PreGE2025 Yesu hakuwatukana Watawala. Hata aliposikia Yohana amekatwa kichwa, alinyamaza. Kwanini?

PreGE2025 Yesu hakuwatukana Watawala. Hata aliposikia Yohana amekatwa kichwa, alinyamaza. Kwanini?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Rafiki yangu WALOLA VUNZYA
Matusi ni dalili kwamba Biblia unaisoma lakini huielewi au unaisoma lakini hutii unaayoagizwa.

Biblia yako inakuambia kwamba watukanaji wataingia mbinguni? Yangu inaniambia hivi:
I Kor 6:9-10
Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, 10wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi.

HIYO MATHAYO 23 YESU ANAONGEA NA VIONGOZI WA KIDINI(MAFARISAYO NA WAALIMU WA SHERIA) SIO VIONGOZI WA KISIASA.
Waalimu wa Sheria na Mafarisayo ndiyo waliomuuwa Yesu na ndiyo walikuwa maadui wa agano.
 
Endelea tu kutukana halafu subiri siku ya mwisho uone utakavyoingizwa kwenye mateso makali zaidi kuliko haya unayoyapata duniani
SIku ya mwisho ni siku ya kifo chako, achana na upotevu wa fikra ulionao. Mungu aliyemkataza mkristu kuoa wake zaidi ya mmoja eti ndo huyo huyo aliyemruhusu muislamu kuoa wake wa4. Does it make sense??
 
Mleta mada tunajua wewe ni mjinga ila kutuonesha ujinga wako waziwwazi hivi ni kujidhalilisha sana.

Kabla hujapost haya mashudu yako ungeniuliza kwa nini Yesu alimwita mtawala Herode Mbweha.

Ungejua usingetuletea upuuzi wako ulioandika hapa.
Inaonekana wewe husomi uzi wote, unakimbilia kusoma comments. Nimeeleza katika post #3 kwanini Yesu alitumia neno "mbweha". Na-paste hapa maelezo ya post #3
===================
Kuna watu wanadai Yesu alitukana au alimkosea heshima Herod Antipas kwa kumuita “mbweha.” aliposema “Mwambieni yule Mbweha...”
Wananukuu Andiko la Luka 13:32, Yesu aliposema:
“...Nendeni, mkamwambie yule mbweha, Tazama, leo na kesho natoa pepo na kuponya wagonjwa, siku ya tatu nakamilisha kazi yangu.”

Ukichunguza vizuri utaona kuwa hilo halikuwa tusi. Katika tamaduni za Wayahudi, "mbweha" ni mfano wa mtu asiye na nguvu kama simba. Kwa mfano huo alikuwa akiwafundisha wanafunzi wake kuwa Herod Antipas hana nguvu ya kumzuia kukamilisha kazi aliyotumwa na Baba.

Kwahiyo andiko hilo halitupi ruhusa ya kuwatukana viongozi wa serikali. Hapana. Nasema tena: NOPE!
 
Yesu alipokuwa duniani, nchi aliyokuwa akiishi ilikuwa chini ya utawala wa Dola ya Kirumi. Wakati Yesu anazaliwa, Herod the Great, ndiye aliyekuwa Mtawala. Huyo ndiye aliyeamuru watoto wa Bethlehemu wauawe ili Yesu aangamie. Baadaye alitawala Herod Antipas, Mwana wa Herod the Great. Huyu alitawala wakati wa huduma ya Yesu na alikuwa pia na nafasi katika hukumu ya Yesu (Luka 23:7-11). Huyu ndiye aliyeamuru Yohana Mbatizaji auawe (Marko 6:17-28). Pontius Pilate, alikuwa liwali wa Kirumi (gavana) wa Yudea kutoka mwaka 26 hadi 36 BK. Huyu alikuwa na mamlaka ya mwisho ya kisiasa na kisheria katika Yudea. Huyu ndiye aliyemhukumu Yesu atundikwe msalabani, ingawa hakuona kosa lolote kwa Yesu (Mathayo 27, Yohana 18–19).

Katikati ya Watawala hao wa kisiasa, Yesu hakuwahi kuwatukana wala kutumia lugha ya dhihaka dhidi yao.
Katika Yohana 18:36-37 tunaona Yesu akizungumza kwa heshima, hata alipokuwa anapewa hukumu ya kifo.

Katika mafundisho yake, Yesu alionyesha kwamba hata watawala wa kidunia wana nafasi waliyopewa na Mungu kwa sababu fulani. Kwa mfano, watu walipomjaribu kuhusu kulipa kodi kwa Kaisari, Yesu alisema: "Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na ya Mungu mpeni Mungu." (Mathayo 22:21). Hapa Yesu anaonesha kwamba hata mamlaka za kisiasa zinastahili kuheshimiwa.

Viongozi aliowakemea Yesu ni wa kidini(Mafarisayo, Masadukayo na Waandishi) kwa sababu walikuwa wanawapotosha watu kwa mafundisho yaliyo kinyume na mapenzi ya Mungu.

Yesu aliwatahadharisha wanafunzi wake kuwa watachukiwa na kuonewa na watu, lakini hakuwahamasisha wafanye uasi au 'kukinukisha.'

