PreGE2025 Yesu hakuwatukana Watawala. Hata aliposikia Yohana amekatwa kichwa, alinyamaza. Kwanini?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
"...akupigaye shavu la kulia, mgeuzie na la kushoto."(Mathayo 5:39).
Hivi unafahamu kwamba hata yeye alipopigwa hilo shavu la kulia hakugeuza la kushoto badala yake alihoji sababu ya kuchapwa kofi?
Yohana 18:23
[23]Yesu akamjibu, Kama nimesema vibaya, ushuhudie ule ubaya; bali kama nimesema vema, wanipigia nini?
Biblia haisomwi kama magazeti yenu ya udaku.
 
Sikuzote nilijua huna akili kumbe kweli huna hata kidogo....Kuna mhubiri katukana mtawala?
Yesu alikemea njia ovu,wahubiri wanakemea njia ovu....hayo matusi ya kumaniner,waseng€,mbona hatujayasikia kutoka kwa wahubiri?
Au matusi kwenye Ukoo wenu ni kukemea maovu? Lakini sishangai sana,ile mada uliyoleta kwamba wanataka reform wakati mioyo yao hawajareform...nikajua tu enheee
Chawa!
No reform No election.
 
Yesu alipokuwa duniani, nchi aliyokuwa akiishi ilikuwa chini ya utawala wa Dola ya Kirumi. Wakati Yesu anazaliwa, Herod the Great, ndiye aliyekuwa Mtawala. Huyo ndiye aliyeamuru watoto wa Bethlehemu wauawe ili Yesu aangamie. Baadaye alitawala Herod Antipas, Mwana wa Herod the Great. Huyu alitawala wakati wa huduma ya Yesu na alikuwa pia na nafasi katika hukumu ya Yesu (Luka 23:7-11). Huyu ndiye aliyeamuru Yohana Mbatizaji auawe (Marko 6:17-28). Pontius Pilate, alikuwa liwali wa Kirumi (gavana) wa Yudea kutoka mwaka 26 hadi 36 BK. Huyu alikuwa na mamlaka ya mwisho ya kisiasa na kisheria katika Yudea. Huyu ndiye aliyemhukumu Yesu atundikwe msalabani, ingawa hakuona kosa lolote kwa Yesu (Mathayo 27, Yohana 18–19).

Katikati ya Watawala hao wa kisiasa, Yesu hakuwahi kuwatukana wala kutumia lugha ya dhihaka dhidi yao.
Katika Yohana 18:36-37 tunaona Yesu akizungumza kwa heshima, hata alipokuwa anapewa hukumu ya kifo.

Katika mafundisho yake, Yesu alionyesha kwamba hata watawala wa kidunia wana nafasi waliyopewa na Mungu kwa sababu fulani. Kwa mfano, watu walipomjaribu kuhusu kulipa kodi kwa Kaisari, Yesu alisema: "Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na ya Mungu mpeni Mungu." (Mathayo 22:21). Hapa Yesu anaonesha kwamba hata mamlaka za kisiasa zinastahili kuheshimiwa.

Viongozi aliowakemea Yesu ni wa kidini(Mafarisayo, Masadukayo na Waandishi) kwa sababu walikuwa wanawapotosha watu kwa mafundisho yaliyo kinyume na mapenzi ya Mungu.

Yesu aliwatahadharisha wanafunzi wake kuwa watachukiwa na kuonewa na watu, lakini hakuwahamasisha wafanye uasi au 'kukinukisha.'

Katika Mathayo 10:16-20 Yesu anawaambia wanafunzi wake wakipelekwa mahakamani au mbele ya watawala wa Kirumi, wawe na busara kama nyoka na wapole kama njiwa.

Katika lile tukio la askari na kundi lililoenda 'kumteka' Yesu, Petro alitoa upanga na kumkata sikio mtumishi wa Kuhani mkuu. Yesu alimuonya Petro na kumwambia arudishe upanga alani mwake, kisha akamponya huyo aliyekatwa sikio!

Yesu hakushabikia matumizi ya nguvu au mashambulizi dhidi ya viongozi, hata wakati huo wa kukamatwa kwake. Hili ni fundisho la wazi kwamba Yesu alipinga ghasia na vurugu dhidi ya wenye mamlaka.

