana nguvu ya kumzuia kukamilisha kazi aliyotumwa na Baba.
Kwahiyo andiko hilo halitupi ruhusa ya kuwatukana viongozi wa serikali. Hapana. Nasema tena: NOPE!
AminaOna sasa umeshindwa kuthibitisha. Wewe unafikiri JamiiForums inasomwa katika nchi yako tu. Ujumbe wa mada hii unawahusu watu wa nchi zote.