peno hasegawa
JF-Expert Member
- Feb 24, 2016
- 18,223
- 31,465
Tutaendelea,kuwapatia taarifa zaidi!
TANZIA: Askofu Mkuu wa kwanza mstaafu wa Tanzania Assemblies Of God (TAG) Dkt.Emmanueli Lazaro amefariki Dunia Mei 17,2025 .
Akitoa taarifa za kifo hicho Makamu Askofu Mkuu wa TAG, Magnus Mhiche amesema kuwa Hayati Dkt.Emmanuel Lazaro alifariki hapo jana mei 17,2025 na maziko yanatarajiwa kufanyika Mei 22,2025 siku ya Alhamis huko Kijijini kwake Masama Modio Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro kwenye Kanisa la zamani alilokuwa akisali.
Askofu Lazaro alisimikwa kuwa Mchungaji mwaka 1964, na baadaye aliongoza Kanisa la TAG kama Askofu Mkuu kwa kipindi cha miaka 24, kuanzia mwaka 1967 hadi 1992.
Alikuwa kiongozi wa kwanza wa Kanisa hilo kuchukua nafasi hiyo kutoka kwa wamishenari wa kizungu, hatua iliyoweka historia mpya katika uongozi wa kanisa hilo nchini Tanzania.
Mbali na uongozi wake ndani ya TAG, Askofu Lazaro pia alikuwa mwanzilishi wa Kanisa la Kilimanjaro Revival Temple (KRT), ambalo alilianzisha mwaka 1971 na kulitumikia kama Mchungaji Kiongozi hadi alipostaafu.
Hayati Mchungaji na Askofu Dkt.Emmanuel Lazaro alizaliwa Mwaka 1937 na amefariki 2025 wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya KCMC akiwa na umri wa miaka 88.