Askofu Kilaini achemsha kwa ushauri huu!

Kilaini si tatizo. Yeye ni binadamu mmoja kama wengine anayetoa maoni. Tatizo nilishawahi kueleza ni malezi ya waumini wa dini karibu zote ikiwemo katoliki. Asilimia kubwa ya waumini wanaamini kitu cha ajabu kinachoitwa utii. Akisema jambo padri au askofu basi tunadanganyana kwamba hilo linatakiwa kutii. Maaskofu wakisema tuchague chama fulani basi tunadhani tuwe watii kwa hilo.

Tumeona humu jinsi tunavyoendelea kubushana kuhusu Katoliki walivyoanzisha waraka wa uchaguzi. Kuna baadhi ya wakatoliki wanaamini kuwa ni jambo la kutii. Hivi ukatoliki unatufundisha tumfikie Mungu au kuchagua watu.

Nilisema hapa wakatoliki wakazanie kuelimisha katekism yao na sheria zao kwa waamini ili wawe mfano wa kufundisha haki baadhi hawakunielewa. Lini ulimsikia Kilaini akitangaza kwamba wakatoliki nunueni Katekism. Lini ulisikia anahimiza wakatoliki wenzake.

Mtamamshi mengi ya maaskofu yaweza kuwa ni ya kisiasa zaidi kuliko imani zao. Haishangazai waumini kuwa na uelewa mdogo wa dini zao kwa sababu priority siku hizi ndizo hizi matamshi yao kila leo.

mimi narudi kulekule, viongozi watakase makanisa yao kabla ya kutoa maoni kwa taasisi zingine serikali au dini zingine eti kwa vile zina waumini wachache.

Ukristu wenyewe ulianza na waumini 12 wale wafuasi wa Yesu.
 

Nadhani unatatizo la conceptualization ndo maana uka chukua baadhi ya maelezo na kutaka kuyapindisha to suit your desire ili uendeleze ubishi. kama nia yako ni kujenga na si kubomoa ungejitahidi kuelewa na si kukariri. Maana unapokua mbishi na wakutopenda kuelewa context bali ku inteprete lines and not comprehensively understanding issues basi sina lakukusaidia zaidi ya kukuacha na wenye busara hawatajibizana na wewe bali watakupa ushindi unaoutaka na hivyo watakuambia tumekubali huku wakiwa wamekupuuza na wewe ukishangilia nimewashinda.

Sometimes doctors use knives to cut diseases not because they hate patients but because they love them and hate the disease.
 

Mazee hizo statements zako mbili ulizoanza nazo nakubaliana nazo na zina-overwrite yote uliyoandika baada ya hapo, ingawa kwa bahati mbaya au nzuri hujalifahamu hili.

Nimeona unataka kuleta mambo ya kwenye thread nyingine yenye maudhui tofauti na kuichomeka hapa. Sasa tusiigeuze thread iwe kama ngoma ya walevi, ni vyema tukaenda step by step kuzichungulia hoja zinazoletwa badala ya kuleta 'theories of everything' at a go.
 

Mkuu,
NImefanya makusudi kabisa kuleta unachodhani ni thread nyingine. Kilaini angekuwa mtu wa kawaida na si askofu hakuna ambaye angejadili. Hii thread isingekuwa ndefu hivi. Tunamjadili kwa sababu nyuma yake kuna waumini ambao wanaamini kuwa yeye ni mtu wa kumtii. Kwamba utii ndiyo dini ya kweli.

Serikali zinalijua hili na ndiyo maana haikurupuki hata askofu au sheikh akichemka kwelikweli. Huenda wengi hamjaliona.

Kilaini angekuwa ni askofu wa America wala asingejadiliwa na dini zingine. Wakatoliki wenzake wangemshughuliki mara moja kwa maoni na thread kama hizi. Huko hawadanh=ganyiki na ile kitu inayoitwa utii.

Naomba mnielewe.
 

Ok..sasa naona tunarudi kwenye mada. Sasa onesha ni wapi unadhani amepotoka au 'amechemsha' kama mleta thread anavyodai. Mijadala inabidi iwe case specific ..tunaenda kwenye general information provided tunahitaji kufanya hivyo mazee. Sio kuogelea kwenye bahari tusiyojua kina chake. Hilo la utii tuliweke pembeni kwanza kwa sababu halipo hapa anyway.
 

lol..i knew ad hominem will be your only way out. Mazee hoja hujibiwa kwa hoja sio hisia wala vioja. Sasa nadhani utakuwa umeshajua upande wa pili wa shilingi unafananaje..

Shukran.
 

Kachemsha aliposema makanisa yenye waumini 200. Kuna mawaziri waliwahi kuapa bila Biblia au Quran. Sijui dini yao wako wangapi. Huenda hawafiki hata 100.

Kilaini hakuchagua ukatoliki eti kwa sababu ina waumini wengi. Hivi leo ukatoliki ukibaki na waumini 200 atasema lugh hiyohiyo?
 

