Askofu Mwamakula: Haiwezekani katika jamii wakakaa kimya wote!

Mbona umemshambulia kwa nguvu mkuu!

Au na wewe ni miongoni mwa"wachache wanaonufaika na mfumo uliopo" (BAK,2020).

Katika hali ya kawaida,nilitegemea ungejikita kueleza namna mfumo uliopo unavyotenda haki, ili kuonyesha kwamba malengo ya matembezi yalipangwa hayaba mashiko.

Lakini kujikita kumshambulia "askofu" ni ishara ya wewe kuwa dhaifu mno...

Sent from my Z9 using JamiiForums mobile app
 
It's human nature you can kill all but you can't silence all
 
Tanzania imekuwa kama nchi ya Zaire ya Mobutu kitu kizuri kikifanyika utasikia tunamshukuru rais wetu mpendwa, Mambo yakienda shagharabhaghala wanalaumiwa wapinzani na mabeberu! Mf.kuanguka bei za mazao hutasikia jina la rais likitajwa.
Mazao ya Kyela ukiwemo mpunga na mchele hauna wanunuzi
 
Mkuu sio namshambulia bali naeleza ukweli wa huyu askofu wenu sababu namfahamu fika,sasa mtu mjanja anapoleta porojo ambazo najua anafanya hivyo kwa lengo la kupotosha inabidi kwanza niseme tabia yake na wasifu wake.
 
Lakini ni Mtanzania anaetumia haki yake ya kikatiba kutoa maoni yake.

Au ninasema uongo ndugu zangu?
Ni kweli kabisa unalolisema lakini yeye anatumia mwamvuli wa dini kusema mambo yasiyohusiana na dini,kwa maana tusichanganye mwavuli wa dini kuendeleza nia zetu mtu wa dini unatakiwa uwe mkweli na simpotoshaji,huyu anayejiita askofu kutwa yupo mitandaoni basi si afanye tu siasa badala ya dini na siasa yenyewe ni kuwa mwana Chadema,na haya si ndio tunayoyapinga kwa hawa watumishi wa dini ambao kutwa wapo majukwaani wakiwa na wanasiasa?huko Rwanda hawa hawa tunaowasifu ndio walioanzisha mauaji ya kimbali.
 
Mazao ya Kyela ukiwemo mpunga na mchele hauna wanunuzi
Nani kasema mpunga au mchele hauna wanunuzi Kyela hii ,wewe upo Kyela au Dar Es Salaam,nenda kwenye masoko na mashineni kama utaona mchele au mpunga hauna wanunuzi au umekosa soko, sasa mchele ni 25000-30000 kutoka 21000 mwezi July, walanguzi ndio wamehifadhi mpunga wakisubiri bei zipande. Mkuu punguza mahaba ya siasa kwenye mambo yasiyo ya kisiasa,njoo Kyela uone au ni DM nikutembeze ukija.
 
Kapotosha nini Baba Askofu Mwamakula? Hebu fafanua upotoshaji wake.
 
Bandekila aka Bak
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…