Askofu Mwamakula napingana nawe na tutaona fimbo ya Haruni ni ipi?

Nimefatilia maandiko mengi ya Askofu Mwamakula kuhusu Rais Magufuli. Nimependa kumwambia ameibuka kuwa mtaabishaji wa nchi hii na kwasababu analitaja Jina la Jehovah basi Mkonoa wa Jehovah utaamua kati yake na Rais Magufuli.

Nimkumbushe tu! Vita anayifanya na Rais Magufuli anafanya vita na Mungu aliyeruhusu akaketi kwenye hicho kiti. Aliwaaminisha Watanzania kuwa Mungu amemuonesha Lisu ni Rais. Kama mtumishi wa Mungu kutoa neno ambalo halikuwa ni ishara tosha kuwa hana Roho wa Mungu na alitakiwa kuvua Joho la Kichungaji. Amedhihirisha Mungu wake ni dhaifu kushindwa kuzuia wizi wa kura anaoutaja.

Makanisa na Miaikiti nchi nzima imeungana kumuombea Rais Magufuli yeye anakuja na ngonjera. Basi tutaona fimbo ya Haruni itakapochanulia.

Kwa kifupi ni hivi:-
Ask Mwamakula ni Askofu asiyemtambua Rais Magufuli na kwa sisi Wakristo hapo ni moja kwa moja AMEKANYAGA NENO LA MUNGU Kwani Mungu humpa amtakaye na humnyima asiyemtaka, Mamlaka lazima ziheshimiwe. Warumi 13

Askofu Mwamakula hatambui uwezo uliopo NDANI YA DAMU YA YESU KRTISTO NA JINA LA YESU. Waefeso 2:13-16 kwwnini asiitumie Damu ya Yesu kuleta upatanisho pale anapoona hakuna? Jina na Damu ya Yesu INALINDA NA INAPONYA

Askofu Mwamakula ANA ULIMI WA HATARI KAMA NYOKA NA MDOMONI MWAKE MNA MANENO YA SUMU YA FIRA (Zaburi 140:3)

Leo asubuhi kwenye maombi ya alfajiri Mchungaji alitupitisha kwenye Zaburi ya 140. Tulitumia Zaburi hii kumuombea Rais Magufuli.
1. Mungu amlinde na watu wakatili wanaomzushia kifo na magonjwa
2. Mungu amlinde na watu wanaomuwazia mabaya
3. Mungu amlinde na mashindano ya ndimi zenye sumu ya fira na ulimi wa nyoka
4. Mungu amlinde na makucha ya wabaya
5. Mungu amlinde watu wenye kiburi waliomtegea mitego na kamba kama wavu
6. Mungu asikilize maombi yake
7. Mungu aendelee kumkinga awe salama mikononi mwake
8. Mungu asiwape waovu wanayoyataka, wala mipango yao mibaya isifanikiwe
9. Mungu amtetee, maneno yote maovu yawapate wenyewe
10. Mungu asababishe makaa ya motoyawaangukie wenyewe watumbukie shimoni wasiinuke tena
11. Mungu asababishe wasengenyaji wote na wazushi wasifanikiwe ktk nchi
12. Mungu amtetee mtumishi wake, atete nao wanaoteta naye
13.Mungu amfanye mtumishi wake mwadilifu na mnyoofu kulisifu jina lake na kukaa kwake.

Ask Mwamakula kwa mara nyingine Mungu anaenda kuudhihirishia ulimwengu wewe sio mtumishi wake. Badilika fanya kazi uliyoitiwa ya kuokoa waliopotea na kuhubiri Injili ya Amani na Mungu atakubariki. Amen
Kabla uzi haujajaa nikukumbushe...

2015 Gwajima alituambia Lowassa ni chaguo la Mungu na hakuwa rais....

2020 Gwajima akasema Magufuli ni chaguo la Mungu baada ya kushughulikiwa na Bashite.

Si kila mamlaka ya kidunia inatoka kwa Mungu. Nyingine ni za hapa hapa na nyingine zinatoka kwa mnayemuita Shetani...

Dunia hii haitawali Mungu pekee... Shetani ana mamlaka pia....

