TANZIA Askofu Mkuu wa Kanisa la Methodist Tanzania, Joseph Bundala ajinyonga kisa madeni, mgogoro

TANZIA Askofu Mkuu wa Kanisa la Methodist Tanzania, Joseph Bundala ajinyonga kisa madeni, mgogoro

Jana nimeiona taarifaa hiyo... Kwa TV.

Kisha nikavuta kumbukumbu hapa jamii forum's miaka ya 2009.. kama sikoseii..


Kuna member mmoja alileta Uzi wa kujitoa uhai kwa njia tofauti tofautii....

Kifo hakina huruma..
 
Kwa kuwa alikuwa askofu Mkuu..!!

Basi Wacha tunukuu vifungu vya biblia...

Je, Yuda iskarioti. Alikufajee..???

Mathews/Mathayo 27:3-10.

"Yuda alipata kujinyonga"

Acts of apostles/Matendo ya mitume 1:15-20.
.

"Yuda alipata kuanguka na tumbo/utumbo lake likapasukaa".




Gossip kama moja ya unification of humankind...


Wadaku/uvumi usio na uthibitisho unadai bwana yule Kutoka nigeria alijnyonga baada ya kuona mambo Sasa yanakuwq wazi juu ya kazi zake-Tb Joshua..
 
Askofu mkuu wa makanisa ya Methodist,Joseph Bundala amejinyonga ofisini kwake kwa kutumia waya wa simu.
---

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Methodist Tanzania, Joseph Bundala (55), amekutwa amejinyonga kwa kamba ndani ya ofisi yake iliyoko kwenye kanisani hilo, Mtaa wa Meriwa, jijini hapa.

Kiongozi huyo wa kiroho, ameacha waraka mrefu ukieleza sababu za kuchukua uamuzi huo kuwa ni madeni na mgogoro ulioko katika uendeshaji wa shule binafsi.

Bundala ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kanisa hilo kwa Afrika, mwili wake uligundulika juzi saa 1:00 usiku ukiwa unaning’inia ofisini kwake.

Akizungumzia tukio hilo jana, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Alchelaus Mutalemwa, alisema Jeshi la Polisi linachunguza tukio la askofu huyo, ambaye ni Mkazi wa Ihumwa jijini hapa kuchukua uamuzi huo.

“Tukio hilo liligundulika Mei 16, 2024 majira ya saa 1:00 usiku katika mtaa wa Meriwa, Dodoma, ndani ya ofisi yake iliyoko katika kanisa hilo. Uchunguzi katika eneo la tukio umekutwa ujumbe unaeleza sababu za kujinyonga ni madeni na mgogoro uliopo katika uendeshaji wa shule binafsi,” alisema.

Alisema taarifa za awali hazijaeleza kiasi anachodai au kudaiwa kupitia ujumbe aliouacha.

Akizungumza na Nipashe, Mwenyekiti wa Mtaa wa Sulungai, Grevas Lugunyale, alisema alipigiwa simu na mchungaji wa kanisa hilo kwa madai kuwa wamekuta Askofu amejinyonga.

“Nilipiga simu polisi kutokana na kukutwa amejinyonga. Katika ukaguzi tulikuta mezani kuna waraka ameuandika yeye mwenyewe. Kuna madai anadai na kuna madai naye anadaiwa. Polisi walipokuja pia walifanya uchunguzi wao tukahojiwa na kuchukua mwili kwenda kuuhifadhi,” alisema.

Alisema tukio kubwa na linaumiza kwa kuwa ni Askofu ambaye watu wengi wanamuamini na wanamjua lakini inaonekana hakuwa na watu wa kuwaambia yaliyomsibu ili apate ushauri ambao ungemsaidia.

Mwenyekiti wa Shina Namba 11, Jonathan Mpando, alisema anamfahamu Askofu Bundala amekuwa akisaidia kwenye kampeni kutokana na kuwa na kundi kubwa la waumini.

Jirani wa Askofu huyo, Kedmond Ngalya, alisema amejinyonga akiwa ofisi kwake na kuacha waraka ambao ulichukuliwa na polisi.

Naye jirani mwingine, Omar Hussein, alisema siku tatu zilizopita alikutana na Askofu huyo na walisalimiana na hakuonyesha dalili zozote za kukatisha maisha yake.

“Ila nimeshangaa taarifa ya kujinyonga kwake usiku ya jana (juzi) kusikia Askofu anayekemea dhambi ya kujinyonga na yeye amejitundika kwa kamba,” alisema.

Steve Magawa ambaye ni Jirani, alisema kifo hicho kimemsikitisha kwa kuwa kiongozi huyo wa dini alikuwa mwalimu wa matendo ya Mungu.

Katibu Mkuu wa Kanisa hilo, Allen Siso, alisema alipigiwa simu majira ya saa nne na mmoja ya watumishi na kwamba taarifa zaidi wataeleza baada ya kukaa kikao.
Kwa hiyo kajinyonga kwa waya wa simu au kajinyonga kwa kamba? Hebu tuwekane sawa kidogo ndugu yangu.

Ova
 
Madeni sio sababu.
Nadaiwa
Branch 297,000
Mpawa 75,000
Nipigie tafu 9,000
Songesha,170,000
Ile songesha ya tigo 252,000
DAWASCO 145,000
Mchepuko anadai kodi ya kuanzia Juni .
Isingekua luku tanesco wangehusika.
Huku uraiani usiseme.
Hata chembe ya stress Sina.
Pole sana Mkuu, naona madeni yako mengi ni kutoka Kampuni za simu 🙌

Ni kweli wengi wetu tuna madeni lakini kama asemavyo Daktari bingwa wa Uchumi wa Nchi yetu (Dr Mwigulu Nchemba) kwamba ni madeni himilivu

Binafsi nina zaidi ya milioni 179 nadaiwa lakini bado nadunda tu 😜

Haya maisha sio ya kuya-complicate
 
Wanaume tunatakiwa kufanya kikao cha dharura. Maana haya matukii zamani yaliwakumba zaidi ndugu zetu wa upande wa pili. Kuna sehemu tumepwaya bila shaka.

Ni vizuri kuwa na sehemu ya kuzipunguza/kuziondoa kabisa sumu ndani ya miili yetu, kabla mambo hayajaharibika.
Nimeipenda hii
 
Back
Top Bottom