The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Askofu Mkuu wa Kanisa la Menonite Tanzania, Askofu Nelson Kisare, ameishauri Serikali pamoja na viongozi wa dini kuweka mifumo bora ya kuwasikiliza Vijana na kuwapa nafasi ya kutoa maoni yao, badala ya kutumia nguvu kubwa katika kuwanyamazisha.
Askofu Kisare ametoa kauli hiyo jana, Desemba 17, 2025 wakati wa semina iliyoandaliwa na Kanisa la Menonite Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation, iliyofanyika katika Manispaa ya Musoma, Mkoani Mara.
Amesema kuwa endapo vijana watasikilizwa kwa dhati na wanasiasa wakaacha tabia ya kuwatumia kwa maslahi binafsi na baadaye kuwatelekeza, hatua hiyo itasaidia kujenga upya jamii ya Watanzania yenye upendo, mshikamano na amani ya kudumu.
“Vijana wanapaswa kusikilizwa. Hakuna haja ya kutumia nguvu kubwa kuwanyamazisha kundi hili. Lisiposikilizwa, linaweza kuwa bomu kubwa baadaye. Ni vyema viongozi wa dini na Serikali wakawasikiliza ili kujenga usawa na kuondoa malalamiko pamoja na manung’uniko yao,” amesema Askofu Kisare.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku, amesisitiza umuhimu wa kulinda amani na utulivu wa Taifa, akibainisha kuwa migogoro inapaswa kutafutiwa suluhu kwa njia ya mazungumzo badala ya hatua zinazoweza kusababisha taharuki kwa jamii.