Kumbuka pale msalabani, jinsi Yesu alivyowaombea waliomsulibisha, Mungu awasamehe. Msimamo wa Yesu ulikuwa ni kuhubiri mabadiliko ya moyo(heart reform), na sio mapinduzi ya kisiasa. Alijua kuwa mioyo ya watu ikibadilika, wataacha uovu. Sauli alikuwa mbaya sana, na alifurahia kuona watu wa Mungu wakiuawa, lakini moyo wake ulipofanyiwa reform, alibadilika na kuwa mtu mwema.
Yesu alitumwa kutafuta kondoo waliopotea kwa nyumba ya Izrael, alikomaa na hao Mafarisayo na Masufukayo walikuwa wauwaji, wadhulumaji, wanyanyasaji, waonezi. Mbaya zaidi ndio waliopewa jukumu la kusimamia torati, hakutumwa kwa mataifa ambao ndio waliokuwa wanatawala yaani dola ya rumi, na hao warumi ndio waliomfanya Herode kuwa mfalme wa wayahudi, wala herode hakutokana na wayahudi.

Yesu aliwakemea wauwaji(Mafarisayo)

Yesu aliwakemea wanyonyaji(Mafarisayo)

Kumbuka ni Mafarisayo hao hao walifurahi Yohana alipokamatwa, Herode alipomuua Yakobo, Mafarisayo hao ndio waliompiga mawe stefano, Ni Mafarisayo waliolitesa kanisa, wala si serikal ya Rumi, kumbuka hata warumi hawakuona makosa ya Yesu, Pilato alinawa mikono.

Yesu alikemea maovu, na sisi tunapaswa kukemea maovu

Mtu anateka na kuua unataka tuseme ndugu Mheshimiwa unajua kuteka na kuua ni dhambi mbele za Mungu?

Ndugu Mheshimiwa mgeni rasmi unajua kuna rushwa kubwa na ubadhilifu wa fedha umetokea kwenye wizara yako au ofisi yako. Maovu yanakemewa

Acha kutumia maandiko vibaya kufanya siasa za kijinga unazofanya
 
Mind-setting and Manipulation inayofanywa na Siasa na nduguye Dini ili Watumwa mwendelee kuwa watumiwaji,, hawa jamaa watakuja kwenye kila angle ili kuwapumbaza huku wao wanaendelea kula mema ya Dunia...
 
Kuna watu wanadai Yesu alitukana au alimkosea heshima Herod Antipas kwa kumuita “mbweha.” aliposema “Mwambieni yule Mbweha...”
Wananukuu Andiko la Luka 13:32, Yesu aliposema:
“...Nendeni, mkamwambie yule mbweha, Tazama, leo na kesho natoa pepo na kuponya wagonjwa, siku ya tatu nakamilisha kazi yangu.”

Ukichunguza vizuri utaona kuwa hilo halikuwa tusi. Katika tamaduni za Wayahudi, "mbweha" ni mfano wa mtu asiye na nguvu kama simba. Kwa mfano huo alikuwa akiwafundisha wanafunzi wake kuwa Herod Antipas hana nguvu ya kumzuia kukamilisha kazi aliyotumwa na Baba.

Kwahiyo andiko hilo halitupi ruhusa ya kuwatukana viongozi wa serikali. Hapana. Nasema tena: NOPE!
Mbweha sio tusi? Wewe tukikuita mbwa sio tusi? Mfalme mwenye nguvu kama Herode umwite mbweha halafu useme sio tusi ? 😆😆😆😆😆
Au tusi kwako mpaka uambiwe viungo vya siri?
 
Setfree acha hizo hubiri neno la Mungu linavyotakiwa, Bibilia imeeleza wazi Mtoto amheshimu Baba yake na mama yake, na mama au baba hatakiwi kumchokoza mtoto

Maandiko yanasema Haki huinua taifa, acha watu wapambanie haki zao, haki inapiganiwa, Mungu mwenyewe anasema njoo tusemezane unielewe hoja zako niweze kukupa haki yako, wewe nani hutaki watu waeleze hoja zao?
 
Nenda kasome vizuri Mathayo Sura ya 23 yoote utaelewa tu na sindano itakuingia vizuri chawa wewe.

Haka ja chawa like hakajui Bible. Hakajui Yesu alikuja hapa kwa mission gani gani.

Pia hakajui kuwa ni Yesu ndiye alikwenda kuleta fujo kwenye soko la watu akapindua meza.
 
