Askofu Mwamakula: Ole kwa Taifa lisilotenda HAKI kwa watu wake! Unamkamata mtu eti upelelezi haujakamilika karne hii?

Askofu Mwamakula: Ole kwa Taifa lisilotenda HAKI kwa watu wake! Unamkamata mtu eti upelelezi haujakamilika karne hii?

Nikupinge si kweli kila mamlaka utoka Kwa Mungu zitokazo Kwa Mungu utenda ya kumpendeza Mungu.Kwann Africa ndo tunapata mamlaka mbovu heri ya hata wakoloni je Mungu atupendi?Ukisoma biblia Watumishi Wangu karibu wote hawakukaa kimya kusimama na uovu hata ikapelekea wengi kuuwawa soma historia za vifo vya mitume wa Yesu na wengine. Tawala zitokazo Kwa Mungu umeheshimu Mungu.
Mkuu correction; hunipingi mimi utakuwa unapingana na biblia.Hao mitume walikufa sababu ya siasa au sababu ya kuhubiri injili na kuwaasa watu waziache njia zao mbaya?Kama utawala ulikuwa na shida Mungu alituma wajumbe wake wakaongea na mfalme hapo sikatai,ambapo hutaki kunielewa nasema hawa wa leo ,Mungu amewatuma waongee public au ni akili zao wenyewe?Hivi unajua Mungu ni mstaarabu sana,huwa hamdhalilishi mtu kabla ya kumwonya mara nyingi.Unatakiwa ujue mtu mwenye mamlaka ni mtu wa aina gani na anauwezo gani otherwise utaumia.Nafasi anayokuwa nayo ndiyo inampa huo uwezo na siyo yeye,nafasi aliyopewa na nchi.
Jifunze hata kwa wadudu,huwezi mchezea malkia au mfalme wao ukabaki salama.
 
Kwa jinsi unavyo jibu kwa haraka bila hata kutafakari , hata aliye upande unao utetea anajionea kabisa jinsi ulivyo mtupu kwa kichwa.
 
Ili nchi iendelee inahitaji kila mtu abobee kwenye eneo lake mfano mkulima alime Sana, injinia afanye Kazi za uinjinia Sana, askofu afanye Kazi za Uaskofu Sana nk ukiona Askofu anavua kofia la Uaskofu kageukia fani ya Sheria au upelelezi ujue nchi inaanza kuchanganyikiwa na kuendelea itakuwa vigumu
Siasa nayo ni taaluma?

Vv
 
Mkuu mimi siyo mpotoshaji na sifurahii dhuluma,soma post yangu kwa umakini usitawaliwe na hisia utanielewa.Na nimeelezea kutafuta suluhisho kwa kumtegemea Mungu ila kama utategemea elimu yako na akili zako huwezi kunielewa.
Kiongozi yeyote hawezi kutoka madarakani kama Mungu hajapanga atoke,mtapoteza muda sana.
Mara nyingi watu mnapokuwa na kitu hamjui kukithamini mpaka kiondoke kawaluliza Walibya kuhusu Gadaffi,wewe unayatazama mambo kwa macho haya ya nyama mimi natazama zaidi katika level ambazo huwezi kunielewa kwa vielimu vya duniani.
Kulaumu na kulalamika ni kati ya mambo yanayomchukiza Mungu,dont just complain do something.Kila kiongozi Mungu humweka kwa kipindi fulani na kwa sababu fulani na muda mwingine si lazima awe ni mzuri au apendwe na watu wote hayo ni maisha ya kufikilika sana.Huwezi kuwa kiongozi mzuri kama wewe mwenyewe hautii walio juu yako,sasa hao hata mkiwapa nchi trust me si kwamba watafanya wonders.Ipe support serikali iuliyopo ili taifa lifike pale ambapo linatakiwa kufika,ila hata usipotoa support Mungu atainua watu watakaosaidia hili taifa kufika anapotaka lifike.
Mimi sijakamaa mtu hasa hawa wanaojiita viongozi wa dini kukemea,swali langu kwao nimeuliza je Mungu amewaambia wakemee publically?Mtu akikosea unaweza mtafuta ukaongea naye si lazima kila mtu ajue.Mkuu makanisani sasa hivi pamevamiwa wewe huwezi kunielewa ,ila kuna siku utanielewa namaanisha nini.
Tena hao wanaojiita watumishi wa Mungu wanasahau maandiko yanasema "muenende kama kondoo katikati ya mbwa mwitu" tafakari hili andiko kama Mungu atakujalia kuelewa maana yake washirikishe na wao.Fuatilia mbwamwitu wakoje alafu jiulize huyu kondoo anakuwa anapataje ujasiri katikati ya mbwa mwitu,utaumizwa hapa pako crystal clear.
"Watu wangu wanaangamizwq kwa kusoma maarifa"
Nimeona kuwa wewe ni mtu usiyeelewa kitu jinsi ulivyoelezea mambo ya Libya. Hujui kitu kabisa.

