PreGE2025 Askofu Mlawi: Kesi ya Lissu ziharakishwe kabla ya Uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Askofu Mkuu wa Makanisa ya SPCT na Rais wa Umoja wa Maaskofu, Wachungaji, Mitume na Manabii na Madhehebu ya Kikristo Tanzania, Askofu Mussa Mlawi, amevitaka vyombo vya utoaji haki nchini kuharakisha usikilizwaji wa kesi zinazomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, na kuhakikisha suala hilo linamalizika kabla ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba.

Askofu Mlawi amesema kuna haja ya serikali kutafuta njia ya mazungumzo na kumsikiliza Tundu Lissu, badala ya kuendelea kusuguana naye mahakamani, jambo ambalo linatia doa katika sura ya demokrasia ya taifa.

Amesisitiza kuwa haki ya kisiasa ni msingi muhimu wa amani na maendeleo, hivyo serikali na vyombo vya sheria vina jukumu la kuhakikisha usawa na haki vinatendeka kwa wote bila upendeleo.
​
Chanzo: Jambo TV

View attachment 3358962
Chanzo: Jambo TV
Kesi yenyewe ni halali? Mbona ni waoga kusema ukweli?
 
..kesi dhidi ya Tundu Lissu zifutwe.

..Na Tume ya Uchaguzi iwe huru kweli.

..Uchaguzi uendeshwe kwa uwazi.
 
Mimi kuna jambo silielewi. Iwapo Tundu Lisu anastasia kwabugaini baada ya kusema "No Reforms No Election", mbona akina Heche na wenzao wanaendelea na mikutano ya kuhamaisha wananchi jambo hilo hilo "No Reforms No Election na nimetazama mikutano yao inalindwa na Askari polisi? Mbona wao hawajakamatwa kushtakiwa jwa kosa hilo?
 
Tatizo wao wanafikiri njia wanazotumia ndo zitawapa faida....ila wangejua mioyo ya binadamu wa kitanzania wangeacha ujinga wanaofanya maana for sure utakuja kuwagharimu hata kama ni maiaka ya mbele....
 
Alishatikiwa kwa kusema kitanuka kama sikosei....sio ishu ya NRNE...
All in all hakuna kesi pale...ni ujinga walio nao watawala waoga tu
 
Tatizo wao wanafikiri njia wanazotumia ndo zitawapa faida....ila wangejua mioyo ya binadamu wa kitanzania wangeacha ujinga wanaofanya maana for sure utakuja kuwagharimu hata kama ni maiaka ya mbele....
Siyo "miaka ya mbele", mkuu 'Makoshoi'.
Gharama watailipa wakati huu huu. Safari hii hakuna tena utani utani waliozoea kuwafanyia waTanzania.

NO REFORM, NO ELECTION.
 
1001172625.png
 
Chadema waliweka mtego kuweka Uchaguzi wao wa chama kua live tena wazi bila zengwe ukawa huru na haki ulikua mtego
 
Ye kama nan au kwa mamlka gan alonayo
Ukiwa Mkiristo unaweza kusema Waislamu walizungumza kuhusu ndugu zao Wapo ndani miaka 10 na hakuna kesi Waliambiwa wanataka kuleta fujo na kupigwa
 
Ni spana kutoka kila kona ya nchi, keki inaliwa lakini dinning room kumejaa siafu hakukaliki.

Ni mwendo wa pressure, moyo na sukari, bila kusahau madonda tumbo kama bonasi.

Ndo ile unasikia matajiri wengi wanaishi kwa stress kuliko masikini.

NO REFORMS NO ELECTION
FREE TUNDU LISSU
 
Back
Top Bottom