Kazi ya kiongozi wa dini sio kuongelea maovu Ni kuongelea mambo ya Mungu
Aisee, unaonekana unajibu kitu usichokielewa na humwelewi hata Mungu aliyekuumba...!!
Mungu aliyetuumba ni wa HAKI na UPENDO. Huwezi kumhubiri Mungu muumba wetu bila kujua haya mambo mawili....
Na sasa hebu rudi kwenye andiko la. Askofu, lisome tena mwanzo mwisho kwa makini. Utagundua kuwa, mantiki ya andiko zima imejikita kwenye HAKI na UPENDO miongoni mwetu binadamu....
Hizi ndizo sifa kuu za MUNGU huyu aliyetuumba kwa mfano wake...
Umeshawahi kujiuliza ni kwanini YESU KRISTO pamoja na kujikita kuhubiri habari ya HAKI na UPENDO na watu kutubu dhambi zao na kumrejea Mungu, lakini watawala wa Rumi ya wakati ule walimchukia sana na kumuona ya kuwa anawaharibia mipango na dili zao?
Ndiyo. Ni kwa sababu (Wanasheria, Mafarisayo, Masadukayo, Watoza Ushuru - sawa na TRA ya kwetu na Watawala/viongozi) waliongozwa na kutawaliwa na unafiki uliozaa uvunjivu wa HAKI za watu kwa ajili ya manufaa yao tu na siyo Mungu sawaswa na ilivyo leo....
Yes, wakamkamata na kumshitaki kwa makosa ya uongo, wakamtesa na kumhukumu KIFO kwa hila tu pasipo HAKI....
Hayo yaliyofanyika nyakati hizo ndiyo yanayofanyika leo ktk tawala za kibinadamu duniani kote na lugha yao haina tofauti yoyote na ya nyakati zile....
Husema "......HUBIRINI DINI na SIASA TUACHIENI SISI WANASIASA.....!!" lengo likiwa watu wasifumbuliwe macho na masikio na fahamu zao kutambua kuwa wanaongozwa na viongozi waovu wasio na UPENDO wala kutenda HAKI....!
Hawa kiuhalisia hawaelewi hata maana ya SIASA kama tu ulivyo wewe.
Ndo kusema: SIASA ndiyo huzaa SERIKALI = UTAWALA/UONGOZI. Uongozi maana yake ni kuongoza watu kwenye NEEMA....
Huwezi kuifikia NEEMA pasipo kuustawisha UPENDO na kuiacha HAKI itamalaki miongoni mwa jamii (watu).....
Mimi nasema SIASA na DINI ni inseparable.....haviachani hata chembe wala nukta moja....