Katika Mathayo 10:16-20 Yesu anawaambia wanafunzi wake wakipelekwa mahakamani au mbele ya watawala wa Kirumi, wawe na busara kama nyoka na wapole kama njiwa.

Katika lile tukio la askari na kundi lililoenda 'kumteka' Yesu, Petro alitoa upanga na kumkata sikio mtumishi wa Kuhani mkuu. Yesu alimuonya Petro na kumwambia arudishe upanga alani mwake, kisha akamponya huyo aliyekatwa sikio!

Yesu hakushabikia matumizi ya nguvu au mashambulizi dhidi ya viongozi, hata wakati huo wa kukamatwa kwake. Hili ni fundisho la wazi kwamba Yesu alipinga ghasia na vurugu dhidi ya wenye mamlaka.

Kumbuka pale msalabani, jinsi Yesu alivyowaombea waliomsulibisha, Mungu awasamehe. Msimamo wa Yesu ulikuwa ni kuhubiri mabadiliko ya moyo(heart reform), na sio mapinduzi ya kisiasa. Alijua kuwa mioyo ya watu ikibadilika, wataacha uovu. Sauli alikuwa mbaya sana, na alifurahia kuona watu wa Mungu wakiuawa, lakini moyo wake ulipofanyiwa reform, alibadilika na kuwa mtu mwema.
Waliotoa amri ya kusurubishwa ni hao hao wanasiasa
 
Inaonekana wewe husomi uzi wote, unakimbilia kusoma comments. Nimeeleza katika post #3 kwanini Yesu alitumia neno "mbweha". Na-paste hapa maelezo ya post #3
===================
Kuna watu wanadai Yesu alitukana au alimkosea heshima Herod Antipas kwa kumuita “mbweha.” aliposema “Mwambieni yule Mbweha...”
Wananukuu Andiko la Luka 13:32, Yesu aliposema:
“...Nendeni, mkamwambie yule mbweha, Tazama, leo na kesho natoa pepo na kuponya wagonjwa, siku ya tatu nakamilisha kazi yangu.”

Ukichunguza vizuri utaona kuwa hilo halikuwa tusi. Katika tamaduni za Wayahudi, "mbweha" ni mfano wa mtu asiye na nguvu kama simba. Kwa mfano huo alikuwa akiwafundisha wanafunzi wake kuwa Herod Antipas hana nguvu ya kumzuia kukamilisha kazi aliyotumwa na Baba.

Kwahiyo andiko hilo halitupi ruhusa ya kuwatukana viongozi wa serikali. Hapana. Nasema tena: NOPE!
Sawa basi tuambie Gwajima kwa maneno aliyoongea amekosea nini? Kuna tusi alitoa?
 
Aliogopa na yeye watakula kichwa, laiti angejua na yeye wanamwinda angetorokea Ethiopia kama wenzake
 
Luka 13:32
"Akawaambia, Nendeni, mkamwambie yule mbweha [Herode], Tazama, leo na kesho natoa pepo na kuponya wagonjwa, siku ya tatu nakamilika."

BTW ukimwambia mtawala kuwa yeye ni dikteta kwa wafuasi wake utahesabiqa kuwa umemtukana hata kama kiukweli ni dikteta.

Vv
Soma post #3 utapata ufafanuzi.
 
Kwa hiyo unamaanisha,no reforms no election Iko poa mkuu!,Safi kabisa
 
BTW ukimwambia mtawala kuwa yeye ni dikteta kwa wafuasi wake utahesabiqa kuwa umemtukana hata kama kiukweli ni dikteta.
Vv
Kwani sheria za nchi yako zinasemaje. Zinakuruhusu kumtukana Mkuu wa nchi?
 
Inaonekana wewe husomi uzi wote, unakimbilia kusoma comments. Nimeeleza katika post #3 kwanini Yesu alitumia neno "mbweha". Na-paste hapa maelezo ya post #3
===================
Kuna watu wanadai Yesu alitukana au alimkosea heshima Herod Antipas kwa kumuita “mbweha.” aliposema “Mwambieni yule Mbweha...”
Wananukuu Andiko la Luka 13:32, Yesu aliposema:
“...Nendeni, mkamwambie yule mbweha, Tazama, leo na kesho natoa pepo na kuponya wagonjwa, siku ya tatu nakamilisha kazi yangu.”

Ukichunguza vizuri utaona kuwa hilo halikuwa tusi. Katika tamaduni za Wayahudi, "mbweha" ni mfano wa mtu asiye na nguvu kama simba. Kwa mfano huo alikuwa akiwafundisha wanafunzi wake kuwa Herod Antipas hana nguvu ya kumzuia kukamilisha kazi aliyotumwa na Baba.

Kwahiyo andiko hilo halitupi ruhusa ya kuwatukana viongozi wa serikali. Hapana. Nasema tena: NOPE!
Kwa hiyo hapa unaweza kumuita Rais Kilaza alafu ukapona?
 
Kwanza asili ya huo msemo unaujua? Au ndiyo kwa mara ya kwanza umemuona Kwa Kristo Yesu?

Yesu aliposema wakristo wawe wapole kama njiwa na werevu kama nyoka wewe ulielewaje?

Kwa ivo Yesu Kristo alikuwa anatetea tawala DHALIMU?
Unaeleza au unauliza?
 
Back
Top Bottom