Askofu Gwajima: Rais Sio mzalendo namba moja nchini, Mwanajeshi ndio mzalendo namba moja

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Your browser is not able to display this video.
Akizungumza na wananchi, Mbunge wa Jimbo la Kawe kupitia tiketi ya CCM, Askofu Josephat Gwajima amesema Rais sio mzalendo namba moja. Wanajeshi ndio wazalendo namba moja kwa kuwa wanatoa uhai wao ili kuilinda nchi.

Hata hivyo amesema kisiasa Rais anaonekana ni mzalendo namba moja. Nje ya siasa, wanasiasa sio wazalendo. Gwajima ametoa wito wanajeshi walipwe vizuri ili wawe na maisha mazuri kwa kuwa wao wanalinda nchi usiku na mchana.

Amesema haya alipokuwa akizungumzua suala la kuwalinda wakuu wa majeshi ya nchi dhidi ya mamlaka zinazowateua ili wasiwe wanaondolkewa kiholela.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…