TANZIA Askofu Mkuu wa Tanzania Assemblies of God, Dkt. Immanuel Lazaro amefariki Dunia

TANZIA Askofu Mkuu wa Tanzania Assemblies of God, Dkt. Immanuel Lazaro amefariki Dunia

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
18,223
Reaction score
31,465
Tutaendelea,kuwapatia taarifa zaidi!

IMG-20250518-WA0010.jpg

TANZIA: Askofu Mkuu wa kwanza mstaafu wa Tanzania Assemblies Of God (TAG) Dkt.Emmanueli Lazaro amefariki Dunia Mei 17,2025 .

Akitoa taarifa za kifo hicho Makamu Askofu Mkuu wa TAG, Magnus Mhiche amesema kuwa Hayati Dkt.Emmanuel Lazaro alifariki hapo jana mei 17,2025 na maziko yanatarajiwa kufanyika Mei 22,2025 siku ya Alhamis huko Kijijini kwake Masama Modio Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro kwenye Kanisa la zamani alilokuwa akisali.

Askofu Lazaro alisimikwa kuwa Mchungaji mwaka 1964, na baadaye aliongoza Kanisa la TAG kama Askofu Mkuu kwa kipindi cha miaka 24, kuanzia mwaka 1967 hadi 1992.

Alikuwa kiongozi wa kwanza wa Kanisa hilo kuchukua nafasi hiyo kutoka kwa wamishenari wa kizungu, hatua iliyoweka historia mpya katika uongozi wa kanisa hilo nchini Tanzania.

Mbali na uongozi wake ndani ya TAG, Askofu Lazaro pia alikuwa mwanzilishi wa Kanisa la Kilimanjaro Revival Temple (KRT), ambalo alilianzisha mwaka 1971 na kulitumikia kama Mchungaji Kiongozi hadi alipostaafu.

Hayati Mchungaji na Askofu Dkt.Emmanuel Lazaro alizaliwa Mwaka 1937 na amefariki 2025 wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya KCMC akiwa na umri wa miaka 88.
Screenshot 2025-05-18 094250.jpg
 
Dah RIP! Namkumbuka miaka ya 80's walikua na mchuano mkali na Moses Kulola (RIP), wakati Assemblies of God inachemka hasa. Tulikua tunafundishwa hadi tunaamini yesu anarudi mwakani yani!
 
Askofu Mkuu wa Kwanza!! Maana yake kwa sasa kuna Askofu mkuu mwingine?

Poleni sana wafiwa
 
He was a good, Commited Man of God, sasa tunabaki na kizazi cha ubishi, manabii wa uongo na wachumia tumbo, wasifia serikali, kupewa posho na wasio Misimamo!

Back then kipindi cha huyu Mzee na Kulola wakifanya mikutano unasikia uwepo, na hakuna ulaghai, injili kavu, Kali na halisi kabisa.

Nakumbuka kipindi cha Tanzania itubu, was pure and good, watu waliokuwa na kuthubutu kukemea Dhambi ya taifa na kuita Taifa in Public kutubu!

Kwa sasa ukikemea Dhambi kama Maghembe unaonekana msaliti na hufai, wokovu ni kweli na halisi, ila watu wameushusha thamani.

Hivi mna amini wakati wa uchaguzi Mkuu wa TAG miaka hii watu wanahofia uhalifu, kupeana sumu na kulogana kugombea uongozi?

RIP Mtu wa Mungu, nitakukumbuka sana!
 
Dah RIP! Namkumbuka miaka ya 80's walikua na mchuano mkali na Moses Kulola (RIP), wakati Assemblies of God inachemka hasa. Tulikua tunafundishwa hadi tunaamini yesu anarudi mwakani yani!
Ulikuwa Mgogoro wa kimaslahi ule walizidiana kete kulola alionekana kukubalika sana kuliko lazaro kikawa kizaa zaa balaa na ndio chanzo cha kukola kuanzisha dhehebu lake
 
Ameenda kule kulikomfanya aishi, kujiandaa na kukutamani. Mwenyezi Mungu ampokee.
 
Mungu ampumzishe kwa amani ni wakati mgumu sana mkwe wake Yuko hospital Hali sio nzuri kabisa
 
Back
Top Bottom