PreGE2025 Askofu Gwajima: Sitayumba, sitabadilika na wala sitabadili msimamo!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kumbe bado yupo?

CCM ukiingia ni secret society, hutakiwi kutoka ukiwa hai.
 
Lakini huwezi kueleza kwa nini hizo kanuni kwenu zinakuwa ni msahafu.
Huko ndiko kukosa hoja kwenyewe. Mtu kama wewe huwezi kulielewa hili.
Hiyo kanuni kutokuwepo inapunguza vipi matatizo tuliyonayo?. Hivyo vyama vingine vyenye utayari wa kuingia kwenye uchaguzi kwa akili yako vinaongozwa na watu wasiojielewa?.

Mtanzania wa kawaida anazo shida zake nyingi na bahati nzuri CCM wamefahamu namna ya kupambana nazo.
 
Wewe ni mtu wa makamo (kiasi kikubwa); lakini umekuwa kama mtoto mdogo anayeanza kubarehe; sababu tu ya kumpigania Samia? Na sababu kuu ni moja tu, ukiacha ile ya ufisadi anaowawezesha nyinyi kuushiriki.

Hayo yote unayo yaeleza hapo juu ni kama kichwani hakuna kitu chochote.
Vyama vingine vipi, ACT na CUF?
Mtanzania wa kawaida sasa hivi hofu yake kubwa ni kutekwa na kuuliwa akidai HAKI yake ya msingi, kuchagua viongozi wake bila ya kubughudhiwa.

Kwa nini Samia hataki KANUNI za kumwezesha mTanzania huyu kuwa na UHURU na HAKI ya kuchagua kiongozi anayemtaka yeye (hata kama ni huyo huyo Samia)? Unabaki unazungukazunguka tu na mambo mengine ila hilo swali hutaki kulijibu, kwa sababu unajuwa Samia hawezi kubaki madarakani kama hizo kanuni zikiwepo.

Safari hii HAMPONI. Hilo Koti bandia la kuitumia CCM litawabana tu.
 
Badala ya kuwa mahali pa sala, maombezi na faraja kwa waumini, madhabahu ya Askofu Josephat Gwajima yamegeuka kuwa jukwaa la mashambulizi ya wazi dhidi ya Rais Samia Suluhu Hassan, yakisambaza chuki, hofu na hisia kali zisizo na mashiko ya kiroho.

Katika ibada ya Jumapili iliyopita, Gwajima alisikika akisema kwa kujiamini: “Niliwahi kumwambia Rais Samia nikiwa Ikulu kuwa, mtu mwenye hofu ya kupinduliwa tayari amepinduliwa.”

Kauli hii haikutoa maarifa ya kiroho wala hamasa ya kiimani, bali ilionekana wazi kuwa ni dongo la kisiasa lililolenga kuipaka tope Serikali ya Awamu ya Sita mbele ya hadhira ya waumini wake.

Badala ya kuhubiri matumaini, mshikamano wa kitaifa na sala kwa ajili ya maendeleo ya nchi, Gwajima ameendelea kugeuza mimbari kuwa uwanja wa kutupia vijembe, kusambaza jazba na kupandikiza dhana potofu miongoni mwa wananchi.

Katika kauli nyingine isiyopimika kwa mizani ya hekima ya kiroho, alisema: “Wapo wanaodhani ninaogopa kutekwa, lakini hata wakiniteka watakuwa wamechelewa.” Hii si lugha ya kiimani bali ni kejeli inayojenga mazingira ya taharuki na hofu ya kutungwa. Ni sauti ya mtu anayeona yuko juu ya taasisi, sheria na hata ukweli wa hali halisi.

Inashangaza kuona Gwajima akiwa kimya kabisa kwenye mambo muhimu yanayogusa maisha ya kila siku ya Watanzania kama mfumuko wa bei duniani, ajira kwa vijana, huduma za afya kwa mama na mtoto au mapambano dhidi ya dawa za kulevya.

Lakini kila mara linapokuja suala la kumshambulia Rais Samia huibuka na maneno yenye ujasiri wa ajabu, hali inayoibua maswali kuhusu malengo halisi ya hotuba zake.

Kwa miaka sasa Gwajima ameacha majukumu ya kiroho aliyokabidhiwa. Amechagua kuwa mwanasiasa wa majukwaa ya mitandaoni anayejificha nyuma ya joho la askofu huku akihubiri hofu, fitna na mivurugano.

