Askofu Gwajima: Viongozi wa dini hatupingi chanjo ya Corona wala Sayansi bali tunataka tujiridhishe kwanza

Askofu Gwajima: Viongozi wa dini hatupingi chanjo ya Corona wala Sayansi bali tunataka tujiridhishe kwanza

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima ambaye pia ni Mbunge wa Kawe amesema viongozi wa dini hawapingi chanjo ya Corona bali wanashangazwa kwa namna chanjo hiyo ilivyotafitiwa kwa muda mfupi sana

Askofu Gwajima amesema watakubali kupokea chanjo endapo patafanyika utafiti wa kutosha utakaobainisha chanjo hizo hazina madhara kwa binadamu

Askofu Gwajima alikuwa anahojiwa na Esther Kahumbi wa BBC

Chanzo: BBC Dira ya Dunia

Maendeleo hayana vyama!
 
Tafiti zaidi ni muhimu..
E586E3DB-75A2-456A-8EFB-EFDD8FDF8188.jpeg
 
Askofu wa kanisa la ufufuo na uzima ambaye pia ni mbunge wa Kawe amesema viongozi wa dini hawapingi chanjo ya Corona bali wanashangazwa kwa namna chanjo hiyo ilivyotafitiwa kwa muda mfupi sana.
Enhee, ameanza kujileta taratibu. Halafu asiseme viongozi wa dini, aseme viongozi wa dini tuliozuia sayansi kuchukua nafasi yake! Maana tunawajua waliozuia na waliohamasisha, asijiweke kwenye kundi lisilomuhusu
 
Gwajima amekwishavumbua chanjo ipi mbadala wa Astrazeneca?

Pia msitutoe relini wanyonge wanamuulizia mtetezi wao yuko wapi?
 
Hayo mamlaka ya kuwa msemaji wa viongozi wote kidini nani kampa yeye angezungumzia kwa huduma yake maana hatujasikia maazimio hayo ya viongozi wa kidini
 
Wakati huohuo Somalia imeanza kuchanja Raia wake
Tukumbuke hili Taifa liko kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe na ni lenye serikali dhaifu
 
Viongozi wa dini na nani, aseme yeye na dini yake asitujumlishe isitsohe yeye si kiongozi wa dini bali ni kiongozi wa kawe jimbo
 
Astra zenecca,ni chanjo yenye kifo ndani yake.yaani ni sawa na kusainishwa,upasuaji wa kichwa,ambao 50/50,kupona ama ku rip.
 
Enhee, ameanza kujileta taratibu. Halafu asiseme viongozi wa dini, aseme viongozi wa dini tuliozuia sayansi kuchukua nafasi yake! Maana tunawajua waliozuia na waliohamasisha, asijiweke kwenye kundi lisilomuhusu
Kwani mwanzo kulikuwa na taarifa gani? Walikataa chanjo?
 
Huyo Askofu mwanasiasa wakati wake wa kurudi kanisani umewadia sasa, aliewabeba hayupo tena.
 
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima ambaye pia ni Mbunge wa Kawe amesema viongozi wa dini hawapingi chanjo ya Corona bali wanashangazwa kwa namna chanjo hiyo ilivyotafitiwa kwa muda mfupi sana.

Askofu Gwajima amesema watakubali kupokea chanjo endapo patafanyika utafiti wa kutosha utakaobainisha chanjo hizo hazina madhara kwa binadamu

Askofu Gwajima alikuwa anahojiwa na Esther Kahumbi wa BBC

Source BBC Dira ya Dunia

Maendeleo hayana vyama!

Gwajima sio kiongozi wa dini bali ni mfanyabiashara haramu aliyejificha kwenye dini. Asubiri kwanza mwenye kiburi tumalize mambo yake ndio atajua corona ni babalao.
 
Back
Top Bottom