Tetesi: Askofu Maximilian Machumu anatishiwa maisha kutokana na kupinga bandari kuuzwa kwa Waarabu

Tetesi: Askofu Maximilian Machumu anatishiwa maisha kutokana na kupinga bandari kuuzwa kwa Waarabu

uwe hodari

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2022
Posts
4,045
Reaction score
8,608
Askofu Maximilian Machumu akiwa miongoni mwa aliyeshiriki mkutano wa Temeke kupingwa uuzwaji wa bandari za nchi kwa waarabu maisha yake yapo hatarini

Baada ya mkutano wa juzi watu wasiojulikana walimfuata kwake Kibaha hawakumkuta, Walipomkosa walienda ofisini kwake kuvunja mipango na madirisha ila hawakumkuta
....
Dr.slaa


My take

Watanganyika tuamke, kama hadi viongozi wa dini wanatishiwa maisha vipi kwa sisi wananchi wa kawaida?

Maisha ya askofu kuwa hatarini kwasababu ya kupinga bandari kuuzwa sio inshara nzuri
Taifa litaanguka

Serikali isianze kuharibu amani ya nchi ilyojengwa na Nyerere
 
Hizi sarakasi mie sizielew mara kupinga bandari kuuzwa kwa muarabu mara mwarabu sio mbaya vipengele vya mkataba virekebishwe Jamani kwani tatizo ni mkataba urekebishwe au mwarabu hatakiwi
 
Yawezekana kuna kikundi kisichoitakia mema nchi, kinataka kuamsha hisia kali na chuki za kidini nchini.

Lakini pamoja na hayo, bado rais anapaswa apingwe kwa namna yoyote ile mpaka aamue kuachana na mawazo ya kuuza nchi kwa waarabu. Asifikiri kuwa sisi tumekubali kuuza urithi wetu milele kama alivyofanya Essau.

Sisi tumeamua kusimama na urithi wetu mpaka tone la mwisho la damu. Akitaka amani basi aelekee visiwani akaviuze atakavyo kwa wanayemtaka.
 
Yupo Clubhouse chumba cha Watanzania ataeleza yote muda si mrefu jiunge umsikie.
 
Hizi sarakasi mie sizielew mara kupinga bandari kuuzwa kwa muarabu mara mwarabu sio mbaya vipengele vya mkataba virekebishwe Jamani kwani tatizo ni mkataba urekebishwe au mwarabu hatakiwi
Mwarabu tunamtaka sana, tatizo ni huo mkataba wa Chifu Mangungo ndio hatutaki.

Ona madhara yake hapa chini.


MKATABA MBOVU WAITIA KITANZI TANZANIA

Ndugu Watanzania!
Video hii ni sehemu ya Kesi ya Madini kati ya Tanzania na Kampuni ya Winshear Gold Corp. Mkataba wa Madini uliosainiwa mwaka 2014 na Waziri wa Nishati na Madini enzi hizo ndio unaobishaniwa hapa. Katika safu ya utetezi, Tanzania ilimpeleka Prof. Abdulkarim Mruma kuwa sehemu ya utetezi. Pamoja na umahiri na usomi wake, Prof. Mruma, hajafua dafu kwani vifungu vya mkataba vinaiumbua Serikali ya Tanzania.

Wakili msomi upande wa Winshear Gold Corp anamhoji Prof. Mruma kuwa inawezekanaje huo mchakato uliopita mikono ya wengi kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Sheria, Kituo cha Uwekezaji cha Tanzania na wasomi wabobezi wa madini kama Prof. Mruma hawakuyabaini hayo mapungufu ndani ya mkataba? Swali hilo alishindwa kujibu Prof. Mruma, hivyo akaishia 'kulenga shabaha mwituni'!

Tunachotaka kusema ni kuwa, kama serikali ikisaini mkataba mbovu, huko mbele ya safari hata ikipeleka wasomi 100 wenye uwezo kama wa Prof. PL Lumumba, Mhe. Tundu Lissu, Peter Kibatara, Dkt. Masumbuko Lamwai (RIP), Prof. Jwani Mwaikusa (RIP), Dkt. Sengondo Mvungi (RIP), nk itapigwa tu.

Tunapohoji na kuupinga Mkataba wa Bandari muwe mnatuelewa. Waambieni Dkt. Tulia, Prof. Mbarawa, Maulidi Kitenge, Cd. Chongolo, na Mwanasheria Mkuu wa Serikali waipitie vizuri video hii. Lakini tutamuomba Gerson Msigwa amuonyeshe Mhe. Rais Samia clip hii. Lakini majibu ya Prof. Mruma yanaonyesha wahusika walipitia mchakato wote. Swali linalojitokeza kwetu sote ni kwa nini serikali iliusaini? Kama ni hivyo, ni kwa nini Serikali iliuvunja baadaye?
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 24 Julai 2023; 15:40 pm.
 
Askofu maximilian machumu akiwa miongoni mwa aliyeshiriki mkutano wa temeke kupingwa uuzwaji wa bandari za nchi kwa waarabu maisha yake yapo hatarini

Baada ya mkutano wa juzi watu wasiojulikana walumfuata kwake kibaha hawakumkuta
Walipomkosa walienda ofisini kwake kuvunja mipango na madirisha ila hawakumkuta
....
Dr.slaa


My take

Watanganyika tuamke,kama hadi viongozi wa dini wanatishiwa maisha vipi kwa sisi wananchi wa kawaida?

Maisha ya askofu kuwa hatarini kwasababu ya kupinga bandari kuuzwa sio inshara nzuri
Taifa litaanguka

Serikali isianze kuharibu amani ya nchi ilyojengwa na Nyerere
Anajitisha mwenyewe ili apate public sympathy.
 
mwarabu amekuja Tanzania kutugawa na kutusambaratisha kabisa. hiii ndio ishara kuwa hatumtaki kabisa.
 
Uoga huo na kushindwa kujibu hoja za wanaoupinga mkataba.

Kizuri kitajiuza chenyewe tu ...
 
Back
Top Bottom