Askofu Mwamakula azungumzia "matembezi ya hiyari"!

Askofu Mwamakula azungumzia "matembezi ya hiyari"!

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165
ASKOFU MWAMAKULA AZUNGUMZIA "MATEMBEZI YA HIYARI"

Baada ya Askofu Mwamakula kutangaza kuwa 'ataingia barabarani' kuongoza "Matembezi ya Hiyari" kwa nchi nzima ili kuhamasisha umma kuhusu umuhimu wa kuunda Tume Huru ya Uchaguzi na kuandika Katiba Mpya, watu wengi wametaka kujua zaidi kuhusiana na adhma hiyo. Ili kuwasaidia wengi, Askofu ameamua kuchapisha hapa mazungumzo baina yake na mmoja wa watu kutoka taasisi mojawapo yaliyofanyika mwanzoni mwa Mwezi Januari. Askofu ameamua kutokuliweka jina halisi la mtu huyo kwa sababu za kimaadili na kiusalama.

Mayila: Baba Askofu nataka kujua machache kuhusu maandano unayotarajia kuyaongoza hivi karibuni.

Askofu Mwamakula: Karibu! Hata hivyo siyo maandamano bali ni "Matembezi ya Hiyari"!

Mayila: Nashukuru kwa ufafanuzi wako! Je, kuna tofauti ye yote kati ya maandamano na matembezi ya hiyari?

Askofu Mwamakula: Mimi nimesukumwa kutoka ndani ya moyo wangu kutembea na kuonyesha hisia pasipo kukaa katika vikao na taasisi ye yote ile! Hakuna shinikizo lo lote la kitaasisi. Hata watu watakaoshiriki ni raia wa Tanzania watakaoamua kwa hiyari yao wenyewe pasipo mashinikizo ye yote!

Mayila: Je! Utaomba kibari kutoka Jeshi la Polisi?

Askofu Mwamakula: Hatuhitaji kuomba kibari, bali tutatoa taarifa sio tu kwa Jeshi la Polisi bali kwa umma wote wa Watanzania na dunia nzima!

Mayila: Je, Jeshi la Polisi wakikuzuia utafanyaje?

Askofu Mwamakula: Nitaingia barabarani na kuendelea na "Matembezi ya Hiyari"!

Mayila: Huoni kuwa utakuwa unahatarisha usalama na kuvuruga amani?

Askofu Mwamakula: Askofu aliyevaa majoho ya Kiaskofu na kushika Fimbo ya Uaskofu atahatarishaje usalama? Askofu atavurugaje amani wakati anaongoza matembezi ya amani?

Mayila: Jeshi la Polisi wakiamua kutumia nguvu?

Askofu Mwamakula: Ni uamuzi wao!

Mayila: Jeshi la Polisi wakiamua kukupiga na kukufyatulia risasi za moto?
Askofu Mwamakula: Hata Makaburu wa Afrika Kusini pamoja na uovu wao hawakuthubutu kumfyatulia risasi Askofu Mkuu Desmond Tutu!

Mayila: Wakikuua itakuwaje?

Askofu Mwamakula: Idd Amin alimuua Askofu Mkuu Janan Luwum kule Uganda! Lakini hakufanikiwa kuua ukweli! Wenye mamlaka nchini Tanzania wakiamua kumuua Askofu Mwamakula watakuwa wameingia katika historia ya kuua Askofu! Lakini hawataweza kuua adhma ya Watanzania ya kutaka Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya!

Mayila: Lakini kwa nini usiombe kibari?

Askofu Mwamakula: Huwezi kumuomba kibari mtu ambaye unataka kufanya jambo la kugusa masilahi yake akakukubalia! Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya ni mwiba kwa watawala na hivyo hawapendi hata kuvisikia! Lakini kwa raia hiyo ni haki yao na haki haiombwi!

Mayila: Kwa nini usingeacha vyama vya siasa kufanya?

Askofu Mwamakula: CCM hakitaki Tume Huru ya Uchaguzi na pia Katiba Mpya siyo agenda yao! Vyama vya Upinzani vimetishwa na haviruhusiwi hata kufanya mikutano ya hadhara na maandamano!

Mayila: Sasa wewe utaweza?

Askofu Mwamakula: Ukiona Askofu ameamua kuingia barabarani kwa ajili ya kutetea haki basi ujue hali ni mbaya zaidi! Mimi ni ishara tu! Nyuma ya ishara hiyo kuna umma wa Watanzania! Watanzania wote kwa umoja wao wataweza!

Mayila: Utafanyaje?

Askofu Mwamakula: Kazi yangu ni kuwatia moyo watu walio kata tamaa na kuwaunganisha makundi ya watu walio tayari! Nitawaambia wawe nyuma yangu mimi nitakuwa mbele yao nikiwa nimevalia mavazi ya Kiaskofu na wao watanifuata nyuma!

Mayila: Watu wasipojitokeza kwa hofu utafanyaje?

Askofu Mwamakula: Tuna imani kuwa watu watajitokeza kwa wingi sana! Lakini pia wapo watakaoshindwa kujitokeza kwa sababu ya hofu au hata dharau! Kwa vyo vyote vile mimi nitaendelea kwa kuwa nitakuwa natimiza wajibu wangu! Hata wakati wa Nuhu, watu hawakujitokeza kuchonga safina kwa kuwa walikuwa wanamdharau Nuhu. Lakini kutokujitokeza kwao na dharau zao dhidi ya Nuhu havikuweza kumzuia Nuhu asitimize wajibu wake!

Mayila: Je, huoni kuwa utaonekana kama utakuwa unapingana na Serikali?

Askofu Mwamakula: Kuipinga Serikali siyo kosa kisheria na wala siyo dhambi kama kuna hoja inayofichua uovu, ukengeufu na upotofu wa Serikali. Kama Serikali haitaki kuwepo kwa Tume Huru ya Uchaguzi itakayotenda hai kwa wote na kama Serikali haitaki kuwa na Katiba iliyokubaliwa na wote isiyotoa mianya ya kufinywa kwa haki, basi itakuwa imekengeuka na kupotoka na inakuwa ni halali kuipinga serikali ya namna hiyo!
 
Mayila: Watu wasipojitokeza kwa hofu utafanyaje?

Askofu Mwamakula: Tuna imani kuwa watu watajitokeza kwa wingi sana!................


Sasa hiyo imani ya kwamba watu watajitokeza kaijenga kwa msingi upi maana kama watu waliogopa kujitokeza kwenye yale maandamano ya Lissu ndio hawatoogopa kujitokeza kwenye hayo matembezi endapo jeshi la polisi itakataza?
 
Askofu Mwamakula amenena vema. Bila shaka anaonekana ni thabiti katika dhamira yake.

Watanzania wenye dhamira njema kwa Taifa letu, wanaoraka Tanzania uwe mahali pazuri, penye matumaini kwa kila raia, tumwunge mkono Baba Askofu, kila mmoja kwa namna anayoiweza. Kwa kufanya hivyo wala hatumfaidishi chochote Askofu bali ni kwaajili ua faida yetu sote, watoto wetu na wana wa wana wetu.

Askofu, Mungu aendelee kusimama nawe, azidi kukuimarisha, lakini zaidi atupe sisi sote ujasiri, atuondolee unafiki, na kutujaza hekima ya kupigania ustawi wa Taifa letu.
 
Mapambano yanaendelea, twende twende twende.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Na wewe falasana unaitoa wapi iman kuwa watu hawatajitokeza??
Mayila: Watu wasipojitokeza kwa hofu utafanyaje?

Askofu Mwamakula: Tuna imani kuwa watu watajitokeza kwa wingi sana!................


Sasa hiyo imani ya kwamba watu watajitokeza kaijenga kwa msingi upi maana kama watu waliogopa kujitokeza kwenye yale maandamano ya Lissu ndio hawatoogopa kujitokeza kwenye hayo matembezi endapo jeshi la polisi itakataza?
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Mboyoyo mingi tu.Hana huo ubavu hata chembe bwana "mshauri wa kiroho".
 
Na wewe falasana unaitoa wapi iman kuwa watu hawatajitokeza??
Sasa mkuu unanitukana kwa sababu ipi ni kipi nilichokukosea hadi unitukane? Swali lililoulizwa kwenye mahojiano limeeleza kabisa wasiwasi wa watu kutojitokeza kwa sababu ya hofu,na mimi nimekazia kwa kukumbushia maandamano ya Lissu ambayo watu hawakutokea kwa hofu ya polisi,sasa Askofu angesema kwanini anaamini watu watatokea kwenye hayo matembezi? maana hata kwa Lissu ilionekana sababu ya maandamano ni kubwa na ya msingi hivyo ikaaaminika kwamba watu lazima watatokea bila kujali chochote ila mwisho wa siku kisingizio ikawa polisi kwa watu walihofia polisi.
 
Kwanini jeshi la polisi likataze matembezi ya amani ya madai halali? Je jeshi la polisi wajibu wake ni kuzuia upatikanaji wa katiba mpya na tume huru ya uchaguzi?
Mimi raia kama wewe sasa kama wewe huna jibu la hilo swali unadhani mie ndio nitakuwa na hilo jibu?

Nadhani hapa cha muhimu ni kuacha uoga muingie mtaani kudai haki zenu bila kuhofia polisi maana hakuna siku ambayo jeshi la polisi litawaachia tu muingie barabarani na kuda kudai haki zenu.
 
Back
Top Bottom