Askofu Mpemba amchana Spika Ndugai na wabunge 19 waliobatizwa jina la "COVID-19"; Wamevunja Katiba, warudishe fedha

Mtazame na msikilize mwenyewe kisha tunaweza kusema na kujadiliana...

View attachment 1765034

Huu ukosoaji enzi za Mwendazake John Pombe, ilikuwa hatari na pengine angeweza kunyang'anywa uhai bila kupenda...

Pengine pia, tunaweza kuamini zile tetesi za kuwa kuna zengwe linasukwa chini chini ili atemeshwe u - Spika kabla ya 2025...

Mbona mashambulizi dhidi yake yameachiliwa hivi...?

Huu ndio uhuru wa habari. Watu hawazuiwi kusema yale yanayovuruga nchi!!
 
Hakika hivi sasa watu wanajiachia ile mbaya!

Enzi za Mwendazake ilikuwa ni ndoto kuona aina hii ya ukosoaji
Watu walikuwa wanaogopa kudukuliwa! Mwendazake kwa kukili mwenyewe alikuwa anadukua mpaka Simu za mawaziri wake!!
 
Hapa ndo naelewa msemo wa ukila nyama ya mtu hutakaa uache...

Yaani bado hata humo bungeni ni mwendo wa vijembe tu, uchakachuzi bila aibu... Tena kwa kiburi na madharau as if nchi hii wao ndo wenye hati miliki... Yaani ni kama hatuna vyombo vya ulinzi na usalama vyenye jukumu la kulinda nchi (kulinda nchi ni pamoja na kuzuia viashiria vyote vya uvunjifu wa amani ikiwa ni pamoja na dharau kwa katiba anavyofanya Ndungai na genge lake)
Waliforge mpaka wakapitiliza njia!
Mwisho wakajikuta hakuna kambi ya zupinzani bungeni.
Ikabidi sasa waforge tena.
Mwalimu alisema ukila nyama ya mtu, utaendelea kula nyama ya mtu.

For good governance CHADEMA walipeleke suala hili mahakamani.
 
Mkuu,

Acha kubeba vitu na kuja kupachika hapa, huyo unayemwita askofu unakumbuka alianza kufanya vituko gani enzi za Jakaya Kikwete wakati huo akiwa mchungaji kanisa moja hapo Mkuyuni Mwanza njia ya kuelekea Butimba?

Unafahamu waumini wake walitaka kumfanya nini?

Unafahamu kuwa huyo alishawahi kuwa mlinzi wa kampuni moja na kuacha kazi hiyo kwa aibu?

Ukosoaji ulio imara na wenye tija ni ule unaotumia ufundi wa kung'arisha rangi ya chatu kwa mfumo wa picha jongefu wakati akihitahitaji mawindo!!

Huyo ni askofu wa mwili na nafsi sio ROHO na yeye analitambua hilo, muulize huko aliko USA, watu wanafahamu A to Z kuhusu huyo mtu aliyevaa kofia ya cowboy
Maswali yote uliyojiuliza ni ya kipuuzi na wewe mwenyewe inaonyesha unamzungumzia askofu usiyemjua! ili kuthibitisha kuwa umeropoka jaribu kuweka majibu ya maswali uliyojiuliza!
 
Hivi Kwa nini Chadema hawakuifuatilia Ile Barua kutaka kujua ilikotokea??

Sawa, walimhofia Jiwe, leo hayupo, ni muda mwafaka wa kufahamu Barua Ile ilitokea wapi na Nani aliwaidhinisha wale wabunge wa Chadema kuingia bungeni
Kuwataka Chadema wafuatilie barua imetoka wapi ni kuhamisha goli. Wajibu wa Chadema katika hilo ni mmoja tu, kuthibitisha kwamba wale Covid-19 walioko bungeni sio wanachama wa Chadema, basi. Kama Tanzania ina serikali kweli na ina vyombo vya dola, Chadema wanapaswa kuwa mashahidi kwenye issue ya kughushi ile barua. Usichofahamu ni nkwamba serikali yenyewe inafahamu kwamba ule ulikuwa mchezo mchafu. waliohusika kutengeneza huo mchezo, nikusaidie ni hawa. Mwita Waitara, Dk. Mashinji, Waziri Mkuu, Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi pamoja na Spika wa Bunge . Hawa ndio walishiriki kufanikisha huu upumbavu. Na kwa taarifa yako, miongoni mwa hao Covid-19 wamo ambao wala hawajawahi kuwa wanachama wa Chadema, bali ni watu ambao ni ama jamaa, ndugu, au michepuko ya akina Spika. Hili jambo kama lingechunguzwa tungeona uozo wa ajabu kuwahi kufanyika katika nchi hii. Kuna wakati unajiuliza hivi watu wanaomlilia Mwendazake wanafahamu kweli alikokuwa anaipeleka hii nchi? Katika kipindi cha Magufuli kuna mambo ya kihuni kupitiliza yalikuwa yakifanyika!
 
