PreGE2025 Askofu Gwajima: Sitayumba, sitabadilika na wala sitabadili msimamo!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kumbe kweli wewe ni chawa.
Kama sio mtekaji kwanini asiungane na gwajima kukemea huo uovu.
 
Unaemtetea mwenyewe ndio yule ajuza ambae kila akifungua mdomo kuongea ni michambo na kejeli tuu hakuna cha maana anaongea, lakini kesi itaamuliwa karibuni tuu
 
Kupinga Utekaji ndio Chuki dhidi ya Samia! Kwahiyo unataka kuiambia Dunia kwamba mtekaji ni Samia?
Mlioa kichwa leo anajuta. Na bado. Haya makanisa yake mawili hapa Jijini Mwanza HAKUNA mbwa inaingia kanisani! Nyambafu!
 
Majibu ya maswali yako
Kabla ya Samia utekaji ulikuwepo
JK aliteka
JPM aliteka na kuua pia
Anachofanya mama ni muendelezo

Mzigo wa utekaji anaangushiwa Rais kwasababu 100% wanaotekwa ni WAKOSOAJI wake
Hata namna serikali inatoa majibu juu ya utekaji huu ni dalili tosha anaye husika ni nani?

Iwapo rais afuataye akiendelea na mtindo huu huu ataendelea kuambiwa UKWELI kwamba anateka na kuua wanao mkosoa


BTW Gwajima hajesema kama anayeteka ni nani
Zaidi nilichosikia ni Gwajima aliyatenganisha haya mambo na Serikali ya chama chake CCM
 
Aiseee
 
Moja ya mahubiri yaletayo faraja kwa waumini ni kuomba Mungu aingilie kati kunusuru watu wasitekwe na kuuawa!
Askofu Gwaji ndiye amejitolea kuhubiri hayo matumaini kwa kumhubiri De-Gwajimanizer aone uchungu,aingilie kati kunusuru watu waliotekwa.
 
Nitajie nchi mojawapo katika afrika ya mashariki ambayo haina mfungwa wa kisiasa gerezani dakika hii, nina uhakika hakuna hata moja.

Kutekwa na kuuwawa ni suala la kidunia mkuu, hakuna nchi ambayo idara za usalama wake hazijawahi kuwa na kesi za utekaji na mauaji, binadamu anavyoishi tegemea kuwepo kwa masuala haya ya kutisha.

Samia anafanya kazi kubwa nchi nzima hahitaji sana kushughulika na hizo kanuni, narudia kukumbusha kwamba waliomo humu mitandaoni hawafiki hata milioni tano nchi nzima, wenye kujua SSH anafanya nini ni milioni zaidi ya 59.

Kusema hatuponi ni upuuzi mwingine sawa na mwingi ambao umeshawahi kuwepo Tanzania hii.
 
Mbona huyo huyo rais anatumia majukwaa ya kisiasa kushambulia viongozi wa kidini ?
 

Propaganda za kijinga. Maza ndiye anaonekana kuwa na hasira na chuki zaidi dhidi ya Gwajima.
 

Ibada ya kweli ya kumtukuza Mungu ni ile ambayo inakemea Uovu na kutukuza HAKI na AMANI kwa Watu wote.

Vitendo vya uhalifu mbaya wa kuteka watu, kuwatesa, kuwabaka, kuwalawiti, kuwajeruhi kwa namna mbalimbali ikiwemo na kuwamwagia tindikali, kuwashambulia kimwili na kihisia, kuwekea sumu, na kuua ni vitendo vya UOVU MBAYA WA SHETANI. Yeyote yule anayetenda vitendo hivi au kuunga mkono vitendo hivi viovu, huyo ndiye SHETANI mwenyewe.
Kutenda au kuunga mkono vitendo hivi Viovu ni kufanya Ibada ya Kumtukuza Shetani, na kupinga Vitendo hivi Viovu ni kufanya Ibada ya Kumtukuza Mungu.

Kati ya hawa Watu wawili ambao umewahusisha kwenye hili bandiko lako, Je, Nani atakuwa ni SHETANI na nani atakuwa ni Malaika wa Mungu kwa jinsi unavyowaona wewe Kutokana na matendo yao hao Watu???
 
Kama hawatekwi na serikali wanatekwa na nani? Mdude yupo wapi? Soka yupo wapi? Amani Manengelo yupo wapi?
 
Ni ipi tofauti ya chuki,ukweli,taarifa na maelezo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…