Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Askofu mkuu wa kanisa la Pentekoste Tanzania na mwenyekiti wa baraza la makanisa ya kipentekoste Tanzania, Peter Konki amewasilisha mada ya umoja na mshikamano katika kongamano la viongozi wa dini kumshukuru Mungu kwa maisha ya hayati John Magufuli ambalo Rais Samia Suluhu alikuwa Mgeni Rasmi
Askofu Peter amesema;
''Nimeona kwenye mitandao ya jamii baadhi ya wanasiasa wakimsifia mama Samia, Rais wa sasa na kutoa kashfa juu ya utendaji wa Rais aliepita, Magufuli. Hii ni kuonyesha namna ya kujipendekeza ili waangaliwe katika nafasi fulani fulani ya uteuzi tena nasema ni unafki mbaya sana.
Watu hawa wanafanya hivyo kwa kutugawa watanzania, tunaanza kushambuliana kwenye mitandao, tumetoka kwenye msiba, wanaturudisha msiba mwengine. Hayari Magufuli ni kipenzi cha watanzania wengi kwahivyo wanasiasa msitugawanye
Natoa Rai kwa wanasiasa wanaohubiri siasa ya chuki waache ili tuendeleze Taifa letu'' Alimaliza Askofu Konki huku akishangiliwa kwa nguvu na hadhira iliyohudhuria na Rais Samia kumpigia makofi