Askofu Mwamakula napingana nawe na tutaona fimbo ya Haruni ni ipi?

Kabla uzi haujajaa nikukumbushe...

2015 Gwajima alituambia Lowassa ni chaguo la Mungu na hakuwa rais....

2020 Gwajima akasema Magufuli ni chaguo la Mungu baada ya kushughulikiwa na Bashite.

Si kila mamlaka ya kidunia inatoka kwa Mungu. Nyingine ni za hapa hapa na nyingine zinatoka kwa mnayemuita Shetani...

Dunia hii haitawali Mungu pekee... Shetani ana mamlaka pia....

Siku njema.
 
Usiwe mbirikimo wa fikra,hakuna siku mpango wa mungu umezuiliwa wanadamu,kama mungu alikuwa amepanga lissu awe rais 2020,hakuna angezuia,mungu hawezi kushindwa na wanadamu,ni kama wewe leo hapo ulipo,mungu akitaka kkuinua wabaya wako hawatazuia ,
 
Mkuu, Warumi 13 inataka watu kutii mamlaka, sasa ilikuwaje Mwl. Nyerere na wenzake walianza kupinga mamlaka (serikali) ya Muingereza miaka ya 1950?
Kutawaliwa na mtu asiyetokana na ardhi husika ni laana. Mwl. Nyerere alikuwa sahihi na alisimama na Biblia
 
Askofu Mwamakula yupo.

Mwamakula ni Malafyale yupo huko Kigamboni huyo mwingine .... I can't mention his name. Am sorry
 
Hakuna jambo linalotokea chini ya jua isipokuwa Mungu ameliruhusu. Shetani hana nguvu kumshinda Mungu!
 
Mkuu, Warumi 13 inataka watu kutii mamlaka, sasa ilikuwaje Mwl. Nyerere na wenzake walianza kupinga mamlaka (serikali) ya Muingereza miaka ya 1950?
Nenda tena kasome historia,nyerere hakupinga mamlaka,nyerere alikuwa mtii sana kwenye utawala wa mzungu,nyerere alichokuwa anakifanya ni kutekeleza maelekezo na mpango wa baraza la udhamini la LG,
 
Yesu alipokuja duniani alikuja na agenda kuu ya kushughulikia dhambi. Na kazi hiyo amewapa watumishi wake. Shida kubwa ni dhambi mengine yanafuata. Angejikita kushughulikia dhambi na kuhubiri amani na uoatanisho hakika Mungu angeshusha neema yake mapema.

Tatizo anafanya vita mwilini badala ya rohoni. Maana yake analazimishia haja ya moyo wake na sio mapenzi ya Mungu. Hafai kuwa Mchungaji.
 
Wewe mwanamke una shida sana! Kwa namna unavyo mtetea huyo mzee, naamini utakuwa unafahamu hata kinacho endelea mpaka muda huu bila shaka.
Sina mashaka na viongozi wangu Mhe. Kassim Majaliwa PM na Mhe. Samia Suluhu VP. Wewe kumbe huwaamini hawa? Sasa unamuamini Ask Mwamakula na hao waliopo nje ya nchi zaidi ya viongozi hawa?
 
Hakuna jambo linalotokea chini ya jua isipokuwa Mungu ameliruhusu. Shetani hana nguvu kumshinda Mungu!
Unaelekea kuwa maandiko unayasoma kama usomavyo vitabu vya Abunuasi, Alfu Lela ulela, Kalumekenge nk lakini hutafakari.
Unataka kutuambia kupotea watu, mauaji, ufisadi, wizi wa kura nk ni matukio yanayo tokea chini ya jua kwa ruhusa ya Mungu?
Acha mihemko kama ya Gwajima na bibie!
 
Nenda tena kasome historia,nyerere hakupinga mamlaka,nyerere alikuwa mtii sana kwenye utawala wa mzungu,nyerere alichokuwa anakifanya ni kutekeleza maelekezo na mpango wa baraza la udhamini la LG,
Vipi kuhusu Msumbiji, A. Kusini n.k alizozisaidia kupambana na mamlaka zilizokuwepo?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…