Uchaguzi 2020 Askofu: Mwaka 2020, Kulikuwa na Wizi Mkubwa wa Kura

Uchaguzi 2020 Askofu: Mwaka 2020, Kulikuwa na Wizi Mkubwa wa Kura

Utawapelekeaje majaji wa Magufuli kesi za Magufuli? Utakuwa na akili kweli?

Urais, Mahera akishatangaza basi hakuna kupinga. Ndivyo ilivyo katiba wapendayo CCM.
Lakini hakuna kesi hata moja mahakamani ya kupinga matokeo ya uchaguzi. Hata Mbowe hajapinga matokeo
 
Sikiliza mchango wa Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki, akieleza mambo machafu yaliyofanywa na utawala wa awamu ya 5 kupora haki ya wananchi kupata viongozi wanaowataka.


Nikikumbuka aliyosema Mtume na Nabii Mwingira inasikitisha sana.
 
Utawapelekeaje majaji wa Magufuli kesi za Magufuli? Utakuwa na akili kweli?

Urais, Mahera akishatangaza basi hakuna kupinga. Ndivyo ilivyo katiba wapendayo CCM.
Mahakama ilishiriki pamoja na vyombo vingine.
 
Ule ulikua upolaji wa kura na sio wizi.wapinzani walitakiwa wasishiriki kwenye uchaguzi ule.maana ccm walianza kupolana wenyewe mapemaa...

Maana tumeona kuanzia kwenye kura za chama za ndani.anashinda mwingine lakini anawekwa mwingine.c ndio maana unaona hata kina kimei wanaona aibu kujitokeza.

Kwasabu ya kuwekwa bila ya kupendwa na wananchi.
Tulishirikia kwa sababu kama vile vyombo nyeti visingeisaidia ccm basi ushindi ulikuwa nje nje. Sio mbwe za Mahera wala za MaDED zingefanikiwa
 
Hawakwenda mahakamani kwa sababu wakati wa dikteta, hakuna chombo kilichokuwa kinafanya kazi kwa weledi.
Akina Siyani na Kina Tiganga. Hapo hapo mwenyekiti wa Tume eti anaitwa Jaji🤣🤣
 
Kwa Uchafuzi ule hata Bunge halina uhalali kuendelea kula kodi zetu.
Laana itaendelea kuwatafuna tu!
 
Lakini hakuna kesi hata moja mahakamani ya kupinga matokeo ya uchaguzi. Hata Mbowe hajapinga matokeo
Hoja yako imeshinda hoja za wengine wote. Uchaguzi wa 2020 hauna tatizo na JPM hakuongoza kupora uchaguzi wa 2020. Mkuu umeshinda.
 
Ligasi gang mtajibu mpaka mchoke. Ya kuanikwa ni mengi
Halafu waanikaji ni wengi kuliko wanaojibu. Kuna baadhi wameanza kuelewa ukweli wa uozo wa Awamu hiyo, wabishi wachache tu ndo wamebaki, nao kwa aibu.
 
Bunge limejaa wezi wa kura! Wameamua kurudisha bunge live ila wananchi wanawafurahia Msukuma na Kishimba tu. Wengine ni proffesorial rubbish tu
 
Mwendazake anazidi kupokea mishale kutoka kwa viongozi wa dini tena wakatoliki wenzake. Aione Wakudadavuwa
Alijua akifika anapewa cheo cha kiranja wa malaika ila kwa sasa nahisi kafikia rockup kwanza kujipumzisha. Haya makombora hata huyo mkuu huko lazima amkane 😀😀
 
Back
Top Bottom