Usisikilize habari za mitaani, fuatilia ukweli. Walibya waliteseka alipoondolewa Gadafi lakini hakuna mtu aliyejutia. Kuondoka kwa Gadafi kulileta shida iliyotegemewa kwa sababu madikteta huwa hawatengenezi mifumo ya kiutawala bali huwa wanahodhi kila kitu wao wenyewe. Hivyo wakiondolewa au wakifa ghafla ni lazima nchi itapata matatizo ya kugombania madaraka.

Kasome takwimu za Dunia. Libya kwa sasa ndiyo nchi inayoongoza kwa ukuaji wa uchumi Duniani. Kwa sasa uchumi wa Libya unakua kwa 10.9%.

Nenda pale Tripoli katamke hayo maneno ya kipuuzi, uone Walibya watakachokufanya. Kwa Walibya, Gadafi alikuwa ni laana ya Taifa. Pamoja na madhira waliyoyapata Walibya mara baada ya kuondolewa dikteta Gadafi, hakuna anayejutia.

Tuna watu wengi ni wajinga wa elimu ya Dunia lakini pia ni wajinga wa neno la Mungu. Na ujinga siyo utakatifu. Hawa hawatairithi nchi wala Mbingu.

Mungu kakutendea muujiza mkubwa wa kwanza, kukuumba tofauti na kingine chochote, akakupa utashi, akili na nguvu. Kwa nia moja kuwa uvitumie vitu hivyo kutenda kazi. Utumie akili, utashi na nguvu. Lakini kuna watu wa kawaida, wachungaji makanjanja na hata waumini wa kawaida wanaoamini kuwa maisha yao yatakwenda kwa miujiza. Mungu alikuwa wa kwanza kufanya kazi, na sisi tunatakiwa kuiga mfano wake. Mungu alimfurusha Lucifer baada ya kuona amekengeuka. Wananchi ambao ndiyo mamlaka iliyo kuu katika Taifa, wakiwa na uhakika kabisa kuwa utawala umekengeuka (siyo kwa hola au chuki), wana haki ya kuuondosha.

Tunatakiwa tuitafute na kuipigania haki iliyo ya kweli, na tufanyapo hivyo, tunamwomba Mungu atupe hekima ya kujua namna ya kuenenda. Na lile tulifanyalo katika kuitafuta haki iliyo ya kweli, Mungu wetu aweke baraka katika nia na jitihada hizo.

Mtume Paulo aliposhtakiwa na kuhukumiwa pale mahakama ya Wayahudi, alikata rufaa mahakama kuu ya Roma. Wangekuwa ni hawa walokole wanaofanya yafsiri potofu ya neno la Mungu, wangesema Paulo asikate rufaa bali kule mahabusu wakati anasubiri kunyongwa, aongeze maombi na kufunga.
 
