Askofu Mwamakula: Ole kwa Taifa lisilotenda HAKI kwa watu wake! Unamkamata mtu eti upelelezi haujakamilika karne hii?

Askofu Mwamakula: Ole kwa Taifa lisilotenda HAKI kwa watu wake! Unamkamata mtu eti upelelezi haujakamilika karne hii?

Yesu alitamka wazi kabisa utawala wangu SI wa dunia hii.Ukiona Askofu anajihusisha na mambo ya utawala wa dunia hii huyo SI Askofu wa Yesu
Umesahau kwamba mnapotetea uovu wa viongozi mnasema mamlaka yote hutoka juu?Pia tambua vitu vyote vilivyopo ni Mali ya Bwana,Unamfahamu Bwana Mwenyewe anaye miliki vitu vyote? Unawafahamu Wasaidizi wake wa hapa Duniani?
 
Unakuta Askofu Koko Kama yeye haheshimu kazi za watu halafu anataka Yake iheshimiwe.Isipoheshimiwa anashangaa
Lakini dhamiri yako inasemaje? Mbona umejawa na hasira sana juu ya Neno la Askofu,unaweza kuonyesha ubaya wake au uwongo wowote katika Andiko hilo?Je,Rais alipoongea na wafungwa hakugusia hilo? Muda Fulani tuzifanye dhamiri zetu kuwa Hai.
 
Ili nchi iendelee inahitaji kila mtu abobee kwenye eneo lake mfano mkulima alime Sana, injinia afanye Kazi za uinjinia Sana, askofu afanye Kazi za Uaskofu Sana nk ukiona Askofu anavua kofia la Uaskofu kageukia fani ya Sheria au upelelezi ujue nchi inaanza kuchanganyikiwa na kuendelea itakuwa vigumu
Na wazulumaji wa haki za watu wengine wazulumu sana,sasa kelele za usaliti mnazotupigia kupitia kiongozi wenu wa uzulumaji pale wazulumiwa wanapojitetea na wasizulumiwe zinatoka wapi wakati huo ndo mtindo wa maisha mliokubaliana huku ccm awamu hii!
 
Ili nchi iendelee inahitaji kila mtu abobee kwenye eneo lake mfano mkulima alime Sana, injinia afanye Kazi za uinjinia Sana, askofu afanye Kazi za Uaskofu Sana nk ukiona Askofu anavua kofia la Uaskofu kageukia fani ya Sheria au upelelezi ujue nchi inaanza kuchanganyikiwa na kuendelea itakuwa vigumu
Kwa akili yako mchungaji mama Lwakatare hahusiki kwa sababu ni mwanaccm! Huyu mama huacha vikao vya bunge na kuenda kuhubiri kanisani kwake, hilo haulioni!
 
Sauti za Yale yanayokukera mpelekee diwani au mbunge wako apeleke mbele .Kila mtu akipaza sauti mabarabarani hatutasikilizana
Sasa zile swaga mnazotufanyia kwamba rais,au waziri au mkuu wa mkoa au mkuu wa wilaya kufanya ziara kusikiliza kero za wadanganyika huwa ni za nini wakati kila kata ina diwani na kila jimbo lina mbunge,any way acha niishie hapa nisije kuwa ninachat na robot
 
Ili nchi iendelee inahitaji kila mtu abobee kwenye eneo lake mfano mkulima alime Sana, injinia afanye Kazi za uinjinia Sana, askofu afanye Kazi za Uaskofu Sana nk ukiona Askofu anavua kofia la Uaskofu kageukia fani ya Sheria au upelelezi ujue nchi inaanza kuchanganyikiwa na kuendelea itakuwa vigumu
Mkiwa kanisani mnawapigia magoti na kubusu pete zao lakini mkiwa nyuma ya keyboard mnawasema vibaya. Wanafiki wakubwa sana nyie.
 
Jeshi la Polisi linamkamata mtu na kumuweka ndani mtuhumiwa huandaliwa mashtaka.