YANI SASAHIVI NDIO NMEJUA KUMBE WEWE SIO MLOKOLE NI TAPELI TUU, ULIPOINGIA HUKU HATA ZILE POST ZAKO ZA UONGO NA UKWELI WATU WATAKUSHTUKIA MAPEMA, TAPELI KWENYE MUAMVULI WA DINI
 
Msimamo wa Yesu ulikuwa ni kuhubiri mabadiliko ya moyo(heart reform), na sio mapinduzi ya kisiasa. Alijua kuwa mioyo ya watu ikibadilika, wataacha uovu. Sauli alikuwa mbaya sana, na alifurahia kuona watu wa Mungu wakiuawa, lakini moyo wake ulipofanyiwa reform, alibadilika na kuwa mtu mwema.
 
Yesu alipokuwa duniani, nchi aliyokuwa akiishi ilikuwa chini ya utawala wa Dola ya Kirumi. Wakati Yesu anazaliwa, Herod the Great, ndiye aliyekuwa Mtawala. Huyo ndiye aliyeamuru watoto wa Bethlehemu wauawe ili Yesu aangamie. Baadaye alitawala Herod Antipas, Mwana wa Herod the Great. Huyu alitawala wakati wa huduma ya Yesu na alikuwa pia na nafasi katika hukumu ya Yesu (Luka 23:7-11). Huyu ndiye aliyeamuru Yohana Mbatizaji auawe (Marko 6:17-28). Pontius Pilate, alikuwa liwali wa Kirumi (gavana) wa Yudea kutoka mwaka 26 hadi 36 BK. Huyu alikuwa na mamlaka ya mwisho ya kisiasa na kisheria katika Yudea. Huyu ndiye aliyemhukumu Yesu atundikwe msalabani, ingawa hakuona kosa lolote kwa Yesu (Mathayo 27, Yohana 18–19).

Katikati ya Watawala hao wa kisiasa, Yesu hakuwahi kuwatukana wala kutumia lugha ya dhihaka dhidi yao.
Katika Yohana 18:36-37 tunaona Yesu akizungumza kwa heshima, hata alipokuwa anapewa hukumu ya kifo.

Katika mafundisho yake, Yesu alionyesha kwamba hata watawala wa kidunia wana nafasi waliyopewa na Mungu kwa sababu fulani. Kwa mfano, watu walipomjaribu kuhusu kulipa kodi kwa Kaisari, Yesu alisema: "Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na ya Mungu mpeni Mungu." (Mathayo 22:21). Hapa Yesu anaonesha kwamba hata mamlaka za kisiasa zinastahili kuheshimiwa.

Viongozi aliowakemea Yesu ni wa kidini(Mafarisayo, Masadukayo na Waandishi) kwa sababu walikuwa wanawapotosha watu kwa mafundisho yaliyo kinyume na mapenzi ya Mungu.

Yesu aliwatahadharisha wanafunzi wake kuwa watachukiwa na kuonewa na watu, lakini hakuwahamasisha wafanye uasi au 'kukinukisha.'

Katika Mathayo 10:16-20 Yesu anawaambia wanafunzi wake wakipelekwa mahakamani au mbele ya watawala wa Kirumi, wawe na busara kama nyoka na wapole kama njiwa.

Katika lile tukio la askari na kundi lililoenda 'kumteka' Yesu, Petro alitoa upanga na kumkata sikio mtumishi wa Kuhani mkuu. Yesu alimuonya Petro na kumwambia arudishe upanga alani mwake, kisha akamponya huyo aliyekatwa sikio!

Yesu hakushabikia matumizi ya nguvu au mashambulizi dhidi ya viongozi, hata wakati huo wa kukamatwa kwake. Hili ni fundisho la wazi kwamba Yesu alipinga ghasia na vurugu dhidi ya wenye mamlaka.

Kumbuka pale msalabani, jinsi Yesu alivyowaombea waliomsulibisha, Mungu awasamehe. Msimamo wa Yesu ulikuwa ni kuhubiri mabadiliko ya moyo(heart reform), na sio mapinduzi ya kisiasa. Alijua kuwa mioyo ya watu ikibadilika, wataacha uovu. Sauli alikuwa mbaya sana, na alifurahia kuona watu wa Mungu wakiuawa, lakini moyo wake ulipofanyiwa reform, alibadilika na kuwa mtu mwema.

Una uhakika hayo mambo yalikuwepo?

Una ushahidi?

