Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,238
- 8,194
Yesu alipokuwa duniani, nchi aliyokuwa akiishi ilikuwa chini ya utawala wa Dola ya Kirumi. Wakati Yesu anazaliwa, Herod the Great, ndiye aliyekuwa Mtawala. Huyo ndiye aliyeamuru watoto wa Bethlehemu wauawe ili Yesu aangamie. Baadaye alitawala Herod Antipas, Mwana wa Herod the Great. Huyu alitawala wakati wa huduma ya Yesu na alikuwa pia na nafasi katika hukumu ya Yesu (Luka 23:7-11). Huyu ndiye aliyeamuru Yohana Mbatizaji auawe (Marko 6:17-28). Pontius Pilate, alikuwa liwali wa Kirumi (gavana) wa Yudea kutoka mwaka 26 hadi 36 BK. Huyu alikuwa na mamlaka ya mwisho ya kisiasa na kisheria katika Yudea. Huyu ndiye aliyemhukumu Yesu atundikwe msalabani, ingawa hakuona kosa lolote kwa Yesu (Mathayo 27, Yohana 18–19).
Katikati ya Watawala hao wa kisiasa, Yesu hakuwahi kuwatukana wala kutumia lugha ya dhihaka dhidi yao.
Katika Yohana 18:36-37 tunaona Yesu akizungumza kwa heshima, hata alipokuwa anapewa hukumu ya kifo.
Katika mafundisho yake, Yesu alionyesha kwamba hata watawala wa kidunia wana nafasi waliyopewa na Mungu kwa sababu fulani. Kwa mfano, watu walipomjaribu kuhusu kulipa kodi kwa Kaisari, Yesu alisema: "Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na ya Mungu mpeni Mungu." (Mathayo 22:21). Hapa Yesu anaonesha kwamba hata mamlaka za kisiasa zinastahili kuheshimiwa.
Viongozi aliowakemea Yesu ni wa kidini(Mafarisayo, Masadukayo na Waandishi) kwa sababu walikuwa wanawapotosha watu kwa mafundisho yaliyo kinyume na mapenzi ya Mungu.
Yesu aliwatahadharisha wanafunzi wake kuwa watachukiwa na kuonewa na watu, lakini hakuwahamasisha wafanye uasi au 'kukinukisha.'
Katika Mathayo 10:16-20 Yesu anawaambia wanafunzi wake wakipelekwa mahakamani au mbele ya watawala wa Kirumi, wawe na busara kama nyoka na wapole kama njiwa.
Katika lile tukio la askari na kundi lililoenda 'kumteka' Yesu, Petro alitoa upanga na kumkata sikio mtumishi wa Kuhani mkuu. Yesu alimuonya Petro na kumwambia arudishe upanga alani mwake, kisha akamponya huyo aliyekatwa sikio!
Yesu hakushabikia matumizi ya nguvu au mashambulizi dhidi ya viongozi, hata wakati huo wa kukamatwa kwake. Hili ni fundisho la wazi kwamba Yesu alipinga ghasia na vurugu dhidi ya wenye mamlaka.
Kumbuka pale msalabani, jinsi Yesu alivyowaombea waliomsulibisha, Mungu awasamehe. Msimamo wa Yesu ulikuwa ni kuhubiri mabadiliko ya moyo(heart reform), na sio mapinduzi ya kisiasa. Alijua kuwa mioyo ya watu ikibadilika, wataacha uovu. Sauli alikuwa mbaya sana, na alifurahia kuona watu wa Mungu wakiuawa, lakini moyo wake ulipofanyiwa reform, alibadilika na kuwa mtu mwema.