Jamhuri inamtuhumu na kumshtaki kwa makosa mbalimbali mazito yasiyodhaminika. Baada ya mtuhumiwa kufikishwa mahakamani kesi hutajwa lakini kesi huahirishwa na mtuhumiwa anaambiwa hawezi kujibu lo lote kwa kuwa 'upelelezi unakuwa bado haujakamilika'!

Kila inapofikia tarehe ya kesi kutajwa, waendesha mashtaka wa Serikali huiambia Mahakama kuwa kesi bado haijakamilika na Hakimu au Jaji hulazimika kuiahirisha tena kesi hadi tarehe nyingine. Huo ndio unakuwa mwanzo wa mateso na kukomolewa kwa mtuhumiwa. Biashara zake na kazi zake huathiriwa vibaya sambamba na familia yake achilia mbali afya yake kuathiriwa akiwa mahabusu!

Haki yoyote iliyocheleweshwa ni sawa na haki iliyokataliwa (justice delayed is justice denied). Hivyo, kuchelewesha kusikiliza kesi za waliotuhumiwa huku wakiachwa kusota mahabusu ni sawa na kuwacheleweshea na kuwanyima haki yao.

Kwanini umkamate mtu na kumtuhumu na kisha kumshtaki lakini unamuweka mahabusu miezi na hata miaka kwa kisingizio cha upelelezi kutokukamilika katika zama hizi?

Hivi ni kiongozi gani au mamlaka gani inayoweza kufidia hasara za mtuhumiwa aliyecheleweshewa haki hadi kuathirika na kupata magonjwa hadi kifo? Mambo haya yanaumiza sana moyo wangu kwani kwa njia hii watu wengine husigina haki za wengine.

Mambo haya hayatakiwi kufanyika katika nchi inayosadikika kuwa na idadi kubwa ya waumini wa dini zinazofundisha kuhusu haki na upendo ikiwemo dini ya Kikristo. Hasira ya Mungu iko dhahiri kwa mtu mmoja mmoja, jamii au taifa lo lote ambalo watawala na viongozi wake husigina haki za wengine (Amos 5:1-27).

Wiki hii ninawaombea wale wote ambao bado wako mahabusu wengine hata miaka kadhaa kwa sababu upelelezi wa kesi zao 'haujakamilika'.

Ninawaomba wahusika yaani washitaki na wale wote wanaohusika na uendeshaji pamoja na 'upelelezi' wa kesi hizo waingiwe na utu na roho ya huruma huku wakijua kuwa hata wao wenyewe ni wakosefu pia kwa namna moja au nyingine. Ninaomba watu wengine tuungane katika maombi haya lakini kikubwa zaidi tuungane katika kupaza sauti zetu kwa mamlaka husika.

Ninawaomba Mahakimu na Majaji katika Mahakama zetu hasa wale wanaosikiliza kesi za namna hiyo kuwa wakali kwa waendesha mashtaka na wapelelezi 'wanaoonekana kucheza mchezo wa kuchelewesha kesi'. Hakimu au Jaji ni mdau muhimu sana katika upatikanaji wa haki kwa wakati.

Nimeguswa na maneno haya ya
Askofu Mkuu, Baba Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula.

Natamani maneno haya yamguse jamaa yangu fulani, it might make a difference.
Mungu Mbariki sana Baba Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula.

Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali.
 
Ni kufanya vizuri kwenye eneo lako la specializatio.

Mfano mleta mada Ni Askofu ambaye ukimwambia onyesha Makanisa yako hata matatu tu yalipo dar es salaam anaingia mitini na kutokomea gizani.Kwake hakujaendelea Hana matawi.

Kwa mkulima maendeleo ni kuongeza uzalishaji na kuongeza kipato kupitia kilimo.
Nawe ni great thinker?
 
