YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,900
- 52,056
Kasimikwa na BakwataAu sheikh al adi kasimikwa na nani?? Tafiti juu ya uyu sheik ubwabwa wa ccm.
Sie tunazingatia ujumbe wake zaidi
Kasimikwa na BakwataAu sheikh al adi kasimikwa na nani?? Tafiti juu ya uyu sheik ubwabwa wa ccm.
Sie tunazingatia ujumbe wake zaidi
Mbona umemshambulia kwa nguvu mkuu!Hivi wewe unamjua Mwamakula au unamsikia na kumuona tu kwenye mitandao ya kijamii,je unalijua hilo kanisa lake hata lilipo na je unajua huo''uaskofu ''kasimikwa na nani na alipata wapi,huyu ni sawa na kusikia kuwa kuna chuo kikuu kinaitwa Sokwine wakati tuna chuo kinaitwa Sokoine...
Mbona umemshambulia kwa nguvu mkuu!..
Kasimikwa na Bakwata
Mazao ya Kyela ukiwemo mpunga na mchele hauna wanunuziTanzania imekuwa kama nchi ya Zaire ya Mobutu kitu kizuri kikifanyika utasikia tunamshukuru rais wetu mpendwa, Mambo yakienda shagharabhaghala wanalaumiwa wapinzani na mabeberu! Mf.kuanguka bei za mazao hutasikia jina la rais likitajwa.
Mkuu sio namshambulia bali naeleza ukweli wa huyu askofu wenu sababu namfahamu fika,sasa mtu mjanja anapoleta porojo ambazo najua anafanya hivyo kwa lengo la kupotosha inabidi kwanza niseme tabia yake na wasifu wake.Mbona umemshambulia kwa nguvu mkuu!
Au na wewe ni miongoni mwa"wachache wanaonufaika na mfumo uliopo" (BAK,2020).
Katika hali ya kawaida,nilitegemea ungejikita kueleza namna mfumo uliopo unavyotenda haki, ili kuonyesha kwamba malengo ya matembezi yalipangwa hayaba mashiko.
Lakini kujikita kumshambulia "askofu" ni ishara ya wewe kuwa dhaifu mno...
Sent from my Z9 using JamiiForums mobile app
Ni kweli kabisa unalolisema lakini yeye anatumia mwamvuli wa dini kusema mambo yasiyohusiana na dini,kwa maana tusichanganye mwavuli wa dini kuendeleza nia zetu mtu wa dini unatakiwa uwe mkweli na simpotoshaji,huyu anayejiita askofu kutwa yupo mitandaoni basi si afanye tu siasa badala ya dini na siasa yenyewe ni kuwa mwana Chadema,na haya si ndio tunayoyapinga kwa hawa watumishi wa dini ambao kutwa wapo majukwaani wakiwa na wanasiasa?huko Rwanda hawa hawa tunaowasifu ndio walioanzisha mauaji ya kimbali.Lakini ni Mtanzania anaetumia haki yake ya kikatiba kutoa maoni yake.
Au ninasema uongo ndugu zangu?
Nani kasema mpunga au mchele hauna wanunuzi Kyela hii ,wewe upo Kyela au Dar Es Salaam,nenda kwenye masoko na mashineni kama utaona mchele au mpunga hauna wanunuzi au umekosa soko, sasa mchele ni 25000-30000 kutoka 21000 mwezi July, walanguzi ndio wamehifadhi mpunga wakisubiri bei zipande. Mkuu punguza mahaba ya siasa kwenye mambo yasiyo ya kisiasa,njoo Kyela uone au ni DM nikutembeze ukija.Mazao ya Kyela ukiwemo mpunga na mchele hauna wanunuzi
Kapotosha nini Baba Askofu Mwamakula? Hebu fafanua upotoshaji wake.Ni kweli kabisa unalolisema lakini yeye anatumia mwamvuli wa dini kusema mambo yasiyohusiana na dini,kwa maana tusichanganye mwavuli wa dini kuendeleza nia zetu mtu wa dini unatakiwa uwe mkweli na simpotoshaji,huyu anayejiita askofu kutwa yupo mitandaoni basi si afanye tu siasa badala ya dini na siasa yenyewe ni kuwa mwana Chadema,na haya si ndio tunayoyapinga kwa hawa watumishi wa dini ambao kutwa wapo majukwaani wakiwa na wanasiasa?huko Rwanda hawa hawa tunaowasifu ndio walioanzisha mauaji ya kimbali.
TANZANIA! TANZANIA! TANZANIA! SIKIA SAUTI YA ASKOFU!
Askofu Mkuu Oscar Romero wa Kanisa [Roman] Katoliki nchini El Salvador alipokuwa akitetea haki hakuwa na nia ya kugombea nafasi za kisiasa nchini El Salvador! Askofu Mkuu Desmond Tutu wa Kanisa Anglikana Afrika Kusini Alipotetea haki hakuwa na lengo la kupata uteuzi wa kisiasa nchini Afrika Kusini!
Kadharika, Askofu Mkuu Janani Luwum wa Church of Uganda (Kanisa Anglikana la Uganda) alipotetea haki nchini Uganda hakuwa na nia ya kutafuta nafasi za kisiasa katika nchi ya Uganda! Pia Askofu Henry Okullu wa Kanisa Anglikana Kenya alipopigania haki hakuwa anatamani kugombea nafasi za kisiasa nchini Kenya!
Maaskofu wa Kanisa Katoliki walipoamua kusaidia maridhiano katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo hawakukusudia kuchukua nafasi za kisiasa katika DRC! Maaskofu wa Malawi walipopambana kuondosha mfumo wa kidikiteta na kupigania haki katika nchi ya Malawi wakati wa Rais Hastings Kamuzu Banda hawakuwa wanatamani nafasi za kisiasa!
Katika Tanzania ya leo, Askofu Mwamakula pamoja na Maaskofu wengine wanapotetea haki, Tume Huru ya Uchaguzi, na Katiba Mpya sio kuwa wanatamani nafasi za kisiasa! Kama walivyofanya watangulizi wao katika nchi zao kama ilivyoelezwa hapo juu, Maaskofu wa Tanzania na wao wanatimiza wajibu wao unaombatana na Wito wao Mkuu uliothibitishwa kupitia viapo vya Kiaskofu!
Haiwezekani katika jamii wakakaa kimya wote! Jamii ambayo watu wote wamenyamazishwa na kukubali kukaa kimya inakuwa imeondokewa na dhamiri ya Mungu! Tunaamini kuwa Tanzania bado ina dhamiri ya Mungu ndio maana sauti za Maaskofu hata kama ni chache sana zingali zinasikika!
Usipotoshwe na wala usitishwe na watu wachache wanaonufaika na mfumo usiotenda haki! Ungana na Askofu Mwamakula katika "Matembezi ya Hiyari" ya kuhamasisha umuhimu wa Kuundwa Tume Huru ya Uchaguzi na kuandikwa kwa Katiba Mpya!
Askofu atawajulisha Watanzania wote na ulimwengu kwa ujumla tarehe ya kuanza kwa matembezi hayo!
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula.