ASKOFU Mwamakula atia neno kuhusu kuchaguliwa kwa Wassira kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM

ASKOFU Mwamakula atia neno kuhusu kuchaguliwa kwa Wassira kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM

Pamoja na na mengine mimi nadhani ni nyongeza tu bali sababu kuu iliyowafanya CCM kufanya hivyo ni IMANI YAO kwamba huyu mzee anaweza akawa karata yao muhimu KANDA YA ZIWA.

Huenda walitamani awe PIUS MSEKWA,lkn huyu alishawahi kuwa hapo na kwa siku za hivi karibuni ni kama HAKUBARIANI na falsafa za CHURA KIZIWI kwa hiyo wakaona huenda asiwe bora kwa kuzingatia match ya October 2025.

Sasa wakaona mtu pekee ambaye huenda akawa msaada ni huyu mzee huenda akawasaidia zaidi na zaidi Mkoani MARA unaotajwa kuwa ni miongoni mwa ngome za UPINZANI hapa Tanganyika.

Na mwisho ni kuwa huyu mzee MUIKIZU mwenye wazazi mchanganyiko kati ya MUIKIZU NA MJITA.
Kuwa MUIKIZU hapa ni ndugu wa WAZANAKI na kuwa na visaba vya KIJITA anakuwa ni MSETO ambao CCM wanauona kama atavuta kura kutoka pande zote HASIMU.

Nasema HASIMU kwasababu kati ya mikoa yote ya Tanganyika nadhani ni Mkoa wa MARA tu ndio MAKABILA yake hayana maelewano toka enzi na enzi ijapo huenda usisikie wakizozana.

Tusishangae kumuona SOKWE akikaa pembeni muda mfupi tu mara baada ya match ya October mwaka huu kwani amewekwa hapo maalumu kwa ajili ya kazi hiyo mahususi.
Nasema HASIMU kwasababu kati ya mikoa yote ya Tanganyika nadhani ni Mkoa wa MARA tu ndio MAKABILA yake hayana maelewano toka enzi na enzi ijapo huenda usisikie wakizozana.

Tusishangae kumuona SOKWE akikaa pembeni muda mfupi tu mara baada ya match ya October mwaka huu kwani amewekwa hapo maalumu kwa ajili ya kazi hiyo mahusus👌🏿i.
 
Palihitaji zindiko na kumbukumbu ya madhabahu,apatikane mmojawapo katika wazee waanzilishi,na atoke mkoa uliobeba historia,haya mambo yako kiroho sana.Hii itasaidie kuunganisha nguvu Kizimkazi ipate kibali,nasema mambo ya rohoni na sio lazima uamini.
 
Zamani ilikuwa nikisikia mtu ni askofu, nashika adabu yangu; najua hiyo ni brain na uadilifu (purity). Siku hz baada ya kuwaona hawa maaskofu kwenye magenge haya ya utapeli wakijumuika kupiga ramli, kueneza chuki zao, Nia zao ovu 'evils', wakiwa wamesimamisha maskio 'dodoliiiiii' kuomba wasikie jambo baya kwa jirani Ili haraka watoke kulitangaza kwa kulikuza basi nimebadilisha kabisa mawazo yangu.

Ingefaa angeanza na uchambuzi muruuuuua kabisa wa rushwa, kejeli na sintofahamu inayoendelea kuleeeee kabla ya kuja Huku. Huku hakuwezi, baba askofu atapasuka msamba........hili lidude ccm ni kuuubwa mno kwake kuanza nalo. Aanze huko kudogo kwanza.
Umeongea vzr wenye akili wamekuelewa
 
Kwa jinsi FISIEM walivojizatiti pale hata akiwekwa Katoto ka form 1 hakuna shida yoyote na 25 Oct wanashinda Mchana kweupe.
Hamna analoenda kufanya jipya huyo mzee kawekwa kama Bosheni tu chama kina mifumo yake tayari.
 
Palihitaji zindiko na kumbukumbu ya madhabahu,apatikane mmojawapo katika wazee waanzilishi,na atoke mkoa uliobeba historia,haya mambo yako kiroho sana.Hii itasaidie kuunganisha nguvu Kizimkazi ipate kibali,nasema mambo ya rohoni na sio lazima uamini.

nasema mambo ya rohoni na sio lazima uamini.💪🏿

Thanks
 
Mhe. Stephen Wasira anaanza kuiongoza CCM kama Makamu Mwenyekiti akiwa na umri wa miaka 80. Pengine, huu ni umri mkubwa sana kwa mtu yeyote kupewa uongozi wa juu katika chama cha siasa. Inawezekana kabisa kuwa Wasira atakuwa kiongozi wa kwanza mwenye umri mkubwa zaidi kushika nafasi ya juu ndani ya CCM baada ya Rashid Mfaume Kawawa.