... tungekuwa na mahakama imara na huru; tungekuwa na majaji imara na huru, alichokielezea Baba Askofu kwa hakika hakikutakiwa kuwepo! Ilikuwa ni jukumu la mahakama kufutilia mbali sheria kandamizi zinazonyima haki za msingi za binadamu kama hii ya kuwekwa mahabusu kusubiri "upelelezi" usiojulikana utaisha lini!

Funny enough, baada ya miaka (apendavyo DPP) anaweza kufuta kesi kwa madai mepesi tu "hana tena nia ya kuendelea nayo"! Halafu hapo hapo nje ya viunga vya mahakama mtuhumiwa anakamatwa na kufunguliwa kesi mpya then upelelezi "usiojulikana" utaisha lini unaanza tena huku mtuhumiwa akiwekwa tena mahabusu! Hapana, this is not fair kwa vigezo vyovyote vile!

Sheria yoyote inayokinzana na Katiba na kanuni za msingi ikiwemo HAKI ZA BINADAMU it's void and null! Wala mahakama haikutakiwa kusita kufutilia mbali sheria za mamna hiyo! Na ni kwa jinsi hii ndipo inapokuja dhana ya Mahakama Kutunga Sheria badala ya Bunge pekee! Bahati mbaya ndio hivyo tena mamlaka hazijitambui wajibu wao.
 
Ninavyojua mtuhumiwa akikaa je anaweza kuvuruga ushahidi....ndiyo maana huwa wakati mwingine huwa wanawekwa ndani...Pia wakati mwingine uwekwa ndani kwa usalama wao. Tuheshimu kazi za wenzetu jamani.
Unakuta Askofu Koko Kama yeye haheshimu kazi za watu halafu anataka Yake iheshimiwe.Isipoheshimiwa anashangaa
Maaskofu namna hii ni hatari kwa ustawi wa nchi!
Inavyoonekana wafuasi wote wa Jiwe. Linapozungumzwa neno HAKI mnapata allergy. Shida ni nini ?! Hamuwezi kutawala/kuongoza bila kukandamiza haki za wananchi ?!. Uongozi siyo mabavu. Uongozi ni kuonyesha njia.

Alichokisema baba Askofu ni kweli. Vyombo vyetu vya dola na vya maamuzi, vinatumia sana udhaifu wa kisheria zenye elements za kikoloni , kukandamiza haki za wananchi wakati siyo lengo.

Wafuasi wa ccm na serikali mnatia aibu. Hebu someni hata hoja zenu. Hazina point hata kidogo .
 
Ni kufanya vizuri kwenye eneo lako la specializatio.

Mfano mleta mada Ni Askofu ambaye ukimwambia onyesha Makanisa yako hata matatu tu yalipo dar es salaam anaingia mitini na kutokomea gizani.Kwake hakujaendelea Hana matawi.

Kwa mkulima maendeleo ni kuongeza uzalishaji na kuongeza kipato kupitia kilimo.
Sasa kama huyo askofu unayemponda kiasi hicho kwamba hawezi hata kuonesha makanisa matatu yalipo hapa Dar, alichaguliwaje kuwa mkuu wa makanisa ya Morovian Tz na mwenyekiti mwenza wa makanisa hayo Africa Mashariki? Nadhani unamwongelea mtu usiyemjua kabisa, na unamkosea adabu.
 
Jeshi la Polisi linamkamata mtu na kumuweka ndani na baada ya kelele nyingi kutoka kwa jamii, mtuhumiwa huandaliwa mashtaka.

Jamhuri inamtuhumu na kumshtaki kwa makosa mbalimbali mazito yasiyodhaminika. Baada ya mtuhumiwa kufikishwa mahakamani kesi hutajwa lakini kesi huahirishwa na mtuhumiwa anaambiwa hawezi kujibu lo lote kwa kuwa 'upelelezi unakuwa bado haujakamilika'!

