PreGE2025 Yesu hakuwatukana Watawala. Hata aliposikia Yohana amekatwa kichwa, alinyamaza. Kwanini?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Wewe mbweha acha kutumia maandiko kwa tamaa zako binafsi,hii dunia utaiacha siku ukifa,kumbuka Kuna jehanum ya moto na funza wasiokufa.
 
Umejichanganya vibaya sana kiongoz wa dini lazima ukemeee maovu
 
Yesu alitumwa kutafuta kondoo waliopotea kwa nyumba ya Izrael, alikomaa na hao Mafarisayo na Masufukayo walikuwa wauwaji, wadhulumaji, wanyanyasaji, waonezi. Mbaya zaidi ndio waliopewa jukumu la kusimamia torati, hakutumwa kwa mataifa ambao ndio waliokuwa wanatawala yaani dola ya rumi, na hao warumi ndio waliomfanya Herode kuwa mfalme wa wayahudi, wala herode hakutokana na wayahudi.

Yesu aliwakemea wauwaji(Mafarisayo)

Yesu aliwakemea wanyonyaji(Mafarisayo)

Kumbuka ni Mafarisayo hao hao walifurahi Yohana alipokamatwa, Herode alipomuua Yakobo, Mafarisayo hao ndio waliompiga mawe stefano, Ni Mafarisayo waliolitesa kanisa, wala si serikal ya Rumi, kumbuka hata warumi hawakuona makosa ya Yesu, Pilato alinawa mikono.

Yesu alikemea maovu, na sisi tunapaswa kukemea maovu

Mtu anateka na kuua unataka tuseme ndugu Mheshimiwa unajua kuteka na kuua ni dhambi mbele za Mungu?

Ndugu Mheshimiwa mgeni rasmi unajua kuna rushwa kubwa na ubadhilifu wa fedha umetokea kwenye wizara yako au ofisi yako. Maovu yanakemewa

Acha kutumia maandiko vibaya kufanya siasa za kijinga unazofanya
Una jina la Daudi 1 lakini nadhani hujasoma kisa cha Nabii Nathan jinsi alivyom-approach Mfalme Daudi baada ya kugundua uovu alioufanya. Alim-approach kwa hekima. Alianza na parable. Hakuanza na matusi. Soma Biblia yako kwa makini huku ukimuomba Roho Mtakatifu akufunulie mapenzi yake.

Uzi wangu inaonekana hujausoma wote. Nimeeleza wazi kwamba Yesu aliwakemea viongozi wa kidini(Mafarisayo, Masadukayo, Walimu wa sheria) lakini kamwe hakuwakemea Viongozi wa kisiasa. Soma tena uzi wote. By the way, sheria za nchi yako zinakuruhusu kuwakemea Wakuu wako wa nchi? Kama hazikuruhusu basi usilalamike ukipigwa upanga(Rum 13:4).
 
Ningependa kujua kimoja tu. Kwanini umeamua kuwasemea watawala na sio wafuasi. Setfree inaonekana bright sana lakini bias.
 
Una jina la Daudi 1 lakini nadhani hujasoma kisa cha Nabii Nathan jinsi alivyom-approach Mfalme Daudi baada ya kugundua uovu alioufanya. Alim-approach kwa hekima. Alianza na parable. Hakuanza na matusi. Soma Biblia yako kwa makini huku ukimuomba Roho Mtakatifu akufunulie mapenzi yake.

Uzi wangu inaonekana hujausoma wote. Nimeeleza wazi kwamba Yesu aliwakemea viongozi wa kidini(Mafarisayo, Masadukayo, Walimu wa sheria) lakini kamwe hakuwakemea Viongozi wa kisiasa. Soma tena uzi wote. By the way, sheria za nchi yako zinakuruhusu kuwakemea Wakuu wako wa nchi? Kama hazikuruhusu basi usilalamike ukipigwa upanga(Rum 13:4).
Nimekuuliza Yesu alikuja kwa ajili ya nani?

Eleza ukweli waliokuwa wauaji ni akina nani enzi za Yesu?

Waliokuwa wanatenda maovu ni akina nani?
 
Mbweha sio tusi? Wewe tukikuita mbwa sio tusi? Mfalme mwenye nguvu kama Herode umwite mbweha halafu useme sio tusi ? 😆😆😆😆😆
Au tusi kwako mpaka uambiwe viungo vya siri?
Biblia yako unaisomaje? Herod Antipas angekuwa ametukanwa, Pilato angenena kwamba haoni kosa lolote ndani ya Yesu?
Luka 23:13-15
Pilato akawaita makuhani wakuu, viongozi na watu akawaambia, “Mmemleta huyu mtu kwangu mkamshtaki kuwa anataka kuwapotosha watu. Nimemhoji mbele yenu, na sikuona kuwa ana hatia...Kama mnavyoona, mtu huyu hakufanya jambo lo lote linalostahili adhabu ya kifo.

