SankaraBoukaka
JF-Expert Member
- Jul 2, 2019
- 3,577
- 5,664
ambalo mimi halinihusu.Kwa mujibu wa Neno la Mungu
ambalo mimi halinihusu.Kwa mujibu wa Neno la Mungu
Yesu alipokuwa duniani, nchi aliyokuwa akiishi ilikuwa chini ya utawala wa Dola ya Kirumi. Wakati Yesu anazaliwa, Herod the Great, ndiye aliyekuwa Mtawala. Huyo ndiye aliyeamuru watoto wa Bethlehemu wauawe ili Yesu aangamie. Baadaye alitawala Herod Antipas, Mwana wa Herod the Great. Huyu alitawala wakati wa huduma ya Yesu na alikuwa pia na nafasi katika hukumu ya Yesu (Luka 23:7-11). Huyu ndiye aliyeamuru Yohana Mbatizaji auawe (Marko 6:17-28). Pontius Pilate, alikuwa liwali wa Kirumi (gavana) wa Yudea kutoka mwaka 26 hadi 36 BK. Huyu alikuwa na mamlaka ya mwisho ya kisiasa na kisheria katika Yudea. Huyu ndiye aliyemhukumu Yesu atundikwe msalabani, ingawa hakuona kosa lolote kwa Yesu (Mathayo 27, Yohana 18–19).
Katikati ya Watawala hao wa kisiasa, Yesu hakuwahi kuwatukana wala kutumia lugha ya dhihaka dhidi yao.
Katika Yohana 18:36-37 tunaona Yesu akizungumza kwa heshima, hata alipokuwa anapewa hukumu ya kifo.
Katika mafundisho yake, Yesu alionyesha kwamba hata watawala wa kidunia wana nafasi waliyopewa na Mungu kwa sababu fulani. Kwa mfano, watu walipomjaribu kuhusu kulipa kodi kwa Kaisari, Yesu alisema: "Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na ya Mungu mpeni Mungu." (Mathayo 22:21). Hapa Yesu anaonesha kwamba hata mamlaka za kisiasa zinastahili kuheshimiwa.
Viongozi aliowakemea Yesu ni wa kidini(Mafarisayo, Masadukayo na Waandishi) kwa sababu walikuwa wanawapotosha watu kwa mafundisho yaliyo kinyume na mapenzi ya Mungu.
Yesu aliwatahadharisha wanafunzi wake kuwa watachukiwa na kuonewa na watu, lakini hakuwahamasisha wafanye uasi au 'kukinukisha.'
Katika Mathayo 10:16-20 Yesu anawaambia wanafunzi wake wakipelekwa mahakamani au mbele ya watawala wa Kirumi, wawe na busara kama nyoka na wapole kama njiwa.
Katika lile tukio la askari na kundi lililoenda 'kumteka' Yesu, Petro alitoa upanga na kumkata sikio mtumishi wa Kuhani mkuu. Yesu alimuonya Petro na kumwambia arudishe upanga alani mwake, kisha akamponya huyo aliyekatwa sikio!
Yesu hakushabikia matumizi ya nguvu au mashambulizi dhidi ya viongozi, hata wakati huo wa kukamatwa kwake. Hili ni fundisho la wazi kwamba Yesu alipinga ghasia na vurugu dhidi ya wenye mamlaka.
Kumbuka pale msalabani, jinsi Yesu alivyowaombea waliomsulibisha, Mungu awasamehe. Msimamo wa Yesu ulikuwa ni kuhubiri mabadiliko ya moyo(heart reform), na sio mapinduzi ya kisiasa. Alijua kuwa mioyo ya watu ikibadilika, wataacha uovu. Sauli alikuwa mbaya sana, na alifurahia kuona watu wa Mungu wakiuawa, lakini moyo wake ulipofanyiwa reform, alibadilika na kuwa mtu mwema.
