Hili lina uhusiano na Sakata la Bandari. Tumeambiwa Waarabu wamewahonga viongozi wetu Fedha na Majumba.Askofu Mwamakula kakosea timing ya tamko lake. Maoni yake haya alipaswa akae nayo kifuani ili kuondoa propaganda za wanaotaka kutumia dini kuua umoja wa kitaifa kwenye kuukataa mkataba huu.
Sasa amewapa ammunition akina Mwaipopo waliyokuwa wanaitafuta.
Njia ya kudeal na akina Mwaipopo ni kuwaignore ili ujinga wao ujionyeshe wenyewe. uachie umma udeal nao kwenye tit for tat, ila Askofu wewe inabidi uconcentrate ktk hoja za mkataba ulivyo.
Ukishaanza kuhoji misikiti, unaibua hisia za waislamu kuwa kumbe wewe ugomvi wako siyo mkataba bali una ugomvi na waislamu kitu ambacho pengine si kweli.
Kumbe DPW hawakuishia hapo, wamehonga mpaka nyumba za Ibada. Huenda baada ya taarifa hii tutasikia hao Waarabu wamehonga kitu gani kingine.
Nadhani sasa ni vizuri tukamuacha Muarabu anayetuhumiwa ajisafishe mwenyewe.
Sisi Wabongo kupambana kumsafisha DPW inaashiria kwamba ni yeye anayepambana lakini kupitia mifukoni mwetu.
Binafsi nampenda sana mama lakini bado tunao wajibu wa kumsaidia kuujua ukweli kwamba HARUFU mbaya imeenea Mijini na Vijijini, Misikitini na Makanisani, vijiweni na kwenye Clubs za starehe, kwenye vyombo vya usafiri na Maofisini.
Tumsaidie mama kwa kumwambia ukweli