Askofu Gwajima omba msamaha, siku ya mahubiri yako kanisani juu ya utekaji ulimkosea Mungu na Rais

Acha kukufuru hii Nchi ipo katika hali mbaya ya mauaji na utekaji si jambo la kuchezea.
Damu za watu wengi zinamwagika pasipo sababu za msingi yaani tuna lazimisha laana katika Nchi na wengine mnaona ni jambo la kawaida!!
kwani kuna mtu umeona anasapoti utekaji na mauaji? shida ni wapi unasemea huo utekaji.kama uko kanisani au msikitini ,soma kwanza kifungu kutoka Biblia au Quran takatifu ,then endelea na mahubiri yako bila kutaja taasisi au jina la mtu .hapo utakuwa unakemea maovu kweli kweli ukiwa madhabahuni.sasa unaingia kanisani kama msanii then unaanza mambo yako .hii siyo sawa
 
Kecho ikidhibitisha kuwa mkuu wa nchi anausika na utekaji utasemaje? Au wewe ndiye yeye unatambua movement zake zote? Punguza ujuaji
 
Formation ya kanisa ni yake, huenda roho alimuagiza hiyo approach
 
Hoja yangu ni kwamba amewakosea nini?
Makosa yake ni haya
1.kanisa : kuhubiri vile kanisani ilionekana kanisani ni sawa na jukwaa la siasa badala ya kuwa sehemu takatifu ya kuhubiri neno la MUNGU liletao uzima.leo waumini wanahaingika wapate wapi pa kusalia na kufungia ndoa na kufanya ibada ya mazishi nk
kwa rais na mwnekiti wachama,: kumtaja kiaina aina kana kwamba labda nahusika na utekaji .sikiliza video ile .

3.Kwa MUNGU ,kutumika kuhubiri siasa wakati MUNGU amekutuma uhubiri neno la uzima

kosa si kufanya kosa bali kujua umekosea na ukatubu usirudie makosa
 
umesababisha uitwe mtumishi wa shetani na siyo wa Mungu.Hii ni kosa lako kubwa
Kwa hiyo mtu mmoja amkebehi Mungu ila kosa liwe juu ya mwingine?
jifunze kwa YESU .yeye ni mpole na mnyenyekevu
Kama hivi
πŸ‘‡
Luka 13:31
Saa ile ile Mafarisayo kadha wa kadha walimwendea, wakamwambia, Toka hapa, uende mahali pengine, kwa sababu Herode anataka kukuua.

Luka 13:32
Akawaambia, Nendeni, mkamwambie yule mbweha, Tazama, leo na kesho natoa pepo na kuponya wagonjwa, siku ya tatu nakamilika.
 
Mjinga sana wewe. Hiyo Nguvu ungeitumia kumkemea Mtekaji siyo kumkemea anayekemea watekaji. Damu za hao waliopotea zitakutafuna
kuna namna unaweza kuwakemea watekaji ukiwa kanisani na isionekane unagombana na mamlaka iliyokupa kibari cha kuabudu kwa uhusu.uhuru usiyokuwa ni mipaka hiyo ni vurugu
 
usijilinganishe na BWANA wa mabwana ,muumba wa mbingu na nchi.we mwambie rais kuwa ni mbweha uone utakachofanyiwa..
 

Warumi 13:1​


Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu.
 

Hivi kupinga na kukemea uovu na uhalifu siku hizi imekuwa ni Kosa Kisheria hapa Tanzania?
 
Kuna siku utafikiwa tu wewe au ndugu zako usifikiri uko salama sana wewe mwanalumumba.

Yaani anayekemea utekaji ndio awe kisababishi cha machafuko na sio mtekaji na boss wao?

Kutoka maktaba miaka 8 iliyopita jionee

Kutoka Bungeni DODOMA, leo April 10, 2017 Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe alisimama kuomba kutoa taarifa kwa Naibu Spika wa Bunge akitaka Bunge lisimamishe shughuli za kawaida na kuanza kujadili matukio ya utekaji watu yanayoendelea nchini.Bashe amesema yeye pia ameshatumiwa ujumbe wa vitisho wakimwambia kuna watu 11 akiwemo yeye watafanyiwa vitendo vibaya popote watakapokuwa, hivyo analiomba Bunge lijadili suala hilo kwa dharula kwasababu sio sawa kukaa kimya.


View: https://youtu.be/Y0Y24wdT9OI?si=KR5hx9Y7psY5kOqd
 
Huna akili njema.Fumba macho nikuombee maji ya kunywa.
 
Yani aombe msamaha kwa kusema watu wanatekwa? Kwani ni uongo? Hii nchi ina wajinga wengi sana
KWANI ANGEENDA BUNGENI ASINGEWEZA KUKEMEA WATEKAJI?
HAHAHAAHAH
Tuache kutafuta kichaka cha kijifichia.Hamas imejenga mahandaki chi ya hospital ,miskiti na shule kwa sababu sheria za kivita zinatambua maeneo hayo kwamba hayatakiwi kushambuliwa.NETANYAHU akasema washenzi wa kubwa kabisa ,nitawafuata huko huko.sasa na sisi tusifaanye misikiti na makanisa kuwa sehemu ya siasa na kuwakemea viongozi wa nchi.iko siku atakuja kiongozi kichaa atakufuata huko huko
 
Huna akili njema.Fumba macho nikuombee maji ya kunywa.
Biblia au Quran ni sawa na kichaka.ukishika njia moja ( neno moja ) unaweza kujikuta uko shimoni ukabaki unalilia na MUNGU akakushangaa umeingiaje humo😳😳
 
Biblia au Quran ni sawa na kichaka.ukishika njia moja ( neno moja ) unaweza kujikuta uko shimoni ukabaki unalilia na MUNGU akakushangaa umeingiaje humo😳😳
Unahitaji nikuombee maji ya kunywa au tende?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…