Askofu Mwamakula: Ole kwa Taifa lisilotenda HAKI kwa watu wake! Unamkamata mtu eti upelelezi haujakamilika karne hii?

Askofu Mwamakula: Ole kwa Taifa lisilotenda HAKI kwa watu wake! Unamkamata mtu eti upelelezi haujakamilika karne hii?

We utakuwa ni mgonjwa wa akili, hivi kuna maaskofu wa Mungu na Yesu.
Yesu alitamka wazi kabisa utawala wangu SI wa dunia hii.Ukiona Askofu anajihusisha na mambo ya utawala wa dunia hii huyo SI Askofu wa Yesu
 
In the same way God warned Israel of their stubborn decision to be led by a human king instead of the King of kings (see 1 Samuel 8), God uses bad leaders to teach His people to pursue righteousness and stand up for it.
When people elect or unite to put up a leader who is wicked, they are the ones who actually suffer the consequences of having bad leadership.

God uses this cause-and-effect scenario to teach us to choose the kind of leaders that He wants – those who are just, honest, righteous, and with integrity.
 
Mkuu muda mwingine mnakosea kwa taarifa yako si kila kiongozi wa dini anayekemea ni wa kweli wengine wana agenda zao za siri.Kiongozi wa dini anayemjua Mungu vizuri huongozwa na Roho Mtakatifu na si kwa matukio na hisia zake mwenyewe.Kwa hiyo viongozi wengine wanaweza wasifanye hivyo unavyotaka wewe wawafanye kwani Mungu hajawaambia wafanye.Ushauri wangu kwako ,hao wanaofanya kawaulize ni Mungu amewaagiza mfanya hayo au ni akili zenu na matukio?
Mnalaumu viongozi wa dini wamekaa kimya,je kama wako wanaombea hayo mambo na hawapendi publicity?Kuna viongozi wa dininawaangalia wanatumia vibaya idadi za memebers walio nao wakizani ni wao kumbe ni wa Mungu.Kwa imani yetu sisi wakristo kila mamlaka inatoka kwa Mungu,kwa hiyo kama kuna tatizo lolote juu ya mamlka husika tunaenda kwa aliyeiweka ambaye ni Mungu.Pia waulize wanapokemea publically ni Mungu anakuwa amewaambia wakemee publically au ni akili zao?Kama Mungu anataka ufikishe ujumbe kwa kiongozi yeyote atakuwekea mazingira ya kiongozi yule kukutana na wewe au ukiomba kuonana naye hakataliwa.
Kuna mtu anaweza akawa anajiita au anaitwa mtumishi wa Mungu duniani lakini Mungu hamtambui,kiongozi yeyote wa dini ya kikristo akianza maneno maneno na serikali ambayo kwa mujibu wa biblia kila mamlaka inatoka kwa Mungu inabidi uwe naye makini.Wakristo hawafundishwi kujipigania wanafundishwa kumtegemea Mungu awapigania muda mwingine Mungu anaweza kuwapigania kwa namna kusiko kwa kibinadamu.Biblia katika kitabu cha efeso inasema vita vyetu si juu ya damu na nyama.Lakini pia inashangaza ukiona mkristo anapigana vita vya kimwili,hapa nielezeee yamkini kuna watu hawajaelewa,siku moja Mungu alituambia tunapigana vita kimwili kwa sababu tulikuwa tunamwangalia mwenye tatizo.
Kama kiongozi anashida,unachotakiwa kujua ipo roho nyuma ya hiyo shida au tabia au chochote anachofanya,unachotakiwa siyo kupigana na huyo kiongozi au kumsema vibaya bali upambane na roho inayosababisha hayo matatizo na siyo mtu anayetenda.
Kuna watu hamjanielewa,kama unaona haki haipo Tanzania,usipambane na mahakimu na watawala bali pambana na Roho zinazowafanya mahakimu,polisi na watawala wafanye hayo wanayofanya.Ukilijua hili huwezi kumpoint mtu,anyway yamkini hii elimu ni ya level ya juu kuliko uelewa wa wengi.Si lazima unielewe leo unaweza nielewa baada ya wiki,mwezi au miaka.
Ushauri kwa wakristo(naongelea wakristo kwa sababu imani zingine wanautaratibu wao na njia zao) kama kuna tatizo lolote katika nchi wakumkimbilia ni Mungu.haijalishi watu watasema mmekuwa "brain washed" care not.Ukianza kutumia akili zako,Mungu huwa anakuacha upambane mwenyewe.
Kuweni makini sana na wanaojiita watumishi wa Mungu wakiyatumia maandiko kwa interest zao,unapoamua kutumia njia zako maana yake Mungu ameshindwa.Wewe kama ni mtumishi wa Mungu kweli always jiulize swali hili,hicho unachofanya Mungu amekuambia ukifanye?
Wito:kama kuna mtu hujampokea Yesu,saa nma wakati wa wokovu ni sasa,kuna mambo mengi siwezi kuyaandika hapa lakini niseme tu,muda uliopoteza klwenye maisha yakumchukiza Mungu unatosha .Amua leo umpokee Yesu afanyike kuwa Bwana na mwokozi wako,dini bila Yesu haina msaada kwako.

