Askofu Machumu wa Gwajima asema Kanisa lao halijafungwa, waapa kurejea kanisani Jumapili

Askofu Machumu wa Gwajima asema Kanisa lao halijafungwa, waapa kurejea kanisani Jumapili

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Askofu Maximillian Machumu wa Kanisa la Askofu Gwajima, Glory Of Christ Tanzania Church amesema Jumapili wataendelea na Ibada kama kawaida kwasababu Kanisa lao halijafungiwa

"Nafasi ya kujitetea hatujapewa, kwahiyo tuna-confirm wazi kwamba Kanisa letu halijafungwa na kwasabau hiyo kwa kuwa halijafungwa Jumapili tunaendelea na Ibada kama kawaida"

==

Wakati kesi iliyofunguliwa na kanisa la Glory of Christ Tanzania Church ikiendelea katika Mahakama Kuu Masjala ya Dodoma, uongozi wa kanisa hilo umesema kanisa lililotajwa kufungiwa na Msajili wa Jumuiya za Kiraia sio lao, bali ni Glory of Christ Church.

Juni 2 Msajili wa Jumuiya za Kiraia, Emmanuel Kihampa alitangaza kulifuta kanisa hilo linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima kwa kile alichoeleza limekiuka Sheria ya Jumuiya Sura ya 337, kwa kutoa mahubiri yenye mwelekeo wa kisiasa na nia ya kuichonganisha Serikali na wananchi.

Hata hivyo, Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari leo jijini Dodoma baada ya kesio hiyo, Naibu Katibu wa kanisa hilo, Askofu Maximilian Machumu maarufu Mwanamapinduzi amesema tangazo hilo la Msajili haliwahusu kwani kanisa linalozungumziwa sio lao, hivyo aamewataka waumini wao wafike kanisani Jumapili kuendelea na ibada kama kawaida.

 

Attachments

  • 6093972-c5707f31f99db92b41a05d24ef2b2525.mp4
    56.9 MB
Yupo sahihi ufufuo ni taasisi na sio gwajima.
Watoe ufafanuzi.
Anafungiwa gwajima au ufufuo na uzima ni vitu viwili tofauti
 
Ushahidi kuwa ameyasema hayo maneno uko wapi mkuu?

Au unatuona mandezi na kwamba unatuweza! 😎.

Anyway , HALLELUJAH!!
 

Wakati kesi iliyofunguliwa na kanisa la Glory of Christ Tanzania Church ikiendelea katika Mahakama Kuu Masjala ya Dodoma, uongozi wa kanisa hilo umesema kanisa lililotajwa kufungiwa na Msajili wa Jumuiya za Kiraia sio lao, bali ni Glory of Christ Church.

Juni 2 Msajili wa Jumuiya za Kiraia, Emmanuel Kihampa alitangaza kulifuta kanisa hilo linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima kwa kile alichoeleza limekiuka Sheria ya Jumuiya Sura ya 337, kwa kutoa mahubiri yenye mwelekeo wa kisiasa na nia ya kuichonganisha Serikali na wananchi.

Hata hivyo, akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari leo jijini Dodoma baada ya kesio hiyo, Naibu Katibu wa kanisa hilo, Askofu Maximilian Machumu maarufu Mwanamapinduzi amesema tangazo hilo la Msajili haliwahusu kwani kanisa linalozungumziwa sio lao, hivyo aamewataka waumini wao wafike kanisani Jumapili kuendelea na ibada kama kawaida.

Tazama video:
 
Waende wapassuliwe ndio watajua lilisajiliwa kanisa au gwajima

USSR
 
20250529_075443~2.jpg
 
Back
Top Bottom