Askofu Mwamakula azungumzia "matembezi ya hiyari"!

Askofu Mwamakula azungumzia "matembezi ya hiyari"!

Mayila: Watu wasipojitokeza kwa hofu utafanyaje?

Askofu Mwamakula: Tuna imani kuwa watu watajitokeza kwa wingi sana!................

Sasa hiyo imani ya kwamba watu watajitokeza kaijenga kwa msingi upi maana kama watu waliogopa kujitokeza kwenye yale maandamano ya Lissu ndio hawatoogopa kujitokeza kwenye hayo matembezi endapo jeshi la polisi itakataza?
Na kwa uoga huo huo wakae kimya wanapodhughulikiwa na Mtawala.
 
Mimi raia kama wewe sasa kama wewe huna jibu la hilo swali unadhani mie ndio nitakuwa na hilo jibu?

Nadhani hapa cha muhimu ni kuacha uoga muingie mtaani kudai haki zenu bila kuhofia polisi maana hakuna siku ambayo jeshi la polisi litawaachia tu muingie barabarani na kuda kudai haki zenu.

Sijaelewa, kudai katiba mpya lazima watu wapigwe ndio waipate?
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Huyu askofu sijui anahangaika na nini
 
Huyu askofu Yuko imara Sana ila watz akili zetu hazipo hivyo Kama askofu anavyodhania
 
Sijaelewa, kudai katiba mpya lazima watu wapigwe ndio waipate?

Mayila: Lakini kwa nini usiombe kibari?

Askofu Mwamakula: Huwezi kumuomba kibari mtu ambaye unataka kufanya jambo la kugusa masilahi yake akakukubalia! Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya ni mwiba kwa watawala na hivyo hawapendi hata kuvisikia! Lakini kwa raia hiyo ni haki yao na haki haiombwi!

Kwahiyo mkuu hapa tunazungumzia suala la watu kudai haki yao hivyo hata ikilazimu kupigwa ama kupigana ni sawa ili haki ipatikane.
 
Hivi mbona hayo maandamano au matembezi hayafanyiki kila siku ni stori tu? Ni lini hasa yatafanyika?
 
Hivi mbona hayo maandamano au matembezi hayafanyiki kila siku ni stori tu? Ni lini hasa yatafanyika?
Halafu huku mtaani sisikii watu kuyazungumzia hayo matembezi zaidi ya huku mitandaoni tu,kwa Lissu pia ilikuwa kama hivi.
 
Huyu inawezekana kila siku anavyotembea ndio anaita matembezi ya hiari..maana hiyo hadithi toka mwaka jana.
 
Hawa maaskofi sijui wanatumika kwa maslahi ya nani? Afande Magufuli mpuuzie huyu mtu kama ulivyompuuza Tundu Lisu na ukaibuka mshindi.
 
Kwa watanzania si rahisi kujitokeza...... he needs another strategy, not this one!
wewe na wenzako watano humu jamiiforums,mkijumuisha na mashangazi wawili wa taifa mnatosha kabisa kufikisha ujumbe mkiungana na huyo baba askofu.

wewe pia ni mtanzania mtafuta haki.
 
Mayila: Lakini kwa nini usiombe kibari?

Askofu Mwamakula: Huwezi kumuomba kibari mtu ambaye unataka kufanya jambo la kugusa masilahi yake akakukubalia! Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya ni mwiba kwa watawala na hivyo hawapendi hata kuvisikia! Lakini kwa raia hiyo ni haki yao na haki haiombwi!

Kwahiyo mkuu hapa tunazungumzia suala la watu kudai haki yao hivyo hata ikilazimu kupigwa ama kupigana ni sawa ili haki ipatikane.
huyu mzee anatafutia watu sababu wamtengue kiuno tu.
 
Dhambi huwezi kuichunguza kwa mtu mmoja mmoja ila mwenendo wa serikali unaweza kuchunguzika vyema[emoji382]
kama maisha yako tu yanakuchanganya,utaweza kuelewa mwenendo wa serikali kweli!!!

paul makonda.
 
Naa wewe umemkalia kooni kweli kweli huyo askofu, kila anachosema unakidaka mazima mazima. Inaonekana ndiyo hope yako pekee iliyobaki baada ya kukimbiwa na yule msepaji
 
Back
Top Bottom