Nashukuru sana kusema vyema kuliko ambavyo ningesema mimi pengine ingeconfuse zaidi. Kilaini kama askofu mkuu msaidizi wa kanisa lenye namba kubwa ya wakristo Tanzania staement yake ina effect kubwa kwa ukristo kwa maana pana na si dhehebu analolioongoza na chochote kitakacho sababisha constrain katika ibaada ya kikristo kwakujua au kutokujua itasababisha effect kubwa kwenye imani nzima ya ukristo na si ukatoliki tu. Kama kutakua na sheria zozote zaidi ya ile inayosema kila RAIA ana uhuru wa kuamini anachotaka bila kuvunja sheria ya nchi then Kilaini akapigania kulink the term "KANISA" to the sheria mama ya kuabudu asingezungumzia idadi ya watu wanaotakiwa kuunda kanisa na kama kuna idadi basi angesaidia kuondoa hiyo contrain ili kuweka huru uinjilishaji maana kila mtu ata hubiri injili ili imfikie kila mmoja:kiumbe bila kuvunja sheria ya nchi. Then si kazi ya Kilaini kuona raia wana vunja au kuheshimu katiba hiyo ni kazi ya serikali na ina njia za kufanya hivyo. Yeye kwa upande wake angesaidia ku impert traits za uaminifu ndani ya souls za raia ili kazi ya serikali iwe rahisi kitu ambacho ndo jukumu kubwa la kanisa la Kikristo wengine mi sijui kwani sijawahi kuwa na imani tofauti na ukristo. na hapo hakuna mwingiliano bali complimentarity. lakini kwakua dini zikaanzisha institutions zao zinazofanana na instituion za Serikali kwa lengo lao binafsi na si kueneza Injili ndo maana mimi nika draw conclusion kuwa hiyo nikwamba ili hiyo instituion i exist basi lazima kuwe na member and anything inayo hatarisha member kuondoka kwenda kujoin instituion/organization nyingine lazima wenye hizo institutions watatumia nguvu zao direct or indirect kulinda interests zao which are far from what they claim to be interested with yaani kueneza injili.

Kazi ya kueneza injili haitakufa hata makanisa ya katoliki na upentekoste ya futike kama katiba haitaondoa uhuru wa kila raia kuabudu na kwahiyo basi serikali pia hata ikifuta kodi mi naona sawa kama in case wataweza kutoa huduma kwa raia wake. Ila tu haya makanisa yasisingizie number kuwa ndo kigezo cha udhibiti wa kulipa kodi. Mbona kuna maduka mengi tu na bado yanalipa kodi? Je kuna maduka ya ushirika tu au hata mtu mmoja anaweza kuanzisha na bado serikali haishindwi ku exempt or to make them pay kodi? Je sisi wafanyakazi wa serikali tunaopata exemption ya kodi kwenye kuagiza magari je tunahitaji kuunda ushirika ili tusipate mwanya wa kutokulipa kodi? So let us not confuse people na kuficha interests zetu behind kwakisingizio ambacho hata huhitaji degree kujua ukweli wake ni upi.
 



Ok binafsi siamini kuwa kuna uhusiano baina ya usahihi wa imani na idadi ya watu wanaoamini ,sidhani mara zote kuna correlation. Hata hivyo wengi wetu hapa kwa sababu ya hisia au pengine chuki, mmehusisha huu mfano wa waumini 200 na usahihi wa imani ya hao waumini. Kana kwamba Kilaini kasema kanisa lenye watu 200 limepotoka. Hili suala la tafsiri sasa kama mtu anadhania hivyo sidhani kama kuna la kufanya.

Nilivyommuelewa Kilaini kuwa alikuwa akizungumzia ktk suala zima la vigezo wakati wa usajili wa makanisa kwenye vyombo vya serikali. Binafsi sijui kiwango cha chini cha waumini kinachohitajika ili kanisa liandikishwe. Mwenye kujua ni vyema akalisema hili ili tusiendelee kujaza thread based on hisia.
 

Mkuu,
Kanisa Katoliki lilianza na Yesu kwa mitume 12 tu. Kwa maana hiyo Yesu angeanzisha Kanisa hilo hapa nchi leo hii basi kwa mawazo ya Kilaini lingedhibitiwa mara moja.
 
Mkuu,
Kanisa Katoliki lilianza na Yesu kwa mitume 12 tu. Kwa maana hiyo Yesu angeanzisha Kanisa hilo hapa nchi leo hii basi kwa mawazo ya Kilaini lingedhibitiwa mara moja.

Mazee tulishatoka kwenye general information..we are now working on details..to be exact..detail. Sasa tusirudi tena kwenye general information. Tatizo lililopo mbele yetu ni je, ni idadi ipi ya chini ya waumini ambayo ni valid kuwezesha kanisa kusajiliwa kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Hapo ndipo tulipo mazee, tusirejee tena nyuma , tutachanganyana.
 