Ile ilikuwa lugha ya picha na ilikubalika katika utamaduni wa huko Mashariki ya Kati. Sasa mambo ya Israeli ukiyaleta kwenye nchi yako bila kutafakari Yesu alikuwa anaongea na watu gani, usilie ukipata kipondo.
 
Setfree acha hizo hubiri neno la Mungu linavyotakiwa, Bibilia imeeleza wazi Mtoto amheshimu Baba yake na mama yake, na mama au baba hatakiwi kumchokoza mtoto

Maandiko yanasema Haki huinua taifa, acha watu wapambanie haki zao, haki inapiganiwa, Mungu mwenyewe anasema njoo tusemezane unielewe hoja zako niweze kukupa haki yako, wewe nani hutaki watu waeleze hoja zao?
Sijasema usitafute haki. Ila kama unaitafuta haki kwa maguvu, utaumia mwenyewe, maana unayejaribu kupambana naye ana upanga uliohalalishwa na sheria za nchi yako kuwakata wavunja sheria. Soma tena uzi huu ujue jinsi ya kutoa maoni yako kwa Wakuu.
 
Kama hujala mema ya nchi basi hujakubali na kutii(Isaya 1:19)
Mind-setting and Manipulation inayofanywa na Siasa na nduguye Dini ili Watumwa mwendelee kuwa watumiwaji,, hawa jamaa watakuja kwenye kila angle ili kuwapumbaza huku wao wanaendelea kula mema ya Dunia...
 
Nimeishakujibu, kama hujala mema ya nchi soma Isaya
 
Yesu alipokuwa duniani, nchi aliyokuwa akiishi ilikuwa chini ya utawala wa Dola ya Kirumi. Wakati Yesu anazaliwa, Herod the Great, ndiye aliyekuwa Mtawala. Huyo ndiye aliyeamuru watoto wa Bethlehemu wauawe ili Yesu aangamie. Baadaye alitawala Herod Antipas, Mwana wa Herod the Great. Huyu alitawala wakati wa huduma ya Yesu na alikuwa pia na nafasi katika hukumu ya Yesu (Luka 23:7-11). Huyu ndiye aliyeamuru Yohana Mbatizaji auawe (Marko 6:17-28). Pontius Pilate, alikuwa liwali wa Kirumi (gavana) wa Yudea kutoka mwaka 26 hadi 36 BK. Huyu alikuwa na mamlaka ya mwisho ya kisiasa na kisheria katika Yudea. Huyu ndiye aliyemhukumu Yesu atundikwe msalabani, ingawa hakuona kosa lolote kwa Yesu (Mathayo 27, Yohana 18–19).

Katikati ya Watawala hao wa kisiasa, Yesu hakuwahi kuwatukana wala kutumia lugha ya dhihaka dhidi yao.
Katika Yohana 18:36-37 tunaona Yesu akizungumza kwa heshima, hata alipokuwa anapewa hukumu ya kifo.

Katika mafundisho yake, Yesu alionyesha kwamba hata watawala wa kidunia wana nafasi waliyopewa na Mungu kwa sababu fulani. Kwa mfano, watu walipomjaribu kuhusu kulipa kodi kwa Kaisari, Yesu alisema: "Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na ya Mungu mpeni Mungu." (Mathayo 22:21). Hapa Yesu anaonesha kwamba hata mamlaka za kisiasa zinastahili kuheshimiwa.

Viongozi aliowakemea Yesu ni wa kidini(Mafarisayo, Masadukayo na Waandishi) kwa sababu walikuwa wanawapotosha watu kwa mafundisho yaliyo kinyume na mapenzi ya Mungu.

Yesu aliwatahadharisha wanafunzi wake kuwa watachukiwa na kuonewa na watu, lakini hakuwahamasisha wafanye uasi au 'kukinukisha.'

Katika Mathayo 10:16-20 Yesu anawaambia wanafunzi wake wakipelekwa mahakamani au mbele ya watawala wa Kirumi, wawe na busara kama nyoka na wapole kama njiwa.

Katika lile tukio la askari na kundi lililoenda 'kumteka' Yesu, Petro alitoa upanga na kumkata sikio mtumishi wa Kuhani mkuu. Yesu alimuonya Petro na kumwambia arudishe upanga alani mwake, kisha akamponya huyo aliyekatwa sikio!

Yesu hakushabikia matumizi ya nguvu au mashambulizi dhidi ya viongozi, hata wakati huo wa kukamatwa kwake. Hili ni fundisho la wazi kwamba Yesu alipinga ghasia na vurugu dhidi ya wenye mamlaka.

