Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Setuba Noel, unapaswa tu kuuliza kwamba huu utamaduni umetoka wapi na kama unaweza kubadilishwa. Ukisema kwamba endapo huu utaratibu ukiendelea kwa miongo kadhaa makanisa yatageuka kuwa makaburi, unaonesha ulivyo na ufinyu wa kufikiria. Kumbuka kanisa katoliki lina umri wa miaka zaidi ya 2000. Kule Ulaya ambapo kanisa lilianza wamekuwa wanazika maaskofu makaburini tangu enzi hizo. Kama utafiti wako ungekuwa sahihi, makanisa kule yangeshageuka kuwa makaburi. Usikurupuke kuongea kitu, jaribu kufanya research kwanza
Poleni wafiwa Mungu awape nguvu ya kustahimili. Naomba kuuliza, ni kwanini wakatoliki wanazika maaskofu wao ndani ya makanisa? Akifa askofu kanisa linageuzwa kaburi, kwanini jamani? Kama Moshi kule naambiwa kuna maaskofu 3 wamezikwa ndani ya kanisa moja. Hali hii ikiendelea miongo mitatu kanisa linaweza kugeuka cemetery kabisa! Kuna sababu gani za kiimani kwa jambo hili, na je haziwezi kubadilishwa?
Achana naye amefungwa na diniKiongozi mbona unajichanganya? Sasa mvivu wa kufikiri hapa nani? Kumbe hata huko Ulaya lilikoanzia kanisa (kwa mawazo yako Israel ni Ulaya, au kanisa halikuanzishwa na Yesu wa Nazareti?), umesema wamekuwa wakizika maaskofu makaburini! Kumbe ndio maana makanisa yao hayajageuka makaburi basi, au? Na huku Tanzania utamaduni wa kuzika askofu kanisani kauanzisha nani? Na utafiti wangu unaoongelea ni upi? Kumbe basi "utafiti" siyo "research" ndiyo maana unanituma nikafanye "research" kabla sijakurupuka kuongea kitu? Hongera mtafiti! Mimi nimetoa angalizo tu kutokana na trend niliyosimuliwa kuwa pale Moshi kuna kanisa moja ambalo katika muda wa miaka kama 30 hivi tayari lina makaburi 3 ya maaskofu ndani yake, kwa hiyo prediction yangu ni kuwa trend ikiendelea hivyo miaka 30 mingine si ajabu kukawa na makaburi 6 ndani, na hapo neno cemetery litakuwa sahihi kutumiwa, au bado unabisha mheshimiwa?