Askofu Mwamakula: Ole kwa Taifa lisilotenda HAKI kwa watu wake! Unamkamata mtu eti upelelezi haujakamilika karne hii?

Askofu Mwamakula: Ole kwa Taifa lisilotenda HAKI kwa watu wake! Unamkamata mtu eti upelelezi haujakamilika karne hii?

Jeshi la Polisi linamkamata mtu na kumuweka ndani na baada ya kelele nyingi kutoka kwa jamii, mtuhumiwa huandaliwa mashtaka.

Jamhuri inamtuhumu na kumshtaki kwa makosa mbalimbali mazito yasiyodhaminika. Baada ya mtuhumiwa kufikishwa mahakamani kesi hutajwa lakini kesi huahirishwa na mtuhumiwa anaambiwa hawezi kujibu lo lote kwa kuwa 'upelelezi unakuwa bado haujakamilika'!

Kila inapofikia tarehe ya kesi kutajwa, waendesha mashtaka wa Serikali huiambia Mahakama kuwa kesi bado haijakamilika na Hakimu au Jaji hulazimika kuiahirisha tena kesi hadi tarehe nyingine. Huo ndio unakuwa mwanzo wa mateso na kukomolewa kwa mtuhumiwa. Biashara zake na kazi zake huathiriwa vibaya sambamba na familia yake achilia mbali afya yake kuathiriwa akiwa mahabusu!

Inaonekana katika nchi yetu, sisi sote tunakosa ujasiri wa kuhoji ukiritimba huu wa Sheria zetu unaochochewa na watendaji wenye husuda na roho mbaya wanaotumia mwanya wa vipengere kandamizi vya Sheria zetu na hivyo kuwatesa na kuwakomoa wale wasiopatana nao ndani na nje ya mfumo wa Serikali.

Haki yoyote iliyocheleweshwa ni sawa na haki iliyokataliwa (justice delayed is justice denied). Hivyo, kuchelewesha kusikiliza kesi za waliotuhumiwa huku wakiachwa kusota mahabusu ni sawa na kuwacheleweshea na kuwanyima haki yao.

Kwanini umkamate mtu na kumtuhumu na kisha kumshtaki lakini unamuweka mahabusu miezi na hata miaka kwa kisingizio cha upelelezi kutokukamilika katika zama hizi?

Hivi ni kiongozi gani au mamlaka gani inayoweza kufidia hasara za mtuhumiwa aliyecheleweshewa haki hadi kuathirika na kupata magonjwa hadi kifo? Mambo haya yanaumiza sana moyo wangu kwani kwa njia hii watu wengine husigina haki za wengine.

Mambo haya hayatakiwi kufanyika katika nchi inayosadikika kuwa na idadi kubwa ya waumini wa dini zinazofundisha kuhusu haki na upendo ikiwemo dini ya Kikristo. Hasira ya Mungu iko dhahiri kwa mtu mmoja mmoja, jamii au taifa lo lote ambalo watawala na viongozi wake husigina haki za wengine (Amos 5:1-27).

Wiki hii ninawaombea wale wote ambao bado wako mahabusu wengine hata miaka kadhaa kwa sababu upelelezi wa kesi zao 'haujakamilika'.

Ninawaomba wahusika yaani washitaki na wale wote wanaohusika na uendeshaji pamoja na 'upelelezi' wa kesi hizo waingiwe na utu na roho ya huruma huku wakijua kuwa hata wao wenyewe ni wakosefu pia kwa namna moja au nyingine. Ninaomba watu wengine tuungane katika maombi haya lakini kikubwa zaidi tuungane katika kupaza sauti zetu kwa mamlaka husika.

Ninawaomba Mahakimu na Majaji katika Mahakama zetu hasa wale wanaosikiliza kesi za namna hiyo kuwa wakali kwa waendesha mashtaka na wapelelezi 'wanaoonekana kucheza mchezo wa kuchelewesha kesi'. Hakimu au Jaji ni mdau muhimu sana katika upatikanaji wa haki kwa wakati.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani

WELL SAID. PAMOJA SANA ASKOFU
 
Nimeikopi mahali.
OLE KWA TAIFA LISILOTENDA HAKI KWA WATU WAKE!
Jeshi la Polisi linamkamata mtu na kumuweka ndani na baada ya kelele nyingi kutoka kwa jamii, mtuhumiwa huandaliwa mashtaka. Jamhuri inamtuhumu na kumshtaki kwa makosa mbalimbali mazito yasiyodhaminika. Baada ya mtuhumiwa kufikishwa mahakamani kesi hutajwa lakini kesi huahirishwa na mtuhumiwa anaambiwa hawezi kujibu lo lote kwa kuwa 'upelelezi unakuwa bado haujakamilika'! Kila inapofikia tarehe ya kesi kutajwa, waendesha mashtaka wa Serikali huiambia Mahakama kuwa kesi bado haijakamilika na Hakimu au Jaji hulazimika kuiahirisha tena kesi hadi tarehe nyingine. Huo ndio unakuwa mwanzo wa mateso na kukomolewa kwa mtuhumiwa. Biashara zake na kazi zake huathiriwa vibaya sambamba na familia yake achilia mbali afya yake kuathiriwa akiwa mahabusu!