Kumbuka pale msalabani, jinsi Yesu alivyowaombea waliomsulibisha, Mungu awasamehe. Msimamo wa Yesu ulikuwa ni kuhubiri mabadiliko ya moyo(heart reform), na sio mapinduzi ya kisiasa. Alijua kuwa mioyo ya watu ikibadilika, wataacha uovu. Sauli alikuwa mbaya sana, na alifurahia kuona watu wa Mungu wakiuawa, lakini moyo wake ulipofanyiwa reform, alibadilika na kuwa mtu mwema.
Stop manipulating the very Scared Word of God (which has inner unit) to suit your political interest. Stop 😡.

Hujui Yesu alihukumiwa Kwa makosa ya uhaini?
 
Stop kuongea uongo. Yesu hakuwa na kosa lolote. Alikufa kwa ajili ya dhambi zako
 
You are too heritical to fear. Usipotoshe maandiko. Kulinda udhalimu wa watawala. Nao ni binadamu wanahitaji wokovu. It very sad 😭 kupotosha neno la Mungu kiasi hiki
 
Nimepotosha nini. Maandiko yako yanakuambia Yesu alitukana watawala?
 
Yesu alipokuwa duniani, nchi aliyokuwa akiishi ilikuwa chini ya utawala wa Dola ya Kirumi. Wakati Yesu anazaliwa, Herod the Great, ndiye aliyekuwa Mtawala. Huyo ndiye aliyeamuru watoto wa Bethlehemu wauawe ili Yesu aangamie. Baadaye alitawala Herod Antipas, Mwana wa Herod the Great. Huyu alitawala wakati wa huduma ya Yesu na alikuwa pia na nafasi katika hukumu ya Yesu (Luka 23:7-11). Huyu ndiye aliyeamuru Yohana Mbatizaji auawe (Marko 6:17-28). Pontius Pilate, alikuwa liwali wa Kirumi (gavana) wa Yudea kutoka mwaka 26 hadi 36 BK. Huyu alikuwa na mamlaka ya mwisho ya kisiasa na kisheria katika Yudea. Huyu ndiye aliyemhukumu Yesu atundikwe msalabani, ingawa hakuona kosa lolote kwa Yesu (Mathayo 27, Yohana 18–19).

Katikati ya Watawala hao wa kisiasa, Yesu hakuwahi kuwatukana wala kutumia lugha ya dhihaka dhidi yao.
Katika Yohana 18:36-37 tunaona Yesu akizungumza kwa heshima, hata alipokuwa anapewa hukumu ya kifo.

Katika mafundisho yake, Yesu alionyesha kwamba hata watawala wa kidunia wana nafasi waliyopewa na Mungu kwa sababu fulani. Kwa mfano, watu walipomjaribu kuhusu kulipa kodi kwa Kaisari, Yesu alisema: "Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na ya Mungu mpeni Mungu." (Mathayo 22:21). Hapa Yesu anaonesha kwamba hata mamlaka za kisiasa zinastahili kuheshimiwa.

Viongozi aliowakemea Yesu ni wa kidini(Mafarisayo, Masadukayo na Waandishi) kwa sababu walikuwa wanawapotosha watu kwa mafundisho yaliyo kinyume na mapenzi ya Mungu.

Yesu aliwatahadharisha wanafunzi wake kuwa watachukiwa na kuonewa na watu, lakini hakuwahamasisha wafanye uasi au 'kukinukisha.'

Katika Mathayo 10:16-20 Yesu anawaambia wanafunzi wake wakipelekwa mahakamani au mbele ya watawala wa Kirumi, wawe na busara kama nyoka na wapole kama njiwa.

Katika lile tukio la askari na kundi lililoenda 'kumteka' Yesu, Petro alitoa upanga na kumkata sikio mtumishi wa Kuhani mkuu. Yesu alimuonya Petro na kumwambia arudishe upanga alani mwake, kisha akamponya huyo aliyekatwa sikio!

Yesu hakushabikia matumizi ya nguvu au mashambulizi dhidi ya viongozi, hata wakati huo wa kukamatwa kwake. Hili ni fundisho la wazi kwamba Yesu alipinga ghasia na vurugu dhidi ya wenye mamlaka.

Kumbuka pale msalabani, jinsi Yesu alivyowaombea waliomsulibisha, Mungu awasamehe. Msimamo wa Yesu ulikuwa ni kuhubiri mabadiliko ya moyo(heart reform), na sio mapinduzi ya kisiasa. Alijua kuwa mioyo ya watu ikibadilika, wataacha uovu. Sauli alikuwa mbaya sana, na alifurahia kuona watu wa Mungu wakiuawa, lakini moyo wake ulipofanyiwa reform, alibadilika na kuwa mtu mwema.

Luka 13:32
Akawaambia, Nendeni, mkamwambie yule mbweha, Tazama, leo na kesho natoa pepo na kuponya wagonjwa, siku ya tatu nakamilika.
 
Back
Top Bottom