Nikupinge si kweli kila mamlaka utoka Kwa Mungu zitokazo Kwa Mungu utenda ya kumpendeza Mungu.Kwann Africa ndo tunapata mamlaka mbovu heri ya hata wakoloni je Mungu atupendi?Ukisoma biblia Watumishi Wangu karibu wote hawakukaa kimya kusimama na uovu hata ikapelekea wengi kuuwawa soma historia za vifo vya mitume wa Yesu na wengine. Tawala zitokazo Kwa Mungu umeheshimu Mungu.
 
Kuna wakati Mungu huruhusu kutokea kwa tawala mbaya ili watu wafanye kitu.
 
Thanks so much, asante sana baba askofu, mungu wa abraham, isaac and jacob akupe maisha marefu na afya jema na akuongeze usujaa wa kuwatetea wanyonge,Mimi naona hii ni ukatili na uyama unayofanywa na hii serikali ya awamu ya 5, huwezi fikisha mtu mahakamani kaa hujakamilisha uchunguzi, maana ndio umusitaki mtu unafanya huo uamuzo kulingana na ile ushahindi ambao uko nae na ambao tayari umeukusaya, cha ajabu unafikisha mtu kortini huna ushahindi sababu huna uchunguzi kamili kisha unaomba korti iahirishe hii kesi mara kadhaa, wakati wingine miaka, kaa ile kesi ya mashee, katika mataifa ambayo inaheshimu haki na binadamu , mtu hufikiswa kortimni pale ushahidi upo , yaani uchunguzi umekamilika, sasa ona vile huyu ndugu yetu kabedera anavyoteseka na kila mara akiletwa kortini uchunguzi unasemekana bado haujakamilika, JE HII NI HAKI KWELI???? asante tena baba askofu kwa kuliongea hili, asante kwa kuwa tofauti na "MAASKOFU NA WACHUNGAJI NA MITUME WENGINE" ambao kazi yao siku hizi imekuwa ni kupigia ccm magoti na kuisifu bila kuona ile maovu inatendwa na ccm. Kweli siku ya mwisho yesu atasema, ONDOKENI KWANGU SIWAJUI HATA KIDOGO, barikiwa sana baba askofu, na kweli MWANA KONDOO AMESHINDA KIFO NA MAUTI

Tungekuwa tuna tawala zifuatazo Sheria zingewajibisha Watumishi wote wawawekao watu ndani bila kukamilisha ushahidi.Mahakimu na majaji wanakenua meno tu na nyumba za ibada hawakosi kumkufukuru Mungu huku wameshikilia haki za watu.Ingekuwa ukimshikilia MTU Miaka bila ushahidi wanakatwa mishahara yao kulipa fidia yasingetokea hayo.Lkn ni rahisi tu kuwekwa ndani ukomolewe ili maisha yako yaharibike kisha utolewe ukute familia ishasambaratika nje hayupo watoto hawana Ramani washapotea,Mali zishafilisika.Nchi nyingi kesi isiyo na dhamana ni mauaji tu na wako kwenye mpango wa kutaka kuwapatia dhamana pia.Huku utashikiriwa Miaka Kwa upotevu wa elf 20, huku ukitumia kulishwa Kwa kodi za wananchi wakati una Mali za thamani zaidi ya hicho ulichoshikiliwa.Hivi mahakimu na majaji kwan mnaenda kufanya nn kwenye nyumba za ibada?,Sheria sio msahaafu zisibadilike.
 
