Askofu Gwajima, umekosea kujifanya mwamba na mwanaume, uwe mfano kwa jamii na heshimu familia yako. Uliyofanya na unayoyatetea si sahihi

field marshall1

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2017
Posts
1,171
Reaction score
2,732
Nimefuatilia kwa karibu majibu machafu na ovyo ya huyo Gwajima (siamini kama kweli ni mchungaji au askofu mwenye karama), Kama kweli ni mchungaji kuna ethics zake, ni upumbavu na upuuzi kujitapa kuwa hata kama amelala na mrembo yule kwani kuna shida gani?

Hivi ni wewe unayehubiri kanisani neno la Mungu na kumdharau mke wako na familia yako? Huo si ubabe bali ni ujinga uliokomaa kupita kiasi. Kwa hiyo mafundisho yako ya dini yana-based wapi? Kwa watu kusaliti ndoa zao?

Sasa una tofauti gani na asie na dini huku ukijidai wewe ni askofu? Kama kweli wewe ni kiongozi wa dini, unapaswa uwe na ile moral behavior na ujali pia ethics za kazi zako.

Unachokifanya kinaendelea kukushushia heshima kiasi kwamba huna tofauti na wengine wenye tabia za kishenzi na kipuuzi.

Hufai kwa lolote wewe mchungaji au askofu Gwajima, huna adabu, wala hekima na pia hujitambui. Sitaki kuongelea mengi kukuhusu ila bottom line ni kuwa hufai.
 
Amekosa sifa za kuitwa Askofu.

Asome; 1 Timotheo 3:2 na Tito 1.7

Askofu anatakiwa awe mume wa mke mmoja, asisemwe kwa mambo mabaya, asiwe mtu wa hasira, asipende ugomvi, awe mwenye busara na kiasi, na asiejipendekeza.
 
" Gwajiboy hapingi chanjo, anasimamia hoja zile zile zilizosimamiwa na wizara ya afya awamu iliyopita kukataa chanjo.

Sasa Gwajiboy ana hoji huo utafiti umefanyika lini hadi kuhalalisha kuwa hizi chanjo ni salama? Ile kamati ya kumshauri mh Rais ndio ilifanya utafiti kwa muda ule kweli?

Hata mimi binafsi naona wataalam wetu wengi wanajibu maswali kupitia madesa yaliyopo mitandaoni hasa sites za chanjo na CDC ambayo yalikuwepo hata mwaka jana na bado tuliyapinga kisayansi!

Hivi pamoja na upunguani wa Gwajiboy unafikiri wanaweza kufanya nae mdahalo? Hushtuki why hafanyiwi mahojiano kutoa maoni yake?

Hizi chanjo issue si Tanzania tu, ni mgogoro dunia nzima jinsi zilivyoibuka haraka bila kufanyiwa majaribio na kuchunguza madhara yake ya muda mrefu hasa kwa aina ya contents zake si za kutumika bila utafiti wa muda mrefu na hapo ndio natamani wataalam wetu wafafanue na sio porojo za sarafu kugandia.

Kwamba wazungu wamechanja na sisi tuchanje ni hoja mfu ambazo hata mababu zetu pamoja na uprimitive wao wasingekubali. Kule ushoga ni kawaida na umepitishwa kisheria kama ndoa zingine! Na sisi tuige kwavile wana akili na technology kutuzidi?

Jana Gwajima amehoji, hivi hao wanaochoma wamepimwa kwanza? Kule vijijini je? Kuna ufuatiliaji wa walio chanja ili wataalam wetu wajue namna ya kumanage madhara kama yatatokea? Huko kwa wenzetu wana utaratibu bora wa afya hata kabla ya chanjo, huku twende hivyo hivyo?"

Kosa lake Ni Nini?
 
Mwenyezi Mungu amesha muacha zamani, sasa anatapapa kama mfa maji...
Anataka kumpasua waziri vipandevipande anaomba ushauri kwa baba. Baba anatoa ruksa. Nikarejea andiko "' ...asulubiwe.." hii si sawa. Lakini kondoo zake wanashangilia. Hakika tz kuna vituko!
 
Kawaida ya askofu anapiga kimoja jumapili ila watu watahangaika wiki nzima kuchomoa ila hawawezi, jpili tena anapiga kingine! Hamumuwezi kabisa. Huu ni wakati wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…