Ni kufanya vizuri kwenye eneo lako la specializatio.

Mfano mleta mada Ni Askofu ambaye ukimwambia onyesha Makanisa yako hata matatu tu yalipo dar es salaam anaingia mitini na kutokomea gizani.Kwake hakujaendelea Hana matawi.

Kwa mkulima maendeleo ni kuongeza uzalishaji na kuongeza kipato kupitia kilimo.
Kesi ambayo iko mahakamani miaka 3 au 8 na mpaka leo mahabusu wanaambiwa upelelzi haujamalizika, huoni hapo kuna dosari, watu wakiandamana titapata madhara, nawe unasema watu wasilikemee na kulizungumza, kwa sababu sio fani yako.

Wewe huna ndugu ama rafiki anayesota mahabusu kwa dhuluma na kubambikizwa kesi, usonge payuka hivi.
 
Kila mtu kwa nafasi yake asimame na kukemea uovu. Tusidanganywe na wanasiasa wanaotawala kwamba wenye kukemea uovu ni wao ilhali wao ndo kwa kiasi kikubwa wanawafanyia uovu wale wasiokubaliana nao kwenye falsafa kadha wa kadha.
 
Jeshi la Polisi linamkamata mtu na kumuweka ndani na baada ya kelele nyingi kutoka kwa jamii, mtuhumiwa huandaliwa mashtaka.

Jamhuri inamtuhumu na kumshtaki kwa makosa mbalimbali mazito yasiyodhaminika. Baada ya mtuhumiwa kufikishwa mahakamani kesi hutajwa lakini kesi huahirishwa na mtuhumiwa anaambiwa hawezi kujibu lo lote kwa kuwa 'upelelezi unakuwa bado haujakamilika'!

Kila inapofikia tarehe ya kesi kutajwa, waendesha mashtaka wa Serikali huiambia Mahakama kuwa kesi bado haijakamilika na Hakimu au Jaji hulazimika kuiahirisha tena kesi hadi tarehe nyingine. Huo ndio unakuwa mwanzo wa mateso na kukomolewa kwa mtuhumiwa. Biashara zake na kazi zake huathiriwa vibaya sambamba na familia yake achilia mbali afya yake kuathiriwa akiwa mahabusu!

Inaonekana katika nchi yetu, sisi sote tunakosa ujasiri wa kuhoji ukiritimba huu wa Sheria zetu unaochochewa na watendaji wenye husuda na roho mbaya wanaotumia mwanya wa vipengere kandamizi vya Sheria zetu na hivyo kuwatesa na kuwakomoa wale wasiopatana nao ndani na nje ya mfumo wa Serikali.

Haki yoyote iliyocheleweshwa ni sawa na haki iliyokataliwa (justice delayed is justice denied). Hivyo, kuchelewesha kusikiliza kesi za waliotuhumiwa huku wakiachwa kusota mahabusu ni sawa na kuwacheleweshea na kuwanyima haki yao.

Kwanini umkamate mtu na kumtuhumu na kisha kumshtaki lakini unamuweka mahabusu miezi na hata miaka kwa kisingizio cha upelelezi kutokukamilika katika zama hizi?

Hivi ni kiongozi gani au mamlaka gani inayoweza kufidia hasara za mtuhumiwa aliyecheleweshewa haki hadi kuathirika na kupata magonjwa hadi kifo? Mambo haya yanaumiza sana moyo wangu kwani kwa njia hii watu wengine husigina haki za wengine.

Mambo haya hayatakiwi kufanyika katika nchi inayosadikika kuwa na idadi kubwa ya waumini wa dini zinazofundisha kuhusu haki na upendo ikiwemo dini ya Kikristo. Hasira ya Mungu iko dhahiri kwa mtu mmoja mmoja, jamii au taifa lo lote ambalo watawala na viongozi wake husigina haki za wengine (Amos 5:1-27).