...Huo ndio unakuwa mwanzo wa mateso na kukomolewa kwa mtuhumiwa. Biashara zake na kazi zake huathiriwa vibaya sambamba na familia yake achilia mbali afya yake kuathiriwa akiwa mahabusu!
Hili ndilo dhumuni na lengo kuu la wanaoagiza mtu akamatwe. Tesa mpaka mtu adondoshe tone la mwisho la mate, damu na jasho.
 
Ni kufanya vizuri kwenye eneo lako la specializatio.

Mfano mleta mada Ni Askofu ambaye ukimwambia onyesha Makanisa yako hata matatu tu yalipo dar es salaam anaingia mitini na kutokomea gizani.Kwake hakujaendelea Hana matawi.

Kwa mkulima maendeleo ni kuongeza uzalishaji na kuongeza kipato kupitia kilimo.
Kwanza nimpongeze sana askofu kwa mafunuo haya ambayo ametushirikisha humu ndani.Haya ni mafunuo yake na ana uhuru na haki ya kutushirikisha au kutokushirikisha.

Askofu amependa kutushirikisha na mimi ninampongeza kwa sababu kwa asilimia 99 aliyoyasema ni ya kweli tena tupu na hakukurupuka amefanya utafiti wa kutosha.

Nakushangaa sana wewe unayezungumza habari ya idadi ya makanisa,ina uhusiano gani na hoja iliyopo mezani.(Nimetambua kuwa hujui hata maana ya kanisa).Huelewi hata mada muhimu sana anayoizungumzia askofu ya kupatikana haki kutoka kwenye vyombo husika vinavyotakiwa kutetea haki ya mtanzania ikiwa ni mahakama na jeshi la polisi.

Inavyoelekea na ilivyo kwa sasa sio rahisi sana kwa mtu mmoja mmoja kukemea hali hii labda awe mzalendo na asiyejali lolote litakalotokea baada ya kutoa hoja kama hii.
Askofu na viongozi wengine wa dini zote,nasema dini zote sio makanisa yote,(nimesema dini zote ili huyu anayedai idadi ya makanisa aelewe)

Viongozi hawa wa dini ndio sasa wenye nguvu ya kulinda nchi kwa kuongoza maombi kwa waumini wao ili hali hii isiendelee na kukemea maovu mbalimbali yanayofanywa na baadhi ya vyombo vinavyolinda haki ya raia katika nchi kama alivyosema askofu na pale viongozi hawa wanapokaa kimya na wengine kujifanya hawaoni,ndio hapo hata waumini wao wanawaona kuwa wapo pamoja na vyombo hivyo.

Haki inapokosekana kwa kubinywa na vyombo fulani na viongozi wa dini kukaa kimya hiyo nchi inaelekea ICU kwa sababu HAKI HUINUA TAIFA BALI DHAMBI NI AIBU KWA WATU WOTE.
 
Baba Askofu Emmaus Bandekile umeongea yale yaliopaswa kuongelewa na viongozi wooote wapenda haki.
Lakini kwa umbumbumbu wa baadhi ya watanzania hawajakuelewa na ndio maana wengine wanakejeli.
Hakuna faida yoyote kuwa na maendeleo kwa jamii ambapo "haki"ya ubinadamu inauzwa.
Wachache wanajifanya kuwa "miungu"watu wanatamaini hata wakifa mwenyezi mungu akawape nafasi ya kuwaongoza malaikaka watakatifu wa mbinguni(Rais JPM) kama sio ushetani ni nini?

Rais wa nchi anamkufuru Mwenyezi Mungu hatharani.....hakika mungu hadhihakiwi!
 