Inaonekana katika nchi yetu, sisi sote tunakosa ujasiri wa kuhoji ukiritimba huu wa Sheria zetu unaochochewa na watendaji wenye husuda na roho mbaya wanaotumia mwanya wa vipengere kandamizi vya Sheria zetu na hivyo kuwatesa na kuwakomoa wale wasiopatana nao ndani na nje ya mfumo wa Serikali. Haki ye yote iliyocheleweshwa ni sawa na haki iliyokataliwa (justice delayed is justice denied). Hivyo, kuchelewesha kusikiliza kesi za waliotuhumiwa huku wakiachwa kusota mahabusu ni sawa na kuwacheleweshea na kuwanyima haki yao.

Kwa nini umkamate mtu na kumtuhumu na kisha kumshtaki lakini unamuweka mahabusu miezi na hata miaka kwa kisingizio cha upelelezi kutokukamilika katika zama hizi? Hivi ni kiongozi gani au mamlaka gani inayoweza kufidia hasara za mtuhumiwa aliyecheleweshewa haki hadi kuathirika na kupata magonjwa hadi kifo? Mambo haya yanaumiza sana moyo wangu kwani kwa njia hii watu wengine husigina haki za wengine. Mambo haya hayatakiwi kufanyika katika nchi inayosadikika kuwa na idadi kubwa ya waumini wa dini zinazofundisha kuhusu haki na upendo ikiwemo dini ya Kikristo. Hasira ya Mungu iko dhahiri kwa mtu mmoja mmoja, jamii au taifa lo lote ambalo watawala na viongozi wake husigina haki za wengine (Amos 5:1-27).

Wiki hii ninawaombea wale wote ambao bado wako mahabusu wengine hata miaka kadhaa kwa sababu upelelezi wa kesi zao 'haujakamilika'. Ninawaomba wahusika yaani washitaki na wale wote wanaohusika na uendeshaji pamoja na 'upelelezi' wa kesi hizo waingiwe na utu na roho ya huruma huku wakijua kuwa hata wao wenyewe ni wakosefu pia kwa namna moja au nyingine. Ninaomba watu wengine tuungane katika maombi haya lakini kikubwa zaidi tuungane katika kupaza sauti zetu kwa mamlaka husika.

Ninawaomba Mahakimu na Majaji katika Mahakama zetu hasa wale wanaosikiliza kesi za namna hiyo kuwa wakali kwa waendesha mashtaka na wapelelezi 'wanaoonekana kucheza mchezo wa kuchelewesha kesi'. Hakimu au Jaji ni mdau muhimu sana katika upatikanaji wa haki kwa wakati.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani
 
Hayana maana yoyote ubaguzi aliopiigania wa kijinga kabisa alipigania wazungu wasibague waafrika ili waafrika kusini weusi wajinafasi kubagua waafrika wenzao wa nchi zingine.Umeshaona Afrika kusini mzungu yeyote anafukuza waafrika na kuchoma maduka ya waafrika weusi? Desmond Tutu alipigania Vita ya kijinga sababu Afrika kusini ubaguzi ni.mkubwa wa waafrika kusini weusi kuwabagua waafrika wenzao weusi wa nchi zingine.Angebaki tu Kanisani kusalisha sababu Hakuna ubaguzi alioumaliza
Kweli umeiva akili zimeyeyuka
 
Ni kufanya vizuri kwenye eneo lako la specializatio.

Mfano mleta mada Ni Askofu ambaye ukimwambia onyesha Makanisa yako hata matatu tu yalipo dar es salaam anaingia mitini na kutokomea gizani.Kwake hakujaendelea Hana matawi.

Kwa mkulima maendeleo ni kuongeza uzalishaji na kuongeza kipato kupitia kilimo.
Na yule anayesema yeye ni mpenzi wa Mungu amepata kutaja jina la mungu kwa mamlaka ya nani? Kwenye siasa kuna Mungu?
 
Mwenge huoo mwenge pole sana
Ili nchi iendelee inahitaji kila mtu abobee kwenye eneo lake mfano mkulima alime Sana, injinia afanye Kazi za uinjinia Sana, askofu afanye Kazi za Uaskofu Sana nk ukiona Askofu anavua kofia la Uaskofu kageukia fani ya Sheria au upelelezi ujue nchi inaanza kuchanganyikiwa na kuendelea itakuwa vigumu
 
Una maana kuwa na mwizi aibe sana, mwana siasa muongo aseme uongo sana?
 
Am sorry mtaje tu
Nimeguswa na maneno haya ya
Askofu Mkuu, Baba Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula.

Natamani maneno haya yamguse jamaa yangu fulani, it might make a difference.
Mungu Mbariki sana Baba Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula.

Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali.
 