Wiki hii ninawaombea wale wote ambao bado wako mahabusu wengine hata miaka kadhaa kwa sababu upelelezi wa kesi zao 'haujakamilika'.

Ninawaomba wahusika yaani washitaki na wale wote wanaohusika na uendeshaji pamoja na 'upelelezi' wa kesi hizo waingiwe na utu na roho ya huruma huku wakijua kuwa hata wao wenyewe ni wakosefu pia kwa namna moja au nyingine. Ninaomba watu wengine tuungane katika maombi haya lakini kikubwa zaidi tuungane katika kupaza sauti zetu kwa mamlaka husika.

Ninawaomba Mahakimu na Majaji katika Mahakama zetu hasa wale wanaosikiliza kesi za namna hiyo kuwa wakali kwa waendesha mashtaka na wapelelezi 'wanaoonekana kucheza mchezo wa kuchelewesha kesi'. Hakimu au Jaji ni mdau muhimu sana katika upatikanaji wa haki kwa wakati.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani
Kwa hili Askofu ametenda alilopaswa kutenda na ameutendea haki uaskofu wake na utumishi wake kwa Mungu. Neno la Mungu halirudi patupu. Hakuna aliye salama kwa hilo.
 
Baba askofu Mungu akupe nguvu & Ujasili zaidi..ila kumbuka kitufe ulichokibonyeza si rafiki usije ukapimwa mkojo au uraia wako kwamba Je wazazi wa wazazi wako walikuwa raia wa Tanzania ama laa.
 
Mkuu mimi siyo mpotoshaji na sifurahii dhuluma,soma post yangu kwa umakini usitawaliwe na hisia utanielewa.Na nimeelezea kutafuta suluhisho kwa kumtegemea Mungu ila kama utategemea elimu yako na akili zako huwezi kunielewa.
Kiongozi yeyote hawezi kutoka madarakani kama Mungu hajapanga atoke,mtapoteza muda sana.
Mara nyingi watu mnapokuwa na kitu hamjui kukithamini mpaka kiondoke kawaluliza Walibya kuhusu Gadaffi,wewe unayatazama mambo kwa macho haya ya nyama mimi natazama zaidi katika level ambazo huwezi kunielewa kwa vielimu vya duniani.
Kulaumu na kulalamika ni kati ya mambo yanayomchukiza Mungu,dont just complain do something.Kila kiongozi Mungu humweka kwa kipindi fulani na kwa sababu fulani na muda mwingine si lazima awe ni mzuri au apendwe na watu wote hayo ni maisha ya kufikilika sana.Huwezi kuwa kiongozi mzuri kama wewe mwenyewe hautii walio juu yako,sasa hao hata mkiwapa nchi trust me si kwamba watafanya wonders.Ipe support serikali iuliyopo ili taifa lifike pale ambapo linatakiwa kufika,ila hata usipotoa support Mungu atainua watu watakaosaidia hili taifa kufika anapotaka lifike.
Mimi sijakamaa mtu hasa hawa wanaojiita viongozi wa dini kukemea,swali langu kwao nimeuliza je Mungu amewaambia wakemee publically?Mtu akikosea unaweza mtafuta ukaongea naye si lazima kila mtu ajue.Mkuu makanisani sasa hivi pamevamiwa wewe huwezi kunielewa ,ila kuna siku utanielewa namaanisha nini.
Tena hao wanaojiita watumishi wa Mungu wanasahau maandiko yanasema "muenende kama kondoo katikati ya mbwa mwitu" tafakari hili andiko kama Mungu atakujalia kuelewa maana yake washirikishe na wao.Fuatilia mbwamwitu wakoje alafu jiulize huyu kondoo anakuwa anapataje ujasiri katikati ya mbwa mwitu,utaumizwa hapa pako crystal clear.
"Watu wangu wanaangamizwq kwa kusoma maarifa"
Huwezi kumtegemea Mungu (roho) kwa kukaa kimya ukafaulu. Tumtegemee Mungu kwa kufanya yatupasayo . Nchi za wenzetu wakizopiga hatua za dhati ktk kila jambo. Walipitia aina hii ya tawala zenye kutotii utaratibu na za ki dictator . Lakini ilifikia wakakubali kutomtukuza mtu, chama tawala, nk . Wakajiwekea utaratibu mzuri wa kuongozana kwa kuheshimu haki za binaadamu .
Sasa sisi huku bado unamkuta mtu kama DC , RC & WEO ana mamlaka ya kikoloni kabisa ya kumumweka mtu ndani bila sababu za msingi . Na hakuna wa kuwahoji !!. Na walipokemewa kidogo siku hizi wamepunguza. Lakini walikuwa wanamharibia mkuu taswira.