Amebakiza sauti ya uchochezi na kiburi cha kisiasa badala ya uzito wa kiroho unaopaswa kumwongoza kiongozi wa dini.
 
Attachments

  • IMG-20250606-WA0038.jpg
    IMG-20250606-WA0038.jpg
    70.5 KB · Views: 18

Katika kauli nyingine isiyopimika kwa mizani ya hekima ya kiroho, alisema: “Wapo wanaodhani ninaogopa kutekwa, lakini hata wakiniteka watakuwa wamechelewa.” Hii si lugha

ya imani bali ni kejeli inayojenga mazingira ya taharuki na hofu ya kutungwa. Ni sauti ya mtu anayeona yuko juu ya taasisi, sheria na hata ukweli wa hali halisi.

Inashangaza kuona Gwajima akiwa kimya kabisa kwenye mambo muhimu yanayogusa maisha ya kila siku ya Watanzania kama mfumuko wa bei duniani, ajira kwa vijana, huduma za afya kwa mama na mtoto au mapambano dhidi ya dawa za kulevya.

Lakini kila mara linapokuja suala la kumshambulia Rais Samia huibuka na maneno yenye ujasiri wa ajabu, hali inayoibua maswali kuhusu malengo halisi ya hotuba zake.

Kwa miaka sasa Gwajima ameacha majukumu ya kiroho aliyokabidhiwa. Amechagua kuwa mwanasiasa wa majukwaa ya mitandaoni anayejificha nyuma ya joho la askofu huku akihubiri hofu, fitna na mivurugano.

Amebakiza sauti ya uchochezi na kiburi cha kisiasa badala ya uzito wa kiroho unaopaswa kumwongoza kiongozi wa dini.
Chawa 🚮🚮
 
Hapo ni pipa na mfuniko vimekutana, hayupo wa kutetewa, mmoja mimbarini mwingine kwenye bibi na bwana.

yaani ni kama mzee yusufu na yule mtoto wa adija kopa marehemu
 
Hivi kwa nini mara zote chuki zake ni dhidi ya viongozi wa nchi wanaotokana na dini ya kiislamu tu?
 
Mandela aliitwa gaidi na akafungwa miaka 27 kisa kupigania haki za South Africans, Mandela alikuwa kwenye watch list ya magaidi nchini USA, walikuja kumtoa kwenye hio list mwaka 2008 , kule DRC zamani Zaire Patrice Lumumba aliyeyushwa kwenye acid kisa tu kukosoa uongozi wa Mobutu...

Yesu mwenyewe aliuawa kikatili mbele ya watu...

Ukifikiri hayo matukio yote utagundua kitu.. Miaka hio dola hizo zilitumia propaganda kuwachafua kwanza wapigania haki , wakosoaji na wasema kweli na baadae baada ya propaganda kuwaingia vilivyo wananchi basi walipata nguvu kuwatendea ubaya watu hao mbele ya raia...

Muda unavyokwenda uongo hua unayeyuka na kupotea kama barafu iliyowekwa kwenye maji moto... na ukweli huwa unachomoza taratibu kama jua lichomozalo alfajiri , kuangaza nuru na kulikimbiza giza....

Hapa duniani hakuna kipya...
Na kila jambo lina mwisho..
 
Kupinga Utekaji ndio Chuki dhidi ya Samia! Kwahiyo unataka kuiambia Dunia kwamba mtekaji ni Samia?
Ndugu ww una Hakika gani wanaotekwa wote wanatekwa na Serikali !!!

kwasasa ata Kenya kuna matatizo tena makubwa zaid ata uko Marekani pia kuna Utekaji !!!

lkn kote uko Akuna shutuma kwa Rais wa nchi kwann utekaji wa TZ mnataka mum bebeshe zigo Rais wa nchi !!!

kabla ajawa RAIS SAMIA akukuwa na utekaji ??

ukisoma msg zenu ni wazi kuna kachuki ndani yake japo kunawakati nikama Ukweli mnaujua !!!

mtu anasema ivi tulidhani Utekaji ulikuwa unafanywa na JPM RIP lkn sasa JPM ayupo na Utekaji unaendelea kumbe Mtekaji mwenyewe atakuwa uyu sio JPM !!¿¿

kwaiyo tuwaamini ndio uyu !!??

maswali ma3 naomba mjibu moja RAIS SAMIA kabla ajawa ata Makamu Rais je nchini kwetu akukuwa na Utekaji ???