Kila inapofikia tarehe ya kesi kutajwa, waendesha mashtaka wa Serikali huiambia Mahakama kuwa kesi bado haijakamilika na Hakimu au Jaji hulazimika kuiahirisha tena kesi hadi tarehe nyingine. Huo ndio unakuwa mwanzo wa mateso na kukomolewa kwa mtuhumiwa. Biashara zake na kazi zake huathiriwa vibaya sambamba na familia yake achilia mbali afya yake kuathiriwa akiwa mahabusu!

Inaonekana katika nchi yetu, sisi sote tunakosa ujasiri wa kuhoji ukiritimba huu wa Sheria zetu unaochochewa na watendaji wenye husuda na roho mbaya wanaotumia mwanya wa vipengere kandamizi vya Sheria zetu na hivyo kuwatesa na kuwakomoa wale wasiopatana nao ndani na nje ya mfumo wa Serikali.

Haki yoyote iliyocheleweshwa ni sawa na haki iliyokataliwa (justice delayed is justice denied). Hivyo, kuchelewesha kusikiliza kesi za waliotuhumiwa huku wakiachwa kusota mahabusu ni sawa na kuwacheleweshea na kuwanyima haki yao.

Kwanini umkamate mtu na kumtuhumu na kisha kumshtaki lakini unamuweka mahabusu miezi na hata miaka kwa kisingizio cha upelelezi kutokukamilika katika zama hizi?

Hivi ni kiongozi gani au mamlaka gani inayoweza kufidia hasara za mtuhumiwa aliyecheleweshewa haki hadi kuathirika na kupata magonjwa hadi kifo? Mambo haya yanaumiza sana moyo wangu kwani kwa njia hii watu wengine husigina haki za wengine.

Mambo haya hayatakiwi kufanyika katika nchi inayosadikika kuwa na idadi kubwa ya waumini wa dini zinazofundisha kuhusu haki na upendo ikiwemo dini ya Kikristo. Hasira ya Mungu iko dhahiri kwa mtu mmoja mmoja, jamii au taifa lo lote ambalo watawala na viongozi wake husigina haki za wengine (Amos 5:1-27).

Wiki hii ninawaombea wale wote ambao bado wako mahabusu wengine hata miaka kadhaa kwa sababu upelelezi wa kesi zao 'haujakamilika'.

Ninawaomba wahusika yaani washitaki na wale wote wanaohusika na uendeshaji pamoja na 'upelelezi' wa kesi hizo waingiwe na utu na roho ya huruma huku wakijua kuwa hata wao wenyewe ni wakosefu pia kwa namna moja au nyingine. Ninaomba watu wengine tuungane katika maombi haya lakini kikubwa zaidi tuungane katika kupaza sauti zetu kwa mamlaka husika.

Ninawaomba Mahakimu na Majaji katika Mahakama zetu hasa wale wanaosikiliza kesi za namna hiyo kuwa wakali kwa waendesha mashtaka na wapelelezi 'wanaoonekana kucheza mchezo wa kuchelewesha kesi'. Hakimu au Jaji ni mdau muhimu sana katika upatikanaji wa haki kwa wakati.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani
HILI NDILO TATIZO KUBWA LA HAWA WANAOITWA MAASKOFU WA MAKANISA YA HAPA TANZANIA.WAO NDIO WANASIASA,WANASHERIA WAKUBWA,MAHAKIMU,MAJAJI,MAINJINIA,MADAKTARI NA KILA FANI UNAYOIJUA.
TAFADHALINI IACHENI SERIKALI NA VYOMBO VYAKE VIFANYE KAZI ILI AMANI YETU IENDELEE KUWEPO.MNATAKA HATA ANAYEKULA NJAMA KUIHUJUMU SERIKALI AU KUFANYA UHAINI AKIKAMATWA ASUBUHI AACHIWE JIONI ? UPELELEZI SIYO SAWA NA KUHUBIRI. UNAWEZA KUHUBIRI HATA UWONGO KISHA UKAJIONDKEA ZAKO.
IWAPENDEZE BASI NYIE WATU WA MUNGU MUACHIE MAMLAKA ZIFANYE KAZI YAKE.
 
Back
Top Bottom