Serikali ni yetu bila kujali unaikubali au la . Lakini utaratibu wa kukamatana na kuwekana ndani kufuate sheria na haki za binaadamu. Bila kujali unamuunga kiongozi au una mpinga. Kwani zote zipo kisheria na kikatiba .

Umezungumzia Libya . Mimi bado nasema kosa lilikuwa la Ghadaffi, kung'ang'ania mamlaka yote ya nchi bila kuweka utaratibu mzuri wa kurithishana madaraka. Mbaya zaidi mwanaye (Saif Al Islam) akionekana mstari wa mbele kutaka kumrithi Baba. Unaongoza wanaadamu si kondoo.
 
MTU yeyote mpenda haki huitetea bila kujali eneo alilo kuwepo, kupinga dhulma na uonevu wa aina yoyote ni sifa kuu kwa kila mpenda haki ni sifa ya kiucha mungu, na yeyote anaye tetea dhulma na uonevu ni muovu kama alivyo muovu mkuu LUCIFER
Kazi ya kiongozi wa dini sio kuongelea maovu Ni kuongelea mambo ya Mungu
 
Tungekuwa tuna tawala zifuatazo Sheria zingewajibisha Watumishi wote wawawekao watu ndani bila kukamilisha ushahidi.Mahakimu na majaji wanakenua meno tu na nyumba za ibada hawakosi kumkufukuru Mungu huku wameshikilia haki za watu.Ingekuwa ukimshikilia MTU Miaka bila ushahidi wanakatwa mishahara yao kulipa fidia yasingetokea hayo.Lkn ni rahisi tu kuwekwa ndani ukomolewe ili maisha yako yaharibike kisha utolewe ukute familia ishasambaratika nje hayupo watoto hawana Ramani washapotea,Mali zishafilisika.Nchi nyingi kesi isiyo na dhamana ni mauaji tu na wako kwenye mpango wa kutaka kuwapatia dhamana pia.Huku utashikiriwa Miaka Kwa upotevu wa elf 20, huku ukitumia kulishwa Kwa kodi za wananchi wakati una Mali za thamani zaidi ya hicho ulichoshikiliwa.Hivi mahakimu na majaji kwan mnaenda kufanya nn kwenye nyumba za ibada?,Sheria sio msahaafu zisibadilike.
Barikiwa sana mkuu
 
Ili nchi iendelee inahitaji kila mtu abobee kwenye eneo lake mfano mkulima alime Sana, injinia afanye Kazi za uinjinia Sana, askofu afanye Kazi za Uaskofu Sana nk ukiona Askofu anavua kofia la Uaskofu kageukia fani ya Sheria au upelelezi ujue nchi inaanza kuchanganyikiwa na kuendelea itakuwa vigumu
Mjinga wa kiwango cha SGR
 
YEHODAYA nadhani muda wako wa kujifungua umewadia (incase wewe ni KE) kama ni me am sorry but utakuwa bashite au baba ubaya mzee wa komwe! Yaani una hoja mufilisi pengine kuliko katuni, nahisi unahitaji mental treatment vinginevyo mshahara wa wanalumumba utakuwa umeongezeka HAIWEZEKANI JITU ZIMA UKAWA NA AKILI MBOVU KIASI HIKI
 
