Kampuni ya DP World ambayo katika Mkataba wa Bandari kati ya Ufalme wa Dubai na Serikali ya Tanzania ndiyo imepewa kuendesha Bandari zote Tanzania Bara (Tanganyika) inatumia faida inayopata katika biashara zake kusaidia misikiti na Waislamu kwa ujumla.
Mwaka huu wakati wa mfungo wa Radhamani, wawakilishi wa DP World walitembelea Mbeya ambako waliahidi kujenga Msikiti wa Masjid Al Jumaa na misaada mbalimbali. Baada ya hapo walisema wanakwenda Zanzibar ambako nako pia watafanya hayo hayo.
Video:
Video hii imerekodiwa kwa lugha ya Kingereza na Kiswahili na ilichukuliwa Mkoani Mbeya! Je, ulijua kuwa Kampuni ya DP ina malengo pia ya kukuza Uislamu mahali popote pale inapokuwa duniani? Je, ulijua kuwa DP World ina malengo ya kidini? Je, unafikiri hii ndiyo sababu Sheikh Mwaipopo alitoa kauli kali ya kutisha na kuonya Waislamu wasihudhurie Mkutano wa Temeke wa 23 Julai 2023 uliolenga kujadili na kuhoji Mkataba wa Bandari unaolalamikiwa sana?
Je, unafikiri kwa nini wawakilishi wa DP World walipofika hawakutembelea Makanisa, viwanja vya michezo, vyuo vikuu badala yake waliamua kutembelea Misikiti na kuahidi kutoa misaada huko? Je, faida watakayopata DP World katika kuendesha Bandari zetu itatokana na Kodi za Waislamu pekee?
Je, unafikiri moja ya sababu za Spika Dkt. Tulia kuutetea Mkataba wa Bandari na kufikia hatua ya kuwaita wanaoupinga kuwa ni 'wapumbavu wasiosha upumbavu wao' ni pamoja na hao DP World kutembelea Mbeya na kuwasidia wapiga kura wake Waislamu kwa kuaahidi kuwajengea Msikiti wa Masjid Al Jumaa?
Usimkarikie Askofu Mwamakula kwa kuandika haya na kuweka video hii hapa, wakasikirikie DP World kwa kuweka malengo yao wazi kuwa wanasaidia misikiti na sio dini nyingine. Pia, walaumu waliovujisha video hii hadi ikamfikia Askofu. Je, ni nani sasa anayeleta udini katika mjadala huu wa Mkataba wa Bandari? Je, ni DP World au wanaoupinga Mkataba wa Bandari?
Je, kuweka hadharani habari hizi ni uchochezi, uhalisia au uzalendo? Je, ni kwa nini viongozi wa Serikali na CCM hawaweki wazi wananchi katika mikutano yao ya hadhara kuwa faida mojawapo ya DP World ni pamoja na kujenga misikiti na kusaidia Uislamu? Je, ni kwa nini hili linafichwa wakati liko wazi hata katika malengo ya DP World? Kama Serikali haikujua malengo hayo, Waarabu hao wangesafiri hadi Mbeya kwa kificho na kuahidi kujenga misikiti nchini?
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 26 Julai 2023; 07:55 am.
Sasa twende mbele turudi nyuma, kuna ubaya gani taasisi ya nje kutoa misaada ya kuendeleza dini mojawapo nchini?
Ghadafi alijenga msikiti mkubwa Dodoma, hata kama angejenga chuo kikuu cha ki Islam, au benk, kuna shida gani? Kwani wa Islam sio wa Tanzania? Je hawastahili msaada kutoka taasisi za, nje zenye mlengo kama wao?
Hapa nchini kuna shule zinafadhiliwa na uturuki, Iran, sasa Dp world kutoa msaada wa, kijamii kwa wa Islam kwanini iwe nongwa? DP world, inatoka nchi ya, ki Islam sasa kimantiki, ulitaka ije kutoa msaada, wa, biblia, rozali na kujenga makanisa?
Wabongo tujifunze critical thinking, sio kuwa emotional na kumeza kila kitu tunacholishwa na hawa alarmists.
Nimefatilia kesi huko ulaya, ambapo tumeshitakiwa, Ambapo Prof Mruma, na wenzie wanajaribu kujitetea, nimegundua, Serikalini, na wizarani kuna wajinga wengi, na vilaza, hawa maofisa kwenye wizara zetu, ni incompetent kanisa, hawa na weredi kabisa,ukiacha kutokuwa na command ya kizungu vzr,lakini hawajiamini, wanababaika, yaani wanaonyesha picha ya unyonge,utafikiri mbongo kafikishwa kituo cha police! Nimeshindwa kuamini kama ndio hawa, wanaotufanyia fujo na vingora vyao wakiwa barabarani na V8 za, STL, STM, STK!
Tupunguze ujinga,Ulaya, Israel, ina,taasisi nyingi zinazosaidia makanisa, na, wakristo, sasa ikija taasisi inataka, kusaidia wa Islam kwanini inakuwa nongwa? Ubaya, upo wapi? Msikiti ni nyumba ya, ibada,sasa, ikijengwa Mbeya, ubaya, upo wapi? Kwani, kuna watu wanalazimishwa kuslim?
Kama, mkataba ni mbaya,tuonyeshe ubaya, tuache hizi, propaganda, za, kijinga.Mkapa alitoa majengo ya chuo cha ufundi cha tanesco kidatu, na kuyagawa kwa wa Islam ndio kikaanzishwa chuo kikuu cha ki Islam morogoro!
Kwa vile alitoa raisi mkristo kwenda kwa Islam, waafidhina wa kikristo, hawa kupiga kelele Sana, ingekuwa ametoa Raisi muislam, kwenda, kwa wa Islam, kelele kutoka kwa wakristo wajinga zingekuwa nyingi.
Tuonyeshe ubaya wa kiuchumi wa mkataba, na wizi ufisadi wa ccm, tuache propaganda za, kijinga.