Askofu Mwamakula napingana nawe na tutaona fimbo ya Haruni ni ipi?

Mungu hawezi kuruhusu watu wake waishi kwatabu. Huwa tunamuomba na anatusikia na kutenda huyo ndiye mungu. Tulimuomba lissu apone akamponya ili uwe ushuhuda na tunaomba mungu aondoe kikwazo na ameondoa
 
Magufuli akizindua daraja la ubu go alisema kwamba hamna diwani aliyeshinda kwa kuchaguliwa na wananchi. Ushahidi wa video upo.
Kwa maana hiyo hata wabunge hawakuwa chaguo la wananchi.
Hata yeye pia hakuwa chaguo la wananchi.
Tuliona kasoro nyingi sana za hovyo kwenye uchaguzi huu.
Mwamakula Yuko sahihi
 
Kutawaliwa na mtu asiyetokana na ardhi husika ni laana. Mwl. Nyerere alikuwa sahihi na alisimama na Biblia
So, makabila ya Wangoni, Wairaq na mengine ya wahamiaji hayaruhusiwi kutawala nchi hii?
 
ameibuka kuwa mtaabishaji wa nchi hii
Kwa kuomba Katiba mpya ndio Ghafla amekuwa mtaabishaji wa Taifa?

Vipi kuhusu huyo Mtaabishaji In chief ambaye mpaka sasa maelfu ya roho za Wananchi wasiokuwa na hatia zimeangamia kwenye mikono yake?
 
Mungu hawezi kuruhusu watu wake waishi kwatabu. Huwa tunamuomba na anatusikia na kutenda huyo ndiye mungu. Tulimuomba lissu apone akamponya ili uwe ushuhuda na tunaomba mungu aondoe kikwazo na ameondoa
Mungu yupi mnaemwomba kwa sasa,ambae 2020 hamkumwomba?!, ambae mlimwomba lissu akapona,lkn mkamwomba tena lissu awe rais na mungu akawajibu!!!!, onyesha basi kuwa unazo hata zile akili kidogo,jifunze kufikili kwa usahihi,na ujifunze kutafakari kwa umakini kabla hujaandika chochote,
 
Labda rais wa mashoga!
 
ASKOFU mwamakula ni kiongozi wa kiroho,kazi yake ni upatanishi sio uchonganishi,hiki anachokifanya leo ni kazi ya ibilisi,
ASKOFU mwamakula ni kiongozi wa kiroho,kazi yake ni upatanishi sio uchonganishi,hiki anachokifanya leo ni kazi ya ibilisi,
ASKOFU mwamakula ni kiongozi wa kiroho,kazi yake ni upatanishi sio uchonganishi,hiki anachokifanya leo ni kazi ya ibilisi,
 
Hakuna jambo linalotokea chini ya jua isipokuwa Mungu ameliruhusu. Shetani hana nguvu kumshinda Mungu!
Mpango wa Mungu si kwa jinsi ya kibinadamu Kama ufikiriavyo, Ni kiroho zaid.
Africa ikiwemo Tanzania ilitawaliwa na wakoloni waliowaua na kuwatesa Babu zetu miaka na miaka

Wana wa Israel, Taifa Teule la Mungu, walichukuliwa utumwani Misri miaka kibao na waliteseka jangwan miaka na miaka wakitafuta kurudi nchi ya Ahadi

Waafrika Kusini walitawaliwa, wakateswa, wakauwawa miaka lukuki.

Mpango wa Mungu si mpango wa kibinadamu. Kwa kuwa umeona leo umeiba na ukafanikiwa kuiba na hujakamatwa Sasa jidanganye kuwa Ni Mungu kakuwezesha/kakuruhusu uibe sababu tu hukukamatwa Ila kaa ukijua za mwizi Ni arobaini.

Uongo huwa unafika haraka kileleni lakini haudumu....ukweli unachelewa kufika lakini ukweli ukifika umefika...unadumu
 
Jamani kwa nini watanzania mnakuwa na mibichwa migumu sana kuelewa,mmeambiwa wakati huu ndio wakati muhimu kushikamana kwa haya yaliyokumba taifa



Nazungumzia nzige wa jangwani wakuu na suala la rubani mkenya kutelekeza ndege
 
Upo sahihi.
Ila labda nikukumbushe tu.

Wakati tundurisu anaumizwa watu wa dini mbalimbali.
Wakristo kwa waislam walitamani wamuombee kwa hali ile iyompata,
Matokeo yake watu wakapigwa marufuku kusubutu kufanya hivyo.

Hatakama mtu huyo ni adui yako wewe umeona ni sawa??

Wakati huo kunawatu wanadhalilisha wenzao kwenye majukwaa na kutaka kuombewa kila siku.

Hivi mwenyez mungu kakuweka hapo uwaone watu wa chini yako kama mifugo yako nyumbani ukijisikia uchu unachinja?

Kama hayajafanyika haya useme hapa.

ILA MUNGU NI MKUBWA SIKU ZOTE.
 
Kwahiyo magufuli alipigiwa kula na mungu sio?
 
Askofu Mwamakula - wewe ni mjumbe wa Mungu - tayari tumeanza kuona misukosuko katika taifa.. Maandamano ya kudai haki na katiba mpya yameshaaza bila watu kujijua.

Tupo kwenye maandamano tayari..... (Wiki sasa na ushee)
 
Maombi ya mwenye haki hupokelewa kwa mungu. Maombi ya mtu asiye haki ni chukizo mbele za bwana.

Mungu anajibu kwa wakati. Maombi yamejibiwa
 
Wewe mwanamke una shida sana! Kwa namna unavyo mtetea huyo mzee, naamini utakuwa unafahamu hata kinacho endelea mpaka muda huu bila shaka.
Alipinga serikali kibao za wakoloni kusini msa Afrika mfano, Msumbiji, Zimbabwe, Afrika ya kusini etc.
 
Idd Amin Dada, Jean Baptiste Bokasa, Sam Nguema, Muamar Guadhafi wote ni viongozi wauaji katika historia ya ulimwengu wetu. Je waliwekwa na Mungu?
Idd Amin Dada katika uongozi wake alinyonga na kuua watu kama nzi. Hadi viongozi wa Kanisa aliwachinjilia mbali. Manabii wengi walijitokeza kumpinga wakaambulia makaburi.
Ulivyoandika nakueleza wazi wewe ni mfaidika wa utawala dhalimu. Hata kipindi cha Eliya, Isaya, Jeremia walikuwepo walamba viatu vya wafalme waovu na hata wafitini kama wewe.
Mwamakula ameamua kuwa Yohana Mbatizaji kwa Mtawala/Herodi wa kumwambia wazi kuwa ni vibaya kumnyanganya ndugu yake mkewe yaani Herodia. Kichwa chake kilidaiwa kwenye bakuli la dhahabu na ndivyo ilivyokuwa. Mwamakula yuko tayari kwa lolote kwa kutetea uhai wa watanzania tofauti na wewe unayelamba miguu ya watawala.
Tuachie Mwamakula wetu wewe endelea kula vinono kutoka mezani mwa mtesi wetu. Lakini tunajua mtetezi wetu mkuu yu hai!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…