Ili nchi iendelee inahitaji kila mtu abobee kwenye eneo lake mfano mkulima alime Sana, injinia afanye Kazi za uinjinia Sana, askofu afanye Kazi za Uaskofu Sana nk ukiona Askofu anavua kofia la Uaskofu kageukia fani ya Sheria au upelelezi ujue nchi inaanza kuchanganyikiwa na kuendelea itakuwa vigumu
Maaskofu na wachungaji wengi pamoja na injili wanazo taaluma zingine ikiwemo ya sheria , udaktari , ualimu nk
 
Mkuu correction; hunipingi mimi utakuwa unapingana na biblia.Hao mitume walikufa sababu ya siasa au sababu ya kuhubiri injili na kuwaasa watu waziache njia zao mbaya?Kama utawala ulikuwa na shida Mungu alituma wajumbe wake wakaongea na mfalme hapo sikatai,ambapo hutaki kunielewa nasema hawa wa leo ,Mungu amewatuma waongee public au ni akili zao wenyewe?Hivi unajua Mungu ni mstaarabu sana,huwa hamdhalilishi mtu kabla ya kumwonya mara nyingi.Unatakiwa ujue mtu mwenye mamlaka ni mtu wa aina gani na anauwezo gani otherwise utaumia.Nafasi anayokuwa nayo ndiyo inampa huo uwezo na siyo yeye,nafasi aliyopewa na nchi.
Jifunze hata kwa wadudu,huwezi mchezea malkia au mfalme wao ukabaki salama.


Hio ni tafsiri yako,hakuna,mtumishi aliyeuwawa na watu Wa kawaida waliuliwa na watawala
Mkuu correction; hunipingi mimi utakuwa unapingana na biblia.Hao mitume walikufa sababu ya siasa au sababu ya kuhubiri injili na kuwaasa watu waziache njia zao mbaya?Kama utawala ulikuwa na shida Mungu alituma wajumbe wake wakaongea na mfalme hapo sikatai,ambapo hutaki kunielewa nasema hawa wa leo ,Mungu amewatuma waongee public au ni akili zao wenyewe?Hivi unajua Mungu ni mstaarabu sana,huwa hamdhalilishi mtu kabla ya kumwonya mara nyingi.Unatakiwa ujue mtu mwenye mamlaka ni mtu wa aina gani na anauwezo gani otherwise utaumia.Nafasi anayokuwa nayo ndiyo inampa huo uwezo na siyo yeye,nafasi aliyopewa na nchi.
Jifunze hata kwa wadudu,huwezi mchezea malkia au mfalme wao ukabaki salama.
Ni tafsiri yako siasa ni Maisha ya kila siku hao watumishi waliuliwa na watawala waliochomwa na maneno ya watumishi juu tawala zao dhalimu. Ukimuona,mtumishi Wa Mungu anafungamana na tawala zisizomuheshimu Mungu,huyo ni mtumishi Wa shetani na mchungaji Wa mshahara.Kazi ya mtumishi Wa Mungu ni kukemea maovu sio kukaa kimya akikaa kimya atimizi kazi yake
 
Ili nchi iendelee inahitaji kila mtu abobee kwenye eneo lake mfano mkulima alime Sana, injinia afanye Kazi za uinjinia Sana, askofu afanye Kazi za Uaskofu Sana nk ukiona Askofu anavua kofia la Uaskofu kageukia fani ya Sheria au upelelezi ujue nchi inaanza kuchanganyikiwa na kuendelea itakuwa vigumu
ungesoma tu hoja ukapita bila kuandika chochote umesababisha niandike.....baba yako au kaka hapo kwenu hata anapotoa wazo/tendo baya wewe huwa unakaa kimya kusubiri ukue ndo uje kumkosoa etii33h......
 
Back
Top Bottom