Kwanini hujasoma uzi wote. Soma post #3 ujue maana ya mbweha. Nyakati zile hilo halikuwa tusi. Ndio sababu Pilato alisema Yesu hakuwa na kosa lolote limpasalo kuuawa.Luka 13:32
Akawaambia, Nendeni, mkamwambie yule mbweha, Tazama, leo na kesho natoa pepo na kuponya wagonjwa, siku ya tatu nakamilika.
Maandiko yako wazi. Alikuja kwa walio wake wakamkataa.
Nilianza kukudharau jinsi unavyoanalyse bible scriptures. Leo umethibitisha kuwa niko sawa. Neno mbwa kwa wayahudi ni tusi. Mbweha ni jamii ya mbwa. Hivyo mbweha ni mbwa.Kuna watu wanadai Yesu alitukana au alimkosea heshima Herod Antipas kwa kumuita “mbweha.” aliposema “Mwambieni yule Mbweha...”
Wananukuu Andiko la Luka 13:32, Yesu aliposema:
“...Nendeni, mkamwambie yule mbweha, Tazama, leo na kesho natoa pepo na kuponya wagonjwa, siku ya tatu nakamilisha kazi yangu.”
Ukichunguza vizuri utaona kuwa hilo halikuwa tusi. Katika tamaduni za Wayahudi, "mbweha" ni mfano wa mtu asiye na nguvu kama simba. Kwa mfano huo alikuwa akiwafundisha wanafunzi wake kuwa Herod Antipas hana nguvu ya kumzuia kukamilisha kazi aliyotumwa na Baba.
Kwahiyo andiko hilo halitupi ruhusa ya kuwatukana viongozi wa serikali. Hapana. Nasema tena: NOPE!
Yesu sio nabii. Yesu ni MunguWanasababu ya kumkataa na zina mashiko.
Hakuna nabii mwoga kwa Yahudi kama Yesu.
Aliwaogopa Warumi na Dola.
Yesu hakuwa na kosa na alikufa kwaajili ya dhambi zetu. Ila mashtaka yake mbele ya Pilato yalikuwa yakiahini kwamba anajifanya Mfalme sawa na Kaisali. Ndio maana walimwambia Pilato usipo msulibisha basi wewe si rafiki ya Kaisari. Pilato akaogopa akamuhukumu.Yesu hakuwa na kosa lolote. Alikufa kwa ajili ya dhambi zako
Wewe mbweha kawaambie mbweha wenzio kuwa hilo neno si la sifa nzuriKwanini hujasoma uzi wote. Soma post #3 ujue maana ya mbweha. Nyakati zile hilo halikuwa tusi. Ndio sababu Pilato alisema Yesu hakuwa na kosa lolote limpasalo kuuawa.
Hiyo mwangi aliitekeleza Kwa vitendo"...akupigaye shavu la kulia, mgeuzie na la kushoto."(Mathayo 5:39).