Siku njema.
 
kuhusu kwamba alioneshwa kuwa lisu ni rais, huwezi kuwa na hakika kabisa kwamba alidanganya, kama ni jambo la kiroho na kama kuna wizi wa kura ulifanyika kweli, mbingu zitamtambua aliyetabiriwa kwamba ndie rahisi halafu huyo wa kimwili ataondelewa kidogo kidogo : case study Daudi na Sauli
Usiwe mbirikimo wa fikra,hakuna siku mpango wa mungu umezuiliwa wanadamu,kama mungu alikuwa amepanga lissu awe rais 2020,hakuna angezuia,mungu hawezi kushindwa na wanadamu,ni kama wewe leo hapo ulipo,mungu akitaka kkuinua wabaya wako hawatazuia ,
 
Mkuu, Warumi 13 inataka watu kutii mamlaka, sasa ilikuwaje Mwl. Nyerere na wenzake walianza kupinga mamlaka (serikali) ya Muingereza miaka ya 1950?
Kutawaliwa na mtu asiyetokana na ardhi husika ni laana. Mwl. Nyerere alikuwa sahihi na alisimama na Biblia
 
Nimefatilia maandiko mengi ya Askofu Mwamakula kuhusu Rais Magufuli. Nimependa kumwambia ameibuka kuwa mtaabishaji wa nchi hii na kwasababu analitaja Jina la Jehovah basi Mkonoa wa Jehovah utaamua kati yake na Rais Magufuli.

Nimkumbushe tu! Vita anayifanya na Rais Magufuli anafanya vita na Mungu aliyeruhusu akaketi kwenye hicho kiti. Aliwaaminisha Watanzania kuwa Mungu amemuonesha Lisu ni Rais. Kama mtumishi wa Mungu kutoa neno ambalo halikuwa ni ishara tosha kuwa hana Roho wa Mungu na alitakiwa kuvua Joho la Kichungaji. Amedhihirisha Mungu wake ni dhaifu kushindwa kuzuia wizi wa kura anaoutaja.

Makanisa na Miaikiti nchi nzima imeungana kumuombea Rais Magufuli yeye anakuja na ngonjera. Basi tutaona fimbo ya Haruni itakapochanulia.

Kwa kifupi ni hivi:-
Ask Mwamakula ni Askofu asiyemtambua Rais Magufuli na kwa sisi Wakristo hapo ni moja kwa moja AMEKANYAGA NENO LA MUNGU Kwani Mungu humpa amtakaye na humnyima asiyemtaka, Mamlaka lazima ziheshimiwe. Warumi 13

Askofu Mwamakula hatambui uwezo uliopo NDANI YA DAMU YA YESU KRTISTO NA JINA LA YESU. Waefeso 2:13-16 kwwnini asiitumie Damu ya Yesu kuleta upatanisho pale anapoona hakuna? Jina na Damu ya Yesu INALINDA NA INAPONYA

Askofu Mwamakula ANA ULIMI WA HATARI KAMA NYOKA NA MDOMONI MWAKE MNA MANENO YA SUMU YA FIRA (Zaburi 140:3)

Leo asubuhi kwenye maombi ya alfajiri Mchungaji alitupitisha kwenye Zaburi ya 140. Tulitumia Zaburi hii kumuombea Rais Magufuli.
1. Mungu amlinde na watu wakatili wanaomzushia kifo na magonjwa
2. Mungu amlinde na watu wanaomuwazia mabaya
3. Mungu amlinde na mashindano ya ndimi zenye sumu ya fira na ulimi wa nyoka
4. Mungu amlinde na makucha ya wabaya
5. Mungu amlinde watu wenye kiburi waliomtegea mitego na kamba kama wavu
6. Mungu asikilize maombi yake
7. Mungu aendelee kumkinga awe salama mikononi mwake
8. Mungu asiwape waovu wanayoyataka, wala mipango yao mibaya isifanikiwe
9. Mungu amtetee, maneno yote maovu yawapate wenyewe
10. Mungu asababishe makaa ya motoyawaangukie wenyewe watumbukie shimoni wasiinuke tena
11. Mungu asababishe wasengenyaji wote na wazushi wasifanikiwe ktk nchi
12. Mungu amtetee mtumishi wake, atete nao wanaoteta naye
13.Mungu amfanye mtumishi wake mwadilifu na mnyoofu kulisifu jina lake na kukaa kwake.

Ask Mwamakula kwa mara nyingine Mungu anaenda kuudhihirishia ulimwengu wewe sio mtumishi wake. Badilika fanya kazi uliyoitiwa ya kuokoa waliopotea na kuhubiri Injili ya Amani na Mungu atakubariki. Amen
Askofu Mwamakula yupo.

