TANZIA Askofu Mkuu wa Kanisa la Methodist Tanzania, Joseph Bundala ajinyonga kisa madeni, mgogoro

TANZIA Askofu Mkuu wa Kanisa la Methodist Tanzania, Joseph Bundala ajinyonga kisa madeni, mgogoro

Pole sana Mkuu, naona madeni yako mengi ni kutoka Kampuni za simu 🙌

Ni kweli wengi wetu tuna madeni lakini kama asemavyo Daktari bingwa wa Uchumi wa Nchi yetu (Dr Mwigulu Nchemba) kwamba ni madeni himilivu

Binafsi nina zaidi ya milioni 179 nadaiwa lakini bado nadunda tu 😜

Haya maisha sio ya kuya-complicate
Aweke picha ya mwamposa Kwenye wallet
 
Wanaume tunatakiwa kufanya kikao cha dharura. Maana haya matukii zamani yaliwakumba zaidi ndugu zetu wa upande wa pili. Kuna sehemu tumepwaya bila shaka.

Ni vizuri kuwa na sehemu ya kuzipunguza/kuziondoa kabisa sumu ndani ya miili yetu, kabla mambo hayajaharibika.
Sijasikia Shehe kajinyonga aisee ila kwa kuwa wote ni binadamu wala hakuna kushangaa
Binadamu anafanya mambo zaidi ya wanyama
 
Kwa hiyo Askofu alipanda kwenye nguzo ya simu za TTCL kisha akakata waya wa unaomtosha kujinyonga, kisha akaingia nao ofisini kwake?

Ova
Kaka, umezaliwawapi? Simu za TTCL za mezani zinaunganishwa na waya mgumu Sana hata kuvutia gari unaweza. Yaani Ni Kama waya wa pasi au birika la umeme.
 
Sijasikia Shehe kajinyonga aisee ila kwa kuwa wote ni binadamu wala hakuna kushangaa
Binadamu anafanya mambo zaidi ya wanyama
Utendaji wa masheikh siyo wa kitaasisi. mtu anweza akaamua nyumba yake uwe msikiti na sala ikaenda.
Maaskofu (ukiacha akina Gwajima, self proclaimed Bishops) wa madhehebu Hawa ni taasisi, zinakuwa na bussiness nyingi kupelekea mtu kuwa engaged katika madeni kuziendesha and many more
 
Tukio la juzi, Mei 16, Askofu Bundala wa Dodoma amejinyonga na kamba,waya wa umeme,amejiua kukimbia madeni yaliyokuwa yanamkabili.
---
ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Methodist Tanzania, Joseph Bundala (55), amekutwa amejinyonga kwa kamba ndani ya ofisi yake iliyoko kwenye kanisani hilo, Mtaa wa Meriwa, jijini hapa.

Kiongozi huyo wa kiroho, ameacha waraka mrefu ukieleza sababu za kuchukua uamuzi huo kuwa ni madeni na mgogoro ulioko katika uendeshaji wa shule binafsi.

Bundala ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kanisa hilo kwa Afrika, mwili wake uligundulika juzi saa 1:00 usiku ukiwa unaning’inia ofisini kwake.

Akizungumzia tukio hilo jana, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Alchelaus Mutalemwa, alisema Jeshi la Polisi linachunguza tukio la askofu huyo, ambaye ni Mkazi wa Ihumwa jijini hapa kuchukua uamuzi huo.

“Tukio hilo liligundulika Mei 16, 2024 majira ya saa 1:00 usiku katika mtaa wa Meriwa, Dodoma, ndani ya ofisi yake iliyoko katika kanisa hilo. Uchunguzi katika eneo la tukio umekutwa ujumbe unaeleza sababu za kujinyonga ni madeni na mgogoro uliopo katika uendeshaji wa shule binafsi,” alisema.

Alisema taarifa za awali hazijaeleza kiasi anachodai au kudaiwa kupitia ujumbe aliouacha.

Akizungumza na Nipashe, Mwenyekiti wa Mtaa wa Sulungai, Grevas Lugunyale, alisema alipigiwa simu na mchungaji wa kanisa hilo kwa madai kuwa wamekuta Askofu amejinyonga.

“Nilipiga simu polisi kutokana na kukutwa amejinyonga. Katika ukaguzi tulikuta mezani kuna waraka ameuandika yeye mwenyewe. Kuna madai anadai na kuna madai naye anadaiwa. Polisi walipokuja pia walifanya uchunguzi wao tukahojiwa na kuchukua mwili kwenda kuuhifadhi,” alisema.

Alisema tukio kubwa na linaumiza kwa kuwa ni Askofu ambaye watu wengi wanamuamini na wanamjua lakini inaonekana hakuwa na watu wa kuwaambia yaliyomsibu ili apate ushauri ambao ungemsaidia.

Mwenyekiti wa Shina Namba 11, Jonathan Mpando, alisema anamfahamu Askofu Bundala amekuwa akisaidia kwenye kampeni kutokana na kuwa na kundi kubwa la waumini.

Jirani wa Askofu huyo, Kedmond Ngalya, alisema amejinyonga akiwa ofisi kwake na kuacha waraka ambao ulichukuliwa na polisi.

Naye jirani mwingine, Omar Hussein, alisema siku tatu zilizopita alikutana na Askofu huyo na walisalimiana na hakuonyesha dalili zozote za kukatisha maisha yake.

“Ila nimeshangaa taarifa ya kujinyonga kwake usiku ya jana (juzi) kusikia Askofu anayekemea dhambi ya kujinyonga na yeye amejitundika kwa kamba,” alisema.

Steve Magawa ambaye ni Jirani, alisema kifo hicho kimemsikitisha kwa kuwa kiongozi huyo wa dini alikuwa mwalimu wa matendo ya Mungu.

Katibu Mkuu wa Kanisa hilo, Allen Siso, alisema alipigiwa simu majira ya saa nne na mmoja ya watumishi na kwamba taarifa zaidi wataeleza baada ya kukaa kikao.
Kwa nn serikali isiwe na kitengo cha counselling amd guidance ? Hiki kitengo wanachukulia kwa watu weny magonjwa ila ishu ya mawazo na wasiwasi ipo kwa sana .

Taarifa za kujinyonga kwa jinsia ''ME'' zimerindima sana kama sijakosea huko Geita mwingine alitoka hospital alipokuwa kalazwa akajinyonga , Viongozi wawili wa dini nao hivyo hivyo .. Huko Arush kuwa wawili wanawake wamejinyonga kuhusishwa kudaiwa kweny vikoba.
 
Utendaji wa masheikh siyo wa kitaasisi. mtu anweza akaamua nyumba yake uwe msikiti na sala ikaenda.
Maaskofu (ukiacha akina Gwajima, self proclaimed Bishops) wa madhehebu Hawa ni taasisi, zinakuwa na bussiness nyingi kupelekea mtu kuwa engaged katika madeni kuziendesha and many more
Nimekupata mkuu
Ila kujiua aisee ni jambo baya sana bora angekimbia nchi wakasema katoroka

Hebu nisaidie hapo mbona wanasema sadaka ni nyingi sana mpaka mishahara ya watu inakatwa juu kwa juu
 
Back
Top Bottom