Mimi sikubaliani na ushauri wa Kilaini. Kwanza naona ushauri huu unaenda kinyume na katiba ya nchi yetu inayoruhusu uhuru wa kuabudu kwa kuzingatia sheria za nchi. Halafu, nani anampa Kilaini mamlaka ya kuamua kanisa flani ni halali na kanisa flani ni batili? Nani anaweza kuipa serikali mamlaka hayo? Hayo mamlaka ni ya Mungu tu! Kilaini, kwa kupitia serikali, anajaribu kujipa mamlaka ya Mungu kitu ambacho kwangu mimi hakikubaliki.

Tukija kwenye kodi, kwa mtazamo wangu dhana ya "msamaha wa kodi" ni dhaifu mno na inapingana na misingi ya kodi inayotetea haki (tax system should be fair). Serikali ikisharuhusu msamaha wa kodi kwa watu, kampuni au taasisi flani hapo inajenga ubaguzi na kuweka maksudi mianya ya kukwepea kodi. Ni jambo linaloeleweka dunia nzima tangu enzi za biblia kwamba watu hawapendi kulipa kodi. Kukisha kua na ubaguzi/upendeleo katika ulipaji wa kodi, ni dhahiri watu watafanya kila namna wanufaike na msamaha huo. Kama leo Tanzania Taasisi za Kidini, Kampuni za Migodi na Kampuni za kigeni zinasamehewa kodi, ni dhahiri watu wengi watafungua makampuni/taasisi zinazofanana na hizi ili kunufaika na huo msamaha wa kodi.

Uamuzi wa awali wa serikali wa kufuta misamaha ya kodi kwa makampuni na taasisi zote ulikua sahihi. Lakini kwasababu serikali ni dhaifu, imeshinikizwa na hizi taasisi na kampuni kufuta uamuzi wake wa awali. Na bado hizi taasisi za kidini na makampuni yanaendelea kuihemea (dictating) serikali iendelee kulinda maslahi yao ya kifedha kama inavyodhihirishwa na matamshi ya Askofu Kilaini. Hizi taasisi na kampuni zinataka kutengeneza "monopolies" na "cartels" kwenye misamaha ya kodi. Kama serikali "inafunikwa" na hizi taasisi na makampuni kwenye utoaji wa huduma kwa jamii, kwanini iendelee kuwepo? Inakusanya kodi ili ijilipe mishahara tu?

Serikali inabidi ijirekebishe. Itoze kodi halali kwa watu, makampuni na taasisi zote bila ubaguzi/upendeleo na itumie hayo mapato ya kodi kutoa huduma za jamii zinazoridhisha. Lasi hivyo ni bora tulipe kodi kwa Taasisi za kidini na makampuni ya kigeni ili yatoe huduma za jamii za kuaminika zaidi.
 

Wakuu, msitoane macho mnajadili dini na makanisa. Mambo yote yako kwenye pesa. Kinachogombewa hapa ni kodi yetu.
 

Ushauri unakwenda kinyume cha katiba.? Sikuelewi hapa. Mi nadhani actually anaitumia ipasavyo haki yake ya kikatiba ya uhuru wa kutoa maoni. Sasa wewe ndugu kama unaona the glass is half-empty kumbuka wengine wanaichukulia glass hiyohiyo kuwa ipo half-full. Pili sioni ni kwa jinsi gani mamlaka ya Mungu inataka kutekwa na Kilaini. Inashangaza hujui kuwa kila kanisa inabidi liandikishwe na serikali na bila kukidhi masherti katu hutosajiliwa..sasa hilo hulioni ..ila Kilaini akitoa maoni unang'aka...
 
Mkuu,
Kanisa Katoliki lilianza na Yesu kwa mitume 12 tu.

Si vizuri sana kutoa hadharani fact ambazo huna uhakika nazo ndugu yangu......yaani Kanisa lilianza na mitume 12 tu.....Hivi hawa mitume walikuja nyakati gani za historia ya kanisa? Kule kny agano la kale hakukuwa na kanisa?

Confirm facts zako kabla hujazimwaga.....utaharibu ndugu yangu!
 
 

Naaaam. Uhuru nnaozungumzia uliotolewa na katiba ni wa kuabudu. Utaratibu wa kuandikisha makanisa ni 'formality' tu, si mchujo. Kama katika kuandikisha makanisa/taasisi zingine zitachujwa basi hiki kitendo ni kinyume na kipengele cha katiba kinachotoa uhuru wa kuabudu. Askofu Kilaini anapendekeza moja ya vigezo vya kutokuandikisha taasisi ya dini iwe idadi ya waumini. Kama watu wawili wameamua wanataka kuabudu mawingu na katika hili hawavunji sheria yoyote ya nchi, wanastahili kunyimwa haki yao kikatiba ya kuabudu? Mkuu huoni 'contradiction' hapa?

Natambua Askofu Kilaini, kama mimi na wewe, ana haki ya kikatiba ya kusema analotaka ilimradi hamkwazi mtu.
 

Loo!! mtu akitaja tu Kanisa Katoliki unaguswa kweli na kuja juu ile mbaya. Badilisha jina basi..
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…