Sasa nyinyi CHADEMA mnataka tuwaamini RAIS SAMIA ndio mtekaji kwa Ushaidi upi ???

mwisho CHADEMA tunaomba mtuakikishie je baada ya RAIS SAMIA SULUHU HASSAN kumaliza muda wake 2030 RAIS mpya ajae amtamuusisha na Utekaji !!??

mana zigo ili mlimtupia Rais JPM sasa limekuwa la RAIS SAMIA uko mbele litakuwa la uyo ajae kumbe niww sio SAMIA???

Chama ichi CHADEMA ndio tuseme mmekosa Sera za kuwaambia Wananchi mmekwamia kwenye Utekaji tu ndio Sera yenu !!!??

Ivi nikweli Watanzania milion 60+ tatizo lao ni Utekaji tu awana matatizo mengine ya Msingi !!?

Au CHADEMA mnadhani mnafanya Siasa na watoto pekeyao mbona sisi watu wazima mnatushangaza namna mnafanya Siasa zenu kwenu turufu ni Utekaji tu !!!

na kuvunja Sheria ili mkamatwe ndio SIASA za kumkomboa Mtanzania kweli.. !!!

kama sasa Uchaguzi pia amtaki yani mmechagua kufanya Siasa za Ujanja Ujanja tu kama kisa cha Fisi na mkono wa Binadam !!!

daaaa sisi watu wazima tunawaonea Uruma tu ujumbe wangu kwenu ni uwo.

GWAJIMA naye kashindwa kuwatumikia wana Kawe pia alikuwa Bubu akiwa Mjengoni kwa Utalatibu wa CCM wewe ufai kwenda Bungeni !!!

GWAJIMA akachagua kuamsha Dude na Waumini wake Wanamshangilia Siasa zasasa za ajaju sana,,,,.
 
Badala ya kuwa mahali pa sala, maombezi na faraja kwa waumini, madhabahu ya Askofu Josephat Gwajima yamegeuka kuwa jukwaa la mashambulizi ya wazi dhidi ya Rais Samia Suluhu Hassan, yakisambaza chuki, hofu na hisia kali zisizo na mashiko ya kiroho.

Katika ibada ya Jumapili iliyopita, Gwajima alisikika akisema kwa kujiamini: “Niliwahi kumwambia Rais Samia nikiwa Ikulu kuwa, mtu mwenye hofu ya kupinduliwa tayari amepinduliwa.”

Kauli hii haikutoa maarifa ya kiroho wala hamasa ya kiimani, bali ilionekana wazi kuwa ni dongo la kisiasa lililolenga kuipaka tope Serikali ya Awamu ya Sita mbele ya hadhira ya waumini wake.

Badala ya kuhubiri matumaini, mshikamano wa kitaifa na sala kwa ajili ya maendeleo ya nchi, Gwajima ameendelea kugeuza mimbari kuwa uwanja wa kutupia vijembe, kusambaza jazba na kupandikiza dhana potofu miongoni mwa wananchi.

Katika kauli nyingine isiyopimika kwa mizani ya hekima ya kiroho, alisema: “Wapo wanaodhani ninaogopa kutekwa, lakini hata wakiniteka watakuwa wamechelewa.” Hii si lugha ya kiimani bali ni kejeli inayojenga mazingira ya taharuki na hofu ya kutungwa. Ni sauti ya mtu anayeona yuko juu ya taasisi, sheria na hata ukweli wa hali halisi.

Inashangaza kuona Gwajima akiwa kimya kabisa kwenye mambo muhimu yanayogusa maisha ya kila siku ya Watanzania kama mfumuko wa bei duniani, ajira kwa vijana, huduma za afya kwa mama na mtoto au mapambano dhidi ya dawa za kulevya.

Lakini kila mara linapokuja suala la kumshambulia Rais Samia huibuka na maneno yenye ujasiri wa ajabu, hali inayoibua maswali kuhusu malengo halisi ya hotuba zake.

Kwa miaka sasa Gwajima ameacha majukumu ya kiroho aliyokabidhiwa. Amechagua kuwa mwanasiasa wa majukwaa ya mitandaoni anayejificha nyuma ya joho la askofu huku akihubiri hofu, fitna na mivurugano.