Ili nchi iendelee inahitaji kila mtu abobee kwenye eneo lake mfano mkulima alime Sana, injinia afanye Kazi za uinjinia Sana, askofu afanye Kazi za Uaskofu Sana nk ukiona Askofu anavua kofia la Uaskofu kageukia fani ya Sheria au upelelezi ujue nchi inaanza kuchanganyikiwa na kuendelea itakuwa vigumu
Kalye empali
 
Mkuu muda mwingine mnakosea kwa taarifa yako si kila kiongozi wa dini anayekemea ni wa kweli wengine wana agenda zao za siri.Kiongozi wa dini anayemjua Mungu vizuri huongozwa na Roho Mtakatifu na si kwa matukio na hisia zake mwenyewe.Kwa hiyo viongozi wengine wanaweza wasifanye hivyo unavyotaka wewe wawafanye kwani Mungu hajawaambia wafanye.Ushauri wangu kwako ,hao wanaofanya kawaulize ni Mungu amewaagiza mfanya hayo au ni akili zenu na matukio?
Mnalaumu viongozi wa dini wamekaa kimya,je kama wako wanaombea hayo mambo na hawapendi publicity?Kuna viongozi wa dininawaangalia wanatumia vibaya idadi za memebers walio nao wakizani ni wao kumbe ni wa Mungu.Kwa imani yetu sisi wakristo kila mamlaka inatoka kwa Mungu,kwa hiyo kama kuna tatizo lolote juu ya mamlka husika tunaenda kwa aliyeiweka ambaye ni Mungu.Pia waulize wanapokemea publically ni Mungu anakuwa amewaambia wakemee publically au ni akili zao?Kama Mungu anataka ufikishe ujumbe kwa kiongozi yeyote atakuwekea mazingira ya kiongozi yule kukutana na wewe au ukiomba kuonana naye hakataliwa.
Kuna mtu anaweza akawa anajiita au anaitwa mtumishi wa Mungu duniani lakini Mungu hamtambui,kiongozi yeyote wa dini ya kikristo akianza maneno maneno na serikali ambayo kwa mujibu wa biblia kila mamlaka inatoka kwa Mungu inabidi uwe naye makini.Wakristo hawafundishwi kujipigania wanafundishwa kumtegemea Mungu awapigania muda mwingine Mungu anaweza kuwapigania kwa namna kusiko kwa kibinadamu.Biblia katika kitabu cha efeso inasema vita vyetu si juu ya damu na nyama.Lakini pia inashangaza ukiona mkristo anapigana vita vya kimwili,hapa nielezeee yamkini kuna watu hawajaelewa,siku moja Mungu alituambia tunapigana vita kimwili kwa sababu tulikuwa tunamwangalia mwenye tatizo.
Kama kiongozi anashida,unachotakiwa kujua ipo roho nyuma ya hiyo shida au tabia au chochote anachofanya,unachotakiwa siyo kupigana na huyo kiongozi au kumsema vibaya bali upambane na roho inayosababisha hayo matatizo na siyo mtu anayetenda.
Kuna watu hamjanielewa,kama unaona haki haipo Tanzania,usipambane na mahakimu na watawala bali pambana na Roho zinazowafanya mahakimu,polisi na watawala wafanye hayo wanayofanya.Ukilijua hili huwezi kumpoint mtu,anyway yamkini hii elimu ni ya level ya juu kuliko uelewa wa wengi.Si lazima unielewe leo unaweza nielewa baada ya wiki,mwezi au miaka.
Ushauri kwa wakristo(naongelea wakristo kwa sababu imani zingine wanautaratibu wao na njia zao) kama kuna tatizo lolote katika nchi wakumkimbilia ni Mungu.haijalishi watu watasema mmekuwa "brain washed" care not.Ukianza kutumia akili zako,Mungu huwa anakuacha upambane mwenyewe.
Kuweni makini sana na wanaojiita watumishi wa Mungu wakiyatumia maandiko kwa interest zao,unapoamua kutumia njia zako maana yake Mungu ameshindwa.Wewe kama ni mtumishi wa Mungu kweli always jiulize swali hili,hicho unachofanya Mungu amekuambia ukifanye?
Wito:kama kuna mtu hujampokea Yesu,saa nma wakati wa wokovu ni sasa,kuna mambo mengi siwezi kuyaandika hapa lakini niseme tu,muda uliopoteza klwenye maisha yakumchukiza Mungu unatosha .Amua leo umpokee Yesu afanyike kuwa Bwana na mwokozi wako,dini bila Yesu haina msaada kwako.
Wewe ni mpotoshaji na ni miongoni mwa wanaofurahia dhulma dhidi ya wananchi . Viongozi wetu hasa wa ki Africa. Ni watu wababe, watemi wanaotumia udhaifu wa taasisi zetu za kisheria na za kimaamuzi kukandamiza watu wa itikadi tofauti na Imani tofauti na hata kabila tofauti.

