Askofu Mwamakula: RC Makonda asome Wafalme 18:22 ambapo Eliya alisema Yeye ni Nabii tofauti na Makonda alivyohubiri

Na hapa ndiyo nimethitisha kuwa Mwamposa naye ni Nabii wa Baali, angekuwa mtumishi wa Mungu angemsahihisha pale pale huyu muuaji.
 
Tena huyo nabii yupo Kibaha, mkoa wa pwani kwa sasaπŸ‘‡πŸΎ

 
Bashite hafai kuwa kiongozi Wa umma nimeshangaa sana jana analeta siasa kwenye dini na e yule jamaa wa kawe ni hovyo Kabisa hadi waumini wake ni vilaza
 
 
JE,
Askofu hakuzungumza chochote kuhusu yule mnyang'anyi wa malori Arusha, ambae sasa hivi anajiita Nabii na anatani kua hata na nafasi kama yesu?[emoji205]

actually,
Zaburi 23:1 inatosha zaidi
Unamjua Mtume Paulo?
Unamjua Sauli!!?

Yesu Kristo alikuja duniani kwa ajili ya watu kama hao, sasa kwa nini unamsengenya na past yake badala ya kufurahia alipo sasa!!??
 
Mkoa wa owani ndio upi huo mkuu!!??
Upo huko ndotoni mwako!!??
 
Kuna viongozi wa dini hawaelewi hutumia mifano ya manabii agano la kale kama Eliya, Samuel nk kukemea wafalme watawala wanasahau kuwa kipindi hicho dini ilikuwa moja na nabii aliiuwa juu ya mfalme sababu ndiye aliyekuwa akisimika wafalme na kuwapa madaraka kwa kuwapaka mafuta

Hivyo yeye alikuwa bosi wa watawala hivyo kuwakemea haikuwa issue sababu ya kwanza walikuwa waumini wao ya pili mabosi wao na nchi nzima waliwatambua kama wako juu yao na juu ya mfalme mtawala

Ikafika kipindi cha Yohana mbatizaji akaamua kujitosa kwenye kukemea wanasiasa ambao sio waumini wake wala hakuwaweka yeye akamkemea mfalme Herode ambaye hakuwa dini yake wala siye aliyemuweka madarakani Herode akamkata kichwa Yohana mbatizaji.
Yohana aliacha jukumu lake la kuhubiri na kubatiza watu akajitosa kusikomhusu

Kwenye kuhubiri na kubatiza Yohana mbatizaji alifanikiwa mno Yerusalem na Yudea yote walienda kwake kwa agenda moja tu kutubu dhambi na kubatizwa sio kutafuta maombi ya utajiri vyeo vya siasa au umaarufu alipojitosa siasa umaarufu ukapotea na akafa

Sasa hivi hata kanisa katoliki waungama dhambi kwa padri wamepungua ni kama hawapo tena baada ya kanisa kujitosa kwenye siasa .Padri muungamishaji aweza tandika hata usingizi sehemu ya kitubio jumapili haji mtu Wiongozi wa dini wabaki kwenye reli ya dini

Kujilingajisha na manabii wa zamani wakati mazingira tofauti sana ni kutoijua theolojia vizuri Hata katoliki walikuwa na nguvu kubwa mno mapapa kukemea watawala kipindi wao ndio wanawapa utawala wafalme kwenye Roman empire

Makonda yuko sahihi Tanzania haina dini viongozi wa Dini wapeleke maombi kwa Mungu wakiona kuna shida kubwa wasielekeze serikalini

Environment ya sasa sio kama ya enzi zile za manabii Eliya nk
 
Huyu askofu njaa ambaye hana clip yoyote akihubiri kanisani. Hayo manguo ya uaskofu anakusanyaga mashuka minadani anashona, amekonda kama kawaka tayari
Kinembe wale watumishi njaa tunawafahamu. Na watu hawahubiri kwa Clip. Wenye njaaa tunawajua huwa wanajipendekeza kwa watawawala. Huyu ni Utake ni Askofu na Usitake ni Askofu. Kalia Jiti kama hutaki.
 
Manabii
Adam (Adamu)
Nuh (Nuhu)
Ibrahim (Ibrahimu)
Ismail (Isma'il)
Ishaq (Isaka)
Yaqub (Yakobo)
Yusuf (Yusufu)
Musa (Musa)
Harun (Haruni)
Dawud (Daudi)
Sulaiman (Sulemani)
Ayub (Ayubu)
Yunus (Yunusi)
Zakariya (Zakaria)
Yahya (Yohana)
Isa (Yesu)
Lut (Lutu)
Idris (Henoko)
Shu'ayb
Hud
Salih
Muhammad (Mtume wa mwisho)
 
Unamjua Mtume Paulo?
Unamjua Sauli!!?

Yesu Kristo alikuja duniani kwa ajili ya watu kama hao, sasa kwa nini unamsengenya na past yake badala ya kufurahia alipo sasa!!??
ni kwasababu ya ile kiburi ako nayo na ile tamaa mbaya ya kutaka kumpindua hata Yesu, ili awe yeye wakati haiwezekani πŸ’
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…