PreGE2025 Askofu Jacob Mameo: Hata baadhi ya wana-CCM wako wanaosema 'no reform, no election', lakini wamejificha hawataki waonekane

PreGE2025 Askofu Jacob Mameo: Hata baadhi ya wana-CCM wako wanaosema 'no reform, no election', lakini wamejificha hawataki waonekane

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Ngoja kwanza CHAWA na baadhi ya Masheikh ubwabwa waone hiki kilichoandikwa hapa! Watakuja na porojo za udini, badala ya kujibu hoja.
Wewe unawaita Masheikh ubwabwa lkn ujuwe kuna Masheikh wengi tu ndio walikuwa wakisema miaka mingi tu ya nyuma Wamewekwa ndani hao Maskofu wanasema leo kwa kuwa Rais sio upande wao ndio ukweli kuna mmoja alisema kitu wakati wa awamu ya 5 watu wamepotea wamepigwa risasi walikuwa wapi
 
Kuna watu utawasikia no reform no election ukimuuliza reform gani anataka hana jibu washazowea ubishi wa Simba na Yanga
 
Wewe unawaita Masheikh ubwabwa lkn ujuwe kuna Masheikh wengi tu ndio walikuwa wakisema miaka mingi tu ya nyuma Wamewekwa ndani hao Maskofu wanasema leo kwa kuwa Rais sio upande wao ndio ukweli kuna mmoja alisema kitu wakati wa awamu ya 5 watu wamepotea wamepigwa risasi walikuwa wapi
Wewe utakataa! Lakini ukweli ndiyo huo. Kuna baadhi ya Masheikh, na hasa wale wa Bakwata hawana mchango wowote ule kwenye kutetea haki za kiraia. Ni Masheikh wa Shura ya Maimamu tu wakiongozwa na Sheikh Ponda Issa Ponda, ndiyo wamekuwa mstari wa mbele kutetea haki.

Na ukija kwenye hoja yako ya kusema eti "Maaskofu (wa Katoliki - TEC) wanasema leo kwa kuwa Rais siyo upande wao..." ni hoja yenye upotoshaji ndani yake! Kwa sababu hakina awamu ambayo Maaskofu wa Katoliko waliacha kukemea maovu kwa sababu Rais wa awamu hiyo ni mwenzao!

Wakati wa utawala wa awamu ya 5, Maaskofu walitishwa, na hata baadhi yao (mfano Askofu Severine Niwemugizi, aliyekuwa rais wa TEC) alifikia mpaka hatua ya kusumbuliwa na uhamiaji kwa kisingizio siyo Mtanzania! Chanzo cha hizo figisu, ni baada ya kutoa Waraka ambao uliikosoa serikali kwa kukandamiza haki za binadamu, kuwanyanyasa wapinzani, nk.

Mwisho kabisa nikukumbeshe tu; linapokuja suala la kupigania haki kwenye nchi yetu, ni vizuri tukaacha kujificha kwenye kichaka cha udini au chama cha siasa.


Kwa ufupi tu, mimi ni mwanachama wa ccm! Lakini siungi mkono uonevu na dhuluma wanazofanyiwa wapinzani kwenye hio nchi! Kwa sababu na wenyewe ni Watanzania. Na hivyo wana haki sawa na Watanzania wengine walioko ccm.
 
Kuna watu utawasikia no reform no election ukimuuliza reform gani anataka hana jibu washazowea ubishi wa Simba na Yanga
Ni kosa kubwa sana miaka yote wananchi ni wajinga, lakini pia hawaoni dhuluma wanayofanyiwa na serikali pamoja na ccm nyakati za uchaguzi.

Kuanzia kwenye utaratibu wa kitoto wa kuwaengua kwenye uchaguzi wagombea wa vyama vya upinzani kwa kisingizio cha kukosea kujaza fomu! wasimamizi wa huo uchaguzi kujificha wakati wagombea wa upinzani wanaporejesha fomu!

Hakuna mwananchi asiyetambua ya kuwa wasimamizi wa huo uchaguzi (Ma DED) na mkurugenzi wa tume ya uchaguzi na maafisa wengine wote; wanateuliwa na mwenyekiti wa chama tawala, na ambaye pia ni Rais na mgombea kwenye huo uchaguzi! Na sifa za kuwateua hao watu huwa hazihojiwi na mtu/mamlaka yoyote ile!
Kwa mantiki hiyo Rais mara zote huteua watu ambao ni watiifu kwake, na ambao hawawezi kwenda kinyume na matakwa yake!

Sasa inapotokea Chadema inawaamsha watu watambue uonevu unaofanywa na serikali ya ccm, mnamkamata mwenyekiti wake na kumbambikia kesi ya uhaini! Ili tu kumnyamazisha! Hii haitasaidia chochote.
Kwa sababu wananchi wanafahamu ili uchaguzi uwe huru na wa haki, tunatakiwa tuwe na tume huru ya uchaguzi! Na siyo hiii ya kuteuliwa na mgombea wa chama tawala.
 
Back
Top Bottom