Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Morogoro Jacob Mameo Ole Paulo, akiongea katika ibada ya Ijumaa Kuu katika usharika wa Ifakara Mjini, ametoa wito kwa serikali kuangalia upya malalamiko ya watu juu ya Tume Huru katika uchaguzi wa mwaka 2025.
"Manung'uniko ya Tume Huru ni kilio sasa katika taifa letu sio kwa uchaguzi huu tu ni hata katika chaguzi zilizotangulia, kwamba uchaguzi sio huru na wala sio wa haki. Tuwaombe watawala waliangalie hilo, kwa sababu kuongoza kwa kufanya haya yanayolalamikiwa sio kutuleta pamoja lakini ni kutugawa pia. Ukigawa taifa na nguvu inagawanyika pia,"
"Watanzania wengi wanalalamikia Tume Huru ya Uchaguzi kwamba sio Tume Huru na wanafanya hivyo kwa matukio yaliyotokea nyuma. Ni wajibu wa serikali kuangalia upya malalamiko ya watu wake."
"Wenzetu CHADEMA wanasema 'no reform, no election' hata baadhi ya wana-CCM wako wanaosema 'no reform, no election', lakini wamejificha hawataki waonekane. Na wakati mwingine haya mambo yanayolalamikiwa yanatoka ndani ya chama tawala yanakwenda kwenye vyama vya upinzani. kwa hiyo tunatakiwa pia tujiangalie, tujihojihivi na sisi tunaolalamika ndani ya chama tawala tunakwenda wapi, tunataka nini."
Pia, Soma: Askofu Mameo: Taifa lirudi katika misingi ya Haki, agusia Tume Huru, na 'No Reforms' asema Ikulu imegeuka kuwa sehemu ya lawama