Amebakiza sauti ya uchochezi na kiburi cha kisiasa badala ya uzito wa kiroho unaopaswa kumwongoza kiongozi wa dini.
all in all, aliyekosa ni gwajima, waumini wake makanisa 2000 hawajaongea chochote kwenye madhabahu, angeadhibiwa gwajima (kama ana kosa) waumini waruhusiwe kuendelea kusali, ni haki yao kikatiba, hawajavunja katiba wala sheria, serikali kufuta usajili ni attack ya moja kwa moja kwenye imani za watu hasa wakristo na hatujui atakayefuata ni nani kwasababu waziri wake kwa kujipendekeza amesema wataanza kutathmini makanisa, kwa nini watathmini makanisa ila hawatakuja kutathmin misikiti? target yao ni makanisa tu

Nilichosikitika ni pale bimkubwa anavyozidi kujiaivisha na hajui kama anajianika. kumtukana gwajima kuwa ni mtumishi wa shetani wakati ana wafuasi wengi sana, makanisa zaidi ya 2000 wote wapiga kura hao na wanamwamini, ni jambo la ajabu sana. halafu kwa mlokole, mtu asiyeamini kama mama na wengine kupanga nani wa shetani nani wa Mungu ni kichekesho kwa sababu mlokole yeyote awe wa gwajima au la huamini waislam na wasio walokole ni watumishi wa shetani.
 
Badala ya kuwa mahali pa sala, maombezi na faraja kwa waumini, madhabahu ya Askofu Josephat Gwajima yamegeuka kuwa jukwaa la mashambulizi ya wazi dhidi ya Rais Samia Suluhu Hassan, yakisambaza chuki, hofu na hisia kali zisizo na mashiko ya kiroho.

Katika ibada ya Jumapili iliyopita, Gwajima alisikika akisema kwa kujiamini: “Niliwahi kumwambia Rais Samia nikiwa Ikulu kuwa, mtu mwenye hofu ya kupinduliwa tayari amepinduliwa.”

Kauli hii haikutoa maarifa ya kiroho wala hamasa ya kiimani, bali ilionekana wazi kuwa ni dongo la kisiasa lililolenga kuipaka tope Serikali ya Awamu ya Sita mbele ya hadhira ya waumini wake.

Badala ya kuhubiri matumaini, mshikamano wa kitaifa na sala kwa ajili ya maendeleo ya nchi, Gwajima ameendelea kugeuza mimbari kuwa uwanja wa kutupia vijembe, kusambaza jazba na kupandikiza dhana potofu miongoni mwa wananchi.

Katika kauli nyingine isiyopimika kwa mizani ya hekima ya kiroho, alisema: “Wapo wanaodhani ninaogopa kutekwa, lakini hata wakiniteka watakuwa wamechelewa.” Hii si lugha ya kiimani bali ni kejeli inayojenga mazingira ya taharuki na hofu ya kutungwa. Ni sauti ya mtu anayeona yuko juu ya taasisi, sheria na hata ukweli wa hali halisi.

Inashangaza kuona Gwajima akiwa kimya kabisa kwenye mambo muhimu yanayogusa maisha ya kila siku ya Watanzania kama mfumuko wa bei duniani, ajira kwa vijana, huduma za afya kwa mama na mtoto au mapambano dhidi ya dawa za kulevya.

Lakini kila mara linapokuja suala la kumshambulia Rais Samia huibuka na maneno yenye ujasiri wa ajabu, hali inayoibua maswali kuhusu malengo halisi ya hotuba zake.

Kwa miaka sasa Gwajima ameacha majukumu ya kiroho aliyokabidhiwa. Amechagua kuwa mwanasiasa wa majukwaa ya mitandaoni anayejificha nyuma ya joho la askofu huku akihubiri hofu, fitna na mivurugano.

Amebakiza sauti ya uchochezi na kiburi cha kisiasa badala ya uzito wa kiroho unaopaswa kumwongoza kiongozi wa dini.
Samia amejipanga pamoja na wauaji, watekaji, wabakaji. Hata hajawakemea.

Amempa Gwajima nafasi ya kuonekana anakemea utekaji, uuaji na ubakaji.

Katika macho ya Watanzania wengi ndivyo inavyoonekana hivyo.
 
Ni muda sahihi kwa Tanzania kuwa na sheria inayozuia hate speech, Kenya ziliwagharimu 2007.
 
Back
Top Bottom