Bila shaka umeona wabunge wote wa upinzani wa majimbo si viti maalum, wakiwa na kesi za uchochezi na wengine wakiwa wamewekwa jela kwa kuwafurahisha tu watawala. Hali kama hii isipokemewa kwa kusubiri roho wa Mungu afanye kazi. Ni kuisaliti nchi na wananchi wenyewe. Roho wa Mungu afanye kazi, lakini wanaadamu (viongozi) nao wakemewe. Kwa sababu taasisi zetu siyo imara kama za wenzetu dhidi ya viongozi wetu.
 
Yesu alitamka wazi kabisa utawala wangu SI wa dunia hii.Ukiona Askofu anajihusisha na mambo ya utawala wa dunia hii huyo SI Askofu wa Yesu
Katika mada hii umeonyesha pasipo shaka kuwa unayo andika sio mawazo yako bali unaitumikia ajira (ni njaa tuu-kwa sauti ya Makonda).
Mimi sidhani kama jambo hili ni la kuletea ushabiki wa kisiasa kwa vile serikali ni ya CCM.
Matendo haya ya ofisi ya DPP, Jeshi la polisi,Takukuru nk. ni matendo ya ofisi za serikali na hata kesho CCM ikianguka na chama kingine kuchukua madaraka bado watendaji hao watafanya matendo hayohayo kama wote hatuyapingi sasa.
Jee wewe unakubaliana na mienendo hii ya kumkamata mtu unamfungulia mashtaka yasiyo dhaminiwa ili tuu asote ndani? Jaribu kuchukulia mfano wa ndugu yako ndio amefanyiwa hivyo?
Jana Kisutu umeona, Aveva na Kaburu wamefutiwa makosa ya kutakatisha fedha kwani hawana kesi ya kujibu ila yale mengine watajibu.
Mtu unamuweka ndani miaka miwili kwa shtaka unalojua kuwa halipo umebambika tuu ili asote tuu?
Hili kama nchi inanufaikaje? Askofu yuko sahihi kulisemea
 
Kwann iwe Africa Miaka yote
Kiimani, Mungu huweza kuruhusu jambo hata baya likupate kama adhabu. Ili ukiwa katika hiyo adhabu, ujutie na kumrudia.

Lakini pia, kuna wakati Mungu huruhusu tawala mbaya ili magumu yatakayowapata, yawafanye muungane na kutengeneza mfumo mpya kabisa utakaowafaa watu wote.

Afrika kuna mambo ya ajabu sana. Watu wakati wa uchaguzi wanahongwa kwa namna ya ajabu tena kwa vitu vya kipuuzi kama kanga, chumvi, sh 5,000, ubwabwa, ngono, n.k. Wagombea na wapambe wao huishia kwa waganga wa kienyeji kwenda kuroga na kutambikiwa, wengine hutengeneza makundi ya kuvamia, kutesa na hata kuua wapinzani wao. Wapambe wao hushangilia maovu yanapotendeka ndidi ya wapinzani wao.