Yesu sio nabii. Yesu ni Mungu
![]()
Kwanini Yesu anaitwa Mungu? Sababu na ushahidi huu hapa
1. Ushahidi wa Kibiblia Yohana 1:1 – "Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu." Tito 2:13 – "Tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Mungu mkuu na Mwokozi wetu Yesu Kristo." Yesu mwenyewe alikiri kuwa ni Mungu: Yohana 10:30 – "Mimi...www.jamiiforums.com
Sasa mtu kama wewe una maana yoyote ile humu duniani?Wewe mbweha kawaambie mbweha wenzio kuwa hilo neno si la sifa nzuri
Nimeishaeleza njia sahihi ya kutoa maoni kwa Wakuu iwapo mnahitaji reforms. Hayo maneno kwamba "mtakinukisha" ndio yanayowaharibiaNo Reforms No Election si kauli ya kupinga uchaguzi kwa utashi wa kisiasa bali ni wito wa haki na demokrasia ya kweli. Tunadai marekebisho ya msingi katika mfumo wa uchaguzi ili kuhakikisha kila kura ina thamani, na matokeo yanayoakisi sauti ya wananchi
#NoReformsNoElection
Jibu ni fupi tu yesu sio mwanadamu .Yesu alipokuwa duniani, nchi aliyokuwa akiishi ilikuwa chini ya utawala wa Dola ya Kirumi. Wakati Yesu anazaliwa, Herod the Great, ndiye aliyekuwa Mtawala. Huyo ndiye aliyeamuru watoto wa Bethlehemu wauawe ili Yesu aangamie. Baadaye alitawala Herod Antipas, Mwana wa Herod the Great. Huyu alitawala wakati wa huduma ya Yesu na alikuwa pia na nafasi katika hukumu ya Yesu (Luka 23:7-11). Huyu ndiye aliyeamuru Yohana Mbatizaji auawe (Marko 6:17-28). Pontius Pilate, alikuwa liwali wa Kirumi (gavana) wa Yudea kutoka mwaka 26 hadi 36 BK. Huyu alikuwa na mamlaka ya mwisho ya kisiasa na kisheria katika Yudea. Huyu ndiye aliyemhukumu Yesu atundikwe msalabani, ingawa hakuona kosa lolote kwa Yesu (Mathayo 27, Yohana 18–19).
Katikati ya Watawala hao wa kisiasa, Yesu hakuwahi kuwatukana wala kutumia lugha ya dhihaka dhidi yao.
Katika Yohana 18:36-37 tunaona Yesu akizungumza kwa heshima, hata alipokuwa anapewa hukumu ya kifo.
Katika mafundisho yake, Yesu alionyesha kwamba hata watawala wa kidunia wana nafasi waliyopewa na Mungu kwa sababu fulani. Kwa mfano, watu walipomjaribu kuhusu kulipa kodi kwa Kaisari, Yesu alisema: "Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na ya Mungu mpeni Mungu." (Mathayo 22:21). Hapa Yesu anaonesha kwamba hata mamlaka za kisiasa zinastahili kuheshimiwa.
Viongozi aliowakemea Yesu ni wa kidini(Mafarisayo, Masadukayo na Waandishi) kwa sababu walikuwa wanawapotosha watu kwa mafundisho yaliyo kinyume na mapenzi ya Mungu.
Yesu aliwatahadharisha wanafunzi wake kuwa watachukiwa na kuonewa na watu, lakini hakuwahamasisha wafanye uasi au 'kukinukisha.'
Katika Mathayo 10:16-20 Yesu anawaambia wanafunzi wake wakipelekwa mahakamani au mbele ya watawala wa Kirumi, wawe na busara kama nyoka na wapole kama njiwa.
Katika lile tukio la askari na kundi lililoenda 'kumteka' Yesu, Petro alitoa upanga na kumkata sikio mtumishi wa Kuhani mkuu. Yesu alimuonya Petro na kumwambia arudishe upanga alani mwake, kisha akamponya huyo aliyekatwa sikio!
Yesu hakushabikia matumizi ya nguvu au mashambulizi dhidi ya viongozi, hata wakati huo wa kukamatwa kwake. Hili ni fundisho la wazi kwamba Yesu alipinga ghasia na vurugu dhidi ya wenye mamlaka.
Kumbuka pale msalabani, jinsi Yesu alivyowaombea waliomsulibisha, Mungu awasamehe. Msimamo wa Yesu ulikuwa ni kuhubiri mabadiliko ya moyo(heart reform), na sio mapinduzi ya kisiasa. Alijua kuwa mioyo ya watu ikibadilika, wataacha uovu. Sauli alikuwa mbaya sana, na alifurahia kuona watu wa Mungu wakiuawa, lakini moyo wake ulipofanyiwa reform, alibadilika na kuwa mtu mwema.
Wewe Mbweha kawaambie mbweha wenzio hawana faida dunianiSasa mtu kama wewe una maana yoyote ile humu duniani?