Mwamakula ni Malafyale yupo huko Kigamboni huyo mwingine .... I can't mention his name. Am sorry
 
Kabla uzi haujajaa nikukumbushe...

2015 Gwajima alituambia Lowassa ni chaguo la Mungu na hakuwa rais....

2020 Gwajima akasema Magufuli ni chaguo la Mungu baada ya kushughulikiwa na Bashite.

Si kila mamlaka ya kidunia inatoka kwa Mungu. Nyingine ni za hapa hapa na nyingine zinatoka kwa mnayemuita Shetani...

Dunia hii haitawali Mungu pekee... Shetani ana mamlaka pia....

Siku njema.
Hakuna jambo linalotokea chini ya jua isipokuwa Mungu ameliruhusu. Shetani hana nguvu kumshinda Mungu!
 
Mkuu, Warumi 13 inataka watu kutii mamlaka, sasa ilikuwaje Mwl. Nyerere na wenzake walianza kupinga mamlaka (serikali) ya Muingereza miaka ya 1950?
Nenda tena kasome historia,nyerere hakupinga mamlaka,nyerere alikuwa mtii sana kwenye utawala wa mzungu,nyerere alichokuwa anakifanya ni kutekeleza maelekezo na mpango wa baraza la udhamini la LG,
 
Kwenye mambo kama haya nakumbuka mawaidha ya baadh ya maostadh kua.

Siku ya mwisho mbele ya mwenyez mungu utaulizwa umeufanyia nini uislam.
Maana uislam unakumbwa na misukosuko mingi huko duniani sasa wewe umeutetea vip!!

Sasa chukulia wewe unaulizwa haya mbele ya hukum wakati huo kule ulikotoka ulikua kibaraka wa wale wanaoutesa uislam na watu wangine.

Kwahiyo mwamakula iwapo atakua anatetea watu wanaoteseka kweli kutoka moyoni basi tetea maana hata yesu alisema USIOGOPE KINACHOUA MWILI,OGOPA KINACHO UA ROHO.

Hivyo anachohangaikia mwamakula kama ni haki basi hata akikaa mbele ya haki siku hiyo atakalibishwa na gras ya maziwa mbele ya mwenyez mungu halafu ndio mahojiano yanaanza.

KUTII MAMLAKA ILIYOPO SIO KUACHA KUTETEA KAMA KUNA WANAOUMIZWA HATA KWA KUONEWA.
Yesu alipokuja duniani alikuja na agenda kuu ya kushughulikia dhambi. Na kazi hiyo amewapa watumishi wake. Shida kubwa ni dhambi mengine yanafuata. Angejikita kushughulikia dhambi na kuhubiri amani na uoatanisho hakika Mungu angeshusha neema yake mapema.

Tatizo anafanya vita mwilini badala ya rohoni. Maana yake analazimishia haja ya moyo wake na sio mapenzi ya Mungu. Hafai kuwa Mchungaji.
 
Wewe mwanamke una shida sana! Kwa namna unavyo mtetea huyo mzee, naamini utakuwa unafahamu hata kinacho endelea mpaka muda huu bila shaka.
Sina mashaka na viongozi wangu Mhe. Kassim Majaliwa PM na Mhe. Samia Suluhu VP. Wewe kumbe huwaamini hawa? Sasa unamuamini Ask Mwamakula na hao waliopo nje ya nchi zaidi ya viongozi hawa?
 
Hakuna jambo linalotokea chini ya jua isipokuwa Mungu ameliruhusu. Shetani hana nguvu kumshinda Mungu!
Unaelekea kuwa maandiko unayasoma kama usomavyo vitabu vya Abunuasi, Alfu Lela ulela, Kalumekenge nk lakini hutafakari.
Unataka kutuambia kupotea watu, mauaji, ufisadi, wizi wa kura nk ni matukio yanayo tokea chini ya jua kwa ruhusa ya Mungu?
Acha mihemko kama ya Gwajima na bibie!
 
Nenda tena kasome historia,nyerere hakupinga mamlaka,nyerere alikuwa mtii sana kwenye utawala wa mzungu,nyerere alichokuwa anakifanya ni kutekeleza maelekezo na mpango wa baraza la udhamini la LG,
Vipi kuhusu Msumbiji, A. Kusini n.k alizozisaidia kupambana na mamlaka zilizokuwepo?.
 
Back
Top Bottom