Usiongee mambo ya kusadikika
 
Unachanganya watawala na Viongozi, Tanzania hatuna watawala bali tuna uongozi; uongozi umekaa hapo ulipo sio kwasababu umesimikwa na nguvu ya ROHO Mtakatifu bali kwa ridhaa na kwa niaba ya Wenye nchi wenyewe ambao ni sisi
Uongozi huanza kujifikiria kama "utawala" pale vichwa vya Wenye nchi wengi kukosa maarifa ya kuuwajibisha (ne wengine kama wewe kujustify ujinga kwa vifungu vya Biblia vinavyoongelea jamii ya watu walioishi jangwani miaka 2000 iliyopita)
 
My friend Allen Kilewella. Asante kwa maoni yako. Ina maana wewe ukipigwa shavu la kulia, unakunja ngumi na kupambana na akupigaye? Au?
Kuna mazingira unajitetea ili kuulinda uhai wako. Uhai ni wenye thamani. Mtu anakubaka huwezi ruhusu aendelee kufanya anachotaka.

Hayo mengine huko juu uko sahihi ila utapopolewa sana
 
Yesu alipokuwa duniani, nchi aliyokuwa akiishi ilikuwa chini ya utawala wa Dola ya Kirumi. Wakati Yesu anazaliwa, Herod the Great, ndiye aliyekuwa Mtawala. Huyo ndiye aliyeamuru watoto wa Bethlehemu wauawe ili Yesu aangamie. Baadaye alitawala Herod Antipas, Mwana wa Herod the Great. Huyu alitawala wakati wa huduma ya Yesu na alikuwa pia na nafasi katika hukumu ya Yesu (Luka 23:7-11). Huyu ndiye aliyeamuru Yohana Mbatizaji auawe (Marko 6:17-28). Pontius Pilate, alikuwa liwali wa Kirumi (gavana) wa Yudea kutoka mwaka 26 hadi 36 BK. Huyu alikuwa na mamlaka ya mwisho ya kisiasa na kisheria katika Yudea. Huyu ndiye aliyemhukumu Yesu atundikwe msalabani, ingawa hakuona kosa lolote kwa Yesu (Mathayo 27, Yohana 18–19).

Katikati ya Watawala hao wa kisiasa, Yesu hakuwahi kuwatukana wala kutumia lugha ya dhihaka dhidi yao.
Katika Yohana 18:36-37 tunaona Yesu akizungumza kwa heshima, hata alipokuwa anapewa hukumu ya kifo.

Katika mafundisho yake, Yesu alionyesha kwamba hata watawala wa kidunia wana nafasi waliyopewa na Mungu kwa sababu fulani. Kwa mfano, watu walipomjaribu kuhusu kulipa kodi kwa Kaisari, Yesu alisema: "Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na ya Mungu mpeni Mungu." (Mathayo 22:21). Hapa Yesu anaonesha kwamba hata mamlaka za kisiasa zinastahili kuheshimiwa.

Viongozi aliowakemea Yesu ni wa kidini(Mafarisayo, Masadukayo na Waandishi) kwa sababu walikuwa wanawapotosha watu kwa mafundisho yaliyo kinyume na mapenzi ya Mungu.

Yesu aliwatahadharisha wanafunzi wake kuwa watachukiwa na kuonewa na watu, lakini hakuwahamasisha wafanye uasi au 'kukinukisha.'

Katika Mathayo 10:16-20 Yesu anawaambia wanafunzi wake wakipelekwa mahakamani au mbele ya watawala wa Kirumi, wawe na busara kama nyoka na wapole kama njiwa.

Katika lile tukio la askari na kundi lililoenda 'kumteka' Yesu, Petro alitoa upanga na kumkata sikio mtumishi wa Kuhani mkuu. Yesu alimuonya Petro na kumwambia arudishe upanga alani mwake, kisha akamponya huyo aliyekatwa sikio!

Yesu hakushabikia matumizi ya nguvu au mashambulizi dhidi ya viongozi, hata wakati huo wa kukamatwa kwake. Hili ni fundisho la wazi kwamba Yesu alipinga ghasia na vurugu dhidi ya wenye mamlaka.

Kumbuka pale msalabani, jinsi Yesu alivyowaombea waliomsulibisha, Mungu awasamehe. Msimamo wa Yesu ulikuwa ni kuhubiri mabadiliko ya moyo(heart reform), na sio mapinduzi ya kisiasa. Alijua kuwa mioyo ya watu ikibadilika, wataacha uovu. Sauli alikuwa mbaya sana, na alifurahia kuona watu wa Mungu wakiuawa, lakini moyo wake ulipofanyiwa reform, alibadilika na kuwa mtu mwema.
Kwa sababu alikuwa anajua wajibu wake na hakuwa tapeli kama Hawa waganga njaa wa saizi
 
Back
Top Bottom