Pengine watu wengi watauliza, inakuwaje CCM wameamua kumteua mtu wa umri wa miaka 80 kuwa Makamu Mwenyekiti? Kwa kawaida huo ndio utamaduni wa vyama dola vyote duniani ambavyo havitegemei kushinda chaguzi zao kwa njia za kidemokrasia. Vyama dola ni vile ambavyo majeshi yote huwa sehemu ya chama ya chama ama kwa kificho ama cha wazi.

Siasa za vyama dola huendeshwa na nguvu za majeshi (Jeshi, Polisi, Usalama wa Taifa, nk). Dola au majeshi hufanya kila kitu lakini wao huhitaji taswira (figure) ya kisiasa kwa ajili ya kugonga muhuri maamuzi yaliyofanywa kijeshi au kiimla. Kwa kawaid, mikakati katika vyama dola hufanywa katika matawi ya majeshi. Hata viongozi wa vyama dola hupata mafunzo yote ya kijeshi, usalama au ujasusi. Lakini mafunzo hayo hayalengi katika kujenga uwezo wa vijana kujenga hoja zenye nguvu, bali katika kujenga nguvu zenye hoja.

Viongozi wa kisiasa katika vyama dola huanza kuandaliwa katika matawi maalum ya usalama na kisha kupelekwa kufanya mazoezi katika nafasi za umma: Katibu Tawala wa Wilaya DAS; Mkurugenzi wa Halmashauri, DED; Mkuu wa Wilaya, DC; Mkuu wa Mkoa, RC; nk.

Lakini pia, minyukano ndani ya CCM inaweza kuwa imepelekea wachague mtu mwenye umri mkubwa sana ili awapitishe katika kipindi cha mpito kuelekea Uchaguzi Mkuu. Mtu huyo pia atawavusha katika kipindi pasipo kugawanyika. Lakini baada ya Uchaguzi Mkuu kumalizika, hapo ndipo ataletwa katika nafasi hiyo mtu ambaye ameandaliwa au anaandaliwa. Lakini kwa hali ilivyo sasa, huyo aliyeandaliwa au pia anayeandaliwa kama jina lake lingeletwa mbele ya wajumbe wa Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na baadaye Mkutano Mkuu, angechafua kabisa hali ya hewa ndani ya CCM.

Kama uchambuzi huu wa Askofu Mwamakula kwako hauna mashiko, achana nao badala yake ungana naye kumpongeza Stephen Wasira kwa kuteuliwa hatimaye kupigiwa kura na Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM kushika wadhifa wa Makamu Mwenyekiti Bara. Moja ya sifa kuu ambayo naweza kumpa Wasira ni unyenyekevu wake. Katika vikao vya kidemokrasia ambavyo tumewahi kushiriki pamoja, hakuwahi hata siku moja kuninyanyapaa kwa sababu ya umbile hili.

Askofu Mwamakula anatoa pongezi kwa Mhe. Wasira kwa kuchaguliwa kuwa Makamu wa Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara. Je, wewe una neno lo lote kwa Mhe. Stephen Wasira?
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 18 Januari 2025; saa 1:20 usikuView attachment 3205843
Nyerere
Mwinyi
Mkapa
Kikwete
Magufuli
Samia

Tunaongelea miaka 60+
 
Kama unadhani hili jibu lako limejitosheleza iweje askofu aliye na umbile la kibinadamu awe na wasiwasi wa kunyanyapaliwa na huyo amsemae wakati na yeye ana umbile la kibinadamu?
Siwezi kumjibia.. Mimi nimejibu kwa muktadha wangu kulingana na ulichouliza
 
Kipanya kamaanisha nini hapaView attachment 3205871
Kipanya ni Noma ! Kwenye kibanda kuna kitu kinapikwa moto ni mkali kweri kweri !
Huku jamaa na gwanda lake ameshamaliza kazi yake ya kuchimba !
Halafu pale kwenye yale mashimo mawili yaliyochimbwa kila shimo kumewekwa Cross moja !
Kisha katika zile Cross hazijaelekea upande mmoja!
Kwenye shimo moja Cross imewekwa kwa mbele ya shimo au nyuma ya shimo !
Na kwenye shimo la pili Cross imewekwa ubavuni !
 
Back
Top Bottom