Hivi kiongozi anayepatikana kwa njia hizo dhalimu, na huku mamilioni ya watu wakifurahia rushwa, na dhulma dhidi ya wenzao, atakuwa na baraka gani? Ataleta baraka gani kwa wale waovu waliokuwa wakiunga mkono maovu ya mchakato wa kuchaguliwa kwake? Wote mtaadhibiwa kwa kupitia mtawala aliyepatikana kwa njia ovu.

Usishangae kuwa mbona haya yanatokea zaidi Afrika. Ni sharti yatokee zaidi huku maana huku ndiko ambako thamani ya utu wa mwanadamu imenajisiwa na wananchi wenyewe na watawala wao.
 
Wewe ni mpotoshaji na ni miongoni mwa wanaofurahia dhulma dhidi ya wananchi . Viongozi wetu hasa wa ki Africa. Ni watu wababe, watemi wanaotumia udhaifu wa taasisi zetu za kisheria na za kimaamuzi kukandamiza watu wa itikadi tofauti na Imani tofauti na hata kabila tofauti.

Bila shaka umeona wabunge wote wa upinzani wa majimbo si viti maalum, wakiwa na kesi za uchochezi na wengine wakiwa wamewekwa jela kwa kuwafurahisha tu watawala. Hali kama hii isipokemewa kwa kusubiri roho wa Mungu afanye kazi. Ni kuisaliti nchi na wananchi wenyewe. Roho wa Mungu afanye kazi, lakini wanaadamu (viongozi) nao wakemewe. Kwa sababu taasisi zetu siyo imara kama za wenzetu dhidi ya viongozi wetu.
Mkuu mimi siyo mpotoshaji na sifurahii dhuluma,soma post yangu kwa umakini usitawaliwe na hisia utanielewa.Na nimeelezea kutafuta suluhisho kwa kumtegemea Mungu ila kama utategemea elimu yako na akili zako huwezi kunielewa.
Kiongozi yeyote hawezi kutoka madarakani kama Mungu hajapanga atoke,mtapoteza muda sana.
Mara nyingi watu mnapokuwa na kitu hamjui kukithamini mpaka kiondoke kawaluliza Walibya kuhusu Gadaffi,wewe unayatazama mambo kwa macho haya ya nyama mimi natazama zaidi katika level ambazo huwezi kunielewa kwa vielimu vya duniani.
Kulaumu na kulalamika ni kati ya mambo yanayomchukiza Mungu,dont just complain do something.Kila kiongozi Mungu humweka kwa kipindi fulani na kwa sababu fulani na muda mwingine si lazima awe ni mzuri au apendwe na watu wote hayo ni maisha ya kufikilika sana.Huwezi kuwa kiongozi mzuri kama wewe mwenyewe hautii walio juu yako,sasa hao hata mkiwapa nchi trust me si kwamba watafanya wonders.Ipe support serikali iuliyopo ili taifa lifike pale ambapo linatakiwa kufika,ila hata usipotoa support Mungu atainua watu watakaosaidia hili taifa kufika anapotaka lifike.
Mimi sijakamaa mtu hasa hawa wanaojiita viongozi wa dini kukemea,swali langu kwao nimeuliza je Mungu amewaambia wakemee publically?Mtu akikosea unaweza mtafuta ukaongea naye si lazima kila mtu ajue.Mkuu makanisani sasa hivi pamevamiwa wewe huwezi kunielewa ,ila kuna siku utanielewa namaanisha nini.
Tena hao wanaojiita watumishi wa Mungu wanasahau maandiko yanasema "muenende kama kondoo katikati ya mbwa mwitu" tafakari hili andiko kama Mungu atakujalia kuelewa maana yake washirikishe na wao.Fuatilia mbwamwitu wakoje alafu jiulize huyu kondoo anakuwa anapataje ujasiri katikati ya mbwa mwitu,utaumizwa hapa pako crystal clear.
"Watu wangu wanaangamizwq kwa kusoma maarifa"
 
Kwani huyo Mungu mambo yake ni yepi.Pumbaaavu,kumbe tunawendawazimu kama nyie wasioisha kwenye hii nchi.Hopeless.
Kazi ya kiongozi wa dini sio kuongelea maovu Ni kuongelea mambo ya Mungu
 
Back
Top Bottom