Ili nchi iendelee inahitaji kila mtu abobee kwenye eneo lake mfano mkulima alime Sana, injinia afanye Kazi za uinjinia Sana, askofu afanye Kazi za Uaskofu Sana nk ukiona Askofu anavua kofia la Uaskofu kageukia fani ya Sheria au upelelezi ujue nchi inaanza kuchanganyikiwa na kuendelea itakuwa vigumu

WATANZANIA AMKENI

CCM KATU HAIWEZI KUKUBALI DEMOKRASIA IFUATE MKONDO WAKE

KIHISTORIA-- CCM NI AFRO SHIRAZI + TANU

AFRO SHIRAZI haikukubali Demokrasia kufuata mkondo Wake na ikatafuta msaada wa Tanu Tanganyika na kupindua matakwa ya wananchi

TANU - Baada ya kupata Uhuru , NYERERE alivifungia vyama vyote vya upinzani na kuanzisha mfumo wa Chama kimoja

KWA HALI HII CCM NI CHAMA KISICHOKUBALIANA NA MAAMUZI YA WANANCHI NA TOKEA MFUMO WA UCHAGUZI KUANZA WANAENDELEZA UHARAMIA WAO
 
Ni kufanya vizuri kwenye eneo lako la specializatio.

Mfano mleta mada Ni Askofu ambaye ukimwambia onyesha Makanisa yako hata matatu tu yalipo dar es salaam anaingia mitini na kutokomea gizani.Kwake hakujaendelea Hana matawi.

Kwa mkulima maendeleo ni kuongeza uzalishaji na kuongeza kipato kupitia kilimo.
Kwahiyo asitetee haki kisa hana makanisa, haki zinazopotea si ni za watanzania wote.
 
Ni kufanya vizuri kwenye eneo lako la specializatio.

Mfano mleta mada Ni Askofu ambaye ukimwambia onyesha Makanisa yako hata matatu tu yalipo dar es salaam anaingia mitini na kutokomea gizani.Kwake hakujaendelea Hana matawi.

Kwa mkulima maendeleo ni kuongeza uzalishaji na kuongeza kipato kupitia kilimo.
Boya wewe kwahiyo kama mimi ni mkulima ni kweli mazao yangu yamestawi vizuri lakin ng'ombe wa mfugaji wanaharibu mazao yangu so nisimkemee huyo mfugaji?

Taifa haliwezi kupiga hatua kwakua na viumbe Wenye uelewa kiduchu kama wako lakin sishangai maana ukiwa mwana fisiem huhitaji kutumia ubongo vizuri
Screenshot_2018-11-20-15-09-16%7E5.png
 
Kama mna uongozi au wafalme waliokosa busara/ wapumbavu basi tegemea kuishi maisha ya taabu na dhiki kuu.
 
Ninavyojua mtuhumiwa akikaa je anaweza kuvuruga ushahidi....ndiyo maana huwa wakati mwingine huwa wanawekwa ndani...Pia wakati mwingine uwekwa ndani kwa usalama wao. Tuheshimu kazi za wenzetu jamani.
Siku yakukute ndipo akili itakukaa sawa.
 
Ni kufanya vizuri kwenye eneo lako la specializatio.

Mfano mleta mada Ni Askofu ambaye ukimwambia onyesha Makanisa yako hata matatu tu yalipo dar es salaam anaingia mitini na kutokomea gizani.Kwake hakujaendelea Hana matawi.

Kwa mkulima maendeleo ni kuongeza uzalishaji na kuongeza kipato kupitia kilimo.
Wewe unahitaji wokovu wa kifikra.
 
Ili nchi iendelee inahitaji kila mtu abobee kwenye eneo lake mfano mkulima alime Sana, injinia afanye Kazi za uinjinia Sana, askofu afanye Kazi za Uaskofu Sana nk ukiona Askofu anavua kofia la Uaskofu kageukia fani ya Sheria au upelelezi ujue nchi inaanza kuchanganyikiwa na kuendelea itakuwa vigumu
Na anayetesa watu awatese kwa bidii na mara nyingi saaaanaaaaaa ndiyo tutaendelea.
 
Hakika yanakera sana watu wanakaa muda mrefu kila siku kesi kuahirishwa, angalia mwandishi Huyu anavyopata tabu, Manji alipata tabu mwisho wa siku anafutiwa mashitaka wakat amesota vya kutosha, angalia wale mashekhe walivyotaabika, sababu ni moja tu upepelezi haujakamilika, sio haki kabisa mtu amekosea apelekwe mahakamani ushahidi uletwe fasta apewe hukumu yake, mtu unakaa miaka mitano upelelezi haujakamilika tu, sasa wapelelezi si waachishwe kazi kama imewashinda?
 
Ninavyojua mtuhumiwa akikaa je anaweza kuvuruga ushahidi....ndiyo maana huwa wakati mwingine huwa wanawekwa ndani...Pia wakati mwingine uwekwa ndani kwa usalama wao. Tuheshimu kazi za wenzetu jamani.
hajakukuta mkuu,hasa pale unapokua hauna hatia ila unawekwa ndani kwa upelelezi,ni bora km una hatia nafsi yako haitaumia
 
Back
Top Bottom