PreGE2025 Askofu Jacob Mameo: Hata baadhi ya wana-CCM wako wanaosema 'no reform, no election', lakini wamejificha hawataki waonekane

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Morogoro Jacob Mameo Ole Paulo, akiongea katika ibada ya Ijumaa Kuu katika usharika wa Ifakara Mjini, ametoa wito kwa serikali kuangalia upya malalamiko ya watu juu ya Tume Huru katika uchaguzi wa mwaka 2025.

"Manung'uniko ya Tume Huru ni kilio sasa katika taifa letu sio kwa uchaguzi huu tu ni hata katika chaguzi zilizotangulia, kwamba uchaguzi sio huru na wala sio wa haki. Tuwaombe watawala waliangalie hilo, kwa sababu kuongoza kwa kufanya haya yanayolalamikiwa sio kutuleta pamoja lakini ni kutugawa pia. Ukigawa taifa na nguvu inagawanyika pia,"

"Watanzania wengi wanalalamikia Tume Huru ya Uchaguzi kwamba sio Tume Huru na wanafanya hivyo kwa matukio yaliyotokea nyuma. Ni wajibu wa serikali kuangalia upya malalamiko ya watu wake."

"Wenzetu CHADEMA wanasema 'no reform, no election' hata baadhi ya wana-CCM wako wanaosema 'no reform, no election', lakini wamejificha hawataki waonekane. Na wakati mwingine haya mambo yanayolalamikiwa yanatoka ndani ya chama tawala yanakwenda kwenye vyama vya upinzani. kwa hiyo tunatakiwa pia tujiangalie, tujihojihivi na sisi tunaolalamika ndani ya chama tawala tunakwenda wapi, tunataka nini."

Pia, Soma: Askofu Mameo: Taifa lirudi katika misingi ya Haki, agusia Tume Huru, na 'No Reforms' asema Ikulu imegeuka kuwa sehemu ya lawama

Your browser is not able to display this video.
 
Sidhani maana KWA wanaCCM wengi kwao Chama ni chanzo cha mapato. Wakijifanya kuleta fyokofyoko wanajua wanaarika umasikini wa kujitakia
 
Wamejificha,hawataki waonekane.chama kinachishi nao hakijawaona ila chama kingine kilicho nje kimewaona.siasa bila uongo sio siasa.
 
Ngoja kwanza CHAWA na baadhi ya Masheikh ubwabwa waone hiki kilichoandikwa hapa! Watakuja na porojo za udini, badala ya kujibu hoja.
 
Kwani tangu lini wana CCM wakakubaliana Kwa Kila jambo?
CCM mwenyekiti ndio supreme leader wewe hulijui hilo?

Fuatilia yaliyowakuta kuanzia kwa Oscar Kambona, Bibi Titi Mohamed, Horace Kolimba , Benard Membe, na karibuni zaidi Nape Nnauye na January Makamba.
 
Kwa hiyo hao waoiga kelele watabadilisha kipi kama unajua Mwenyekiti ndio Kila kitu? Zitaishia kuwa kelele kama za Chadomo na TEC.

Ieleweke wakati Mbowe ni Mwenyekiti KKKT ndio walikuwa wanasapoti Chadomo.

Leo hii mtu wao kashika chama wanamtumia ku push ajenda zao za dini na madaraka
 
Kwa hiyo hao waoiga kelele watabadilisha kipi kama unajua Mwenyekiti ndio Kila kitu?
Mbona unajicontradict?

Umesema mwanzo "kwani CCM wote wanafanana mawazo"

Halafu ghafla mtu wa CCM akitoa mawazo kinzani wewe unamuita "mpiga kelele"?

Wenye maoni tofauti CCM unajua kinachowakuta.
 
Mbona unajicontradict?

Umesema mwanzo "kwani CCM wote wanafanana mawazo"

Halafu ghafla mtu wa CCM akitoa mawazo kinzani wewe unamuita "mpiga kelele"?

Wenye maoni tofauti CCM unajua kinachowakuta.
Ndio ni kelele tuu hizokwa sababu Hazina tofauti na za Wapinzani na wal no on cares Kwa sababu Mwenyekiti ndio alfa na omega.
 
Ndio ni kelele tuu hizokwa sababu Hazina tofauti na za Wapinzani na wal no on cares Kwa sababu Mwenyekiti ndio alfa na omega.
Kwahiyo na wewe umekubali ni mpiga kelele wa mama Abdul uliyehitimu na kuwa kunguni mkuu sasa unaelekea kuwa vuvuzela hata akiamka akasema siku za wiki zimekuwa 4 na sio 7 utasema ndio na zidumu fikra za mwenyekiti?
 
Ndio, Tupo Wengi.
Reforms zitasaidia hadi CCM kuwe na chaguzi za haki
 
Mengi yamesemwa
 
Mbona unajicontradict?

Umesema mwanzo "kwani CCM wote wanafanana mawazo"

Halafu ghafla mtu wa CCM akitoa mawazo kinzani wewe unamuita "mpiga kelele"?

Wenye maoni tofauti CCM unajua kinachowakuta.
😀😀anajichanganya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…