Dogo maelezo yako sio sahihi. Huyu "Askofu" alikimbia kipindi cha JK. Na kilichomkimbiza ni ishu ya kukomalia eti na Wakristu wapewe haki ya kuchinja kama ilivyo kwa Waislamu. Aliishadidia sana hii ishu hasa kupitia "karedio" kake hapa Jijini Mwanza. Serikali ya JK ilipochoka naye ikataka "kumshughulikia" ndio akakimbia nchi hadi leo!
Kumbe hata Jk nae alikuwa anawshughulikia?
 
Hakika hivi sasa watu wanajiachia ile mbaya!

Enzi za Mwendazake ilikuwa ni ndoto kuona aina hii ya ukosoaji
Ukikosoa namna hii mitandaoni special task force ilikufuatilia. Kama una bahati utaokotwa Unonio, kama huna bahati utaishia kwenye sandarusi baharini.
 
Hakika hivi sasa watu wanajiachia ile mbaya!

Enzi za Mwendazake ilikuwa ni ndoto kuona aina hii ya ukosoaji
Inasaidia nini wakati wewe unasema wenzako wanaendelea kula posho za bungeni
 
Kuwataka Chadema wafuatilie barua imetoka wapi ni kuhamisha goli. Wajibu wa Chadema katika hilo ni mmoja tu, kuthibitisha kwamba wale Covid-19 walioko bungeni sio wanachama wa Chadema, basi. Kama Tanzania ina serikali kweli na ina vyombo vya dola, Chadema wanapaswa kuwa mashahidi kwenye issue ya kughushi ile barua. Usichofahamu ni nkwamba serikali yenyewe inafahamu kwamba ule ulikuwa mchezo mchafu. waliohusika kutengeneza huo mchezo, nikusaidie ni hawa. Mwita Waitara, Dk. Mashinji, Waziri Mkuu, Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi pamoja na Spika wa Bunge . Hawa ndio walishiriki kufanikisha huu upumbavu. Na kwa taarifa yako, miongoni mwa hao Covid-19 wamo ambao wala hawajawahi kuwa wanachama wa Chadema, bali ni watu ambao ni ama jamaa, ndugu, au michepuko ya akina Spika. Hili jambo kama lingechunguzwa tungeona uozo wa ajabu kuwahi kufanyika katika nchi hii. Kuna wakati unajiuliza hivi watu wanaomlilia Mwendazake wanafahamu kweli alikokuwa anaipeleka hii nchi? Katika kipindi cha Magufuli kuna mambo ya kihuni kupitiliza yalikuwa yakifanyika!
Mkuu, kumbe Una ushahidi kabisa, Wakati huohuo unataka kufanyike uchunguzi....! Kwa ushahidi huohuo mi nadhani, anzia hapohapo, peleka mahakamani
 
Mtazame na msikilize mwenyewe kisha tunaweza kusema na kujadiliana...

View attachment 1765034

Huu ukosoaji enzi za Mwendazake John Pombe, ilikuwa hatari na pengine angeweza kunyang'anywa uhai bila kupenda...

Pengine pia, tunaweza kuamini zile tetesi za kuwa kuna zengwe linasukwa chini chini ili atemeshwe u - Spika kabla ya 2025...

Mbona mashambulizi dhidi yake yameachiliwa hivi...?
Ndugai hafai ni mtu hatari sn
 
Ku

Kuhusu subwoofer kutoka before 2025 msijali, Mungu ni bonge la fundi. Nadhani naeleweka.
 
Acha uongo wako we kapuku, huyu askofu aliondoka Tanzania wakati wa Jakaya mwaka 2013 baada ya vurugu za kuchinja nyama baina ya waislamu na wakristo kuibuka. Kila kitu kusingizia watu waliokufa ni upuuzi.
Kuhusu kuwasema watu waliokufa kwa mazuri au kwa mabaya sijui imekatazwa wapi? Mbona CCM mpaka Leo mnatuaminisha Iddi Amin alikuwa anakula nyama za watu na hamkuwahi kutoa ushahidi?
 
Ishu ni kumsema marehemu au kusema ukweli?
 
Back
Top Bottom