Askofu Gwajima: Siasa ni kipaji siyo akili za darasani. Ya siasani hayapelekwi kwenye dini ila kinyume chake ni sahihi

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Askofu Gwajima amesema mtu kuwa mwanasiasa mahiri hakuhitaji kwenda darasani kwani uanasiasa ni kipaji " taranta" Siasa ni swala zima la kuwaletea watu maendeleo ikiwemo maji, umeme, elimu na Huduma za afya na kuyaweza hayo siyo lazima uwende darasani, amesisitiza.

Askofu Gwajima pia amesema kuna tofauti kati ya majukwaa ya kidini na majukwaa ya kisiasa na kwamba mambo ya kisiasa huwezi kuyapeleka kwenye imani za watu ( dini) lakini mafundisho ya dini unaweza kuyapeleka kwenye siasa ili watu wawe na amani na upendo utamalaki.

Chanzo: Channel ten!

Maendeleo hayana vyama!
 
Kwangu mimi naona kura ni mahusiano kura ni affiliation, kura ni mtazamo, kura ni matarajio ya ndani, kura ni falsafa ya wakati husika na abadani kura sio umeme wala maji wala barabara wala Maendeleo kama wengi wanavyoamini.

Kuna watu hupata kura nyingi tu na hawajafanya lolote.

Ndio maana labda wenzetu wanatuambia sauti ya wengi ni sauti ya Mungu maana mwenye kura nyingi halali ndio anatakiwa kuwa mshindi.

Mathalani huu waweza kuwa mjadala mzito eti
 
Nimekuelewa mkuu!
 
Chid kashachemsha aache kutia huruma ,yeye kama alichanganya dini na siasa muwache imcost,kitendo cha kuwatukana waislamu huko nyuma jibu lake atalipata tar 28 oct saa sita mchana tu.
Aliwatukana Waislamu wa wapi bwashee?
 
Chid kashachemsha aache kutia huruma ,yeye kama alichanganya dini na siasa muwache imcost,kitendo cha kuwatukana waislamu huko nyuma jibu lake atalipata tar 28 oct saa sita mchana tu.
Na sijui ile misukule yake pale ubungo ataibebea mbeleko gani maana ameshaikana imani aliyokuwa anaitumia kuwachukulia hela kiboya.
 
Wewe jitoe ufahamu tu mkuu ,clip kibao za kuwatukana waislamu zipo mitandaoni na pia hata ile ya kumla kondoo nayo utasema ipo wapi? Chid HATOBOI Jimbo la kawe wakazi wake wengi wanajielewa.
Askofu Gwajima amechimba visima misikitini wewe unataka kumzushia nini?
 
Mwambie kuwa anajitahidi sana kuupaka rangi upepo ila hatofanikiwa kamwe!!

Ni Heri tusiwe na mbunge kuliko Kuna na mbunge tapeli wa aina yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…