Askofu Mwamakula: Sikutarajia yaliyoandikwa na Kabendera yangewekwa hadharani wakati wa uhai wangu

Nauliza hivi, Naye Askofu Mwamakula ni "Kitengo" ndani ya ngozi ya kondoo? ... u-classified info anaupata wapi? Awe wazi ili tumuongezee sifa ya ukitengo.
Ukisoma andiko lake hapo juu, zile aya 3 za kwanza zina majibu.
 
Mkuu kuna mtu gani angeweza kusema uovu wa JPM akiwa hai? Acha ungese aisee.
Nadhani ni Lissu pekee alikuwa na hiyo audacity. ALimwambia waziwazi weqe ni "dikteta uchwara". akaswekwa ndani kwa wiki kadhaa, alifunguliwa kesi na kutakiwa kupimwa mkojo! Hakuna mwingine aliyethubutu kumsema mfalme hadharani!
 
Huyu askofu aache uwongo, wale wabunge miongoni mwao ni wake wa viongozi wa Chadema. Kama Chadema wenyewe walishindwa kuwazuia Magufuli angewazuiaje.
Magufuli kafariki, Ndugai siyo Tena mbunge, je hao wabunge wameondilewa?
Ndugai alipokonywa lini ubunge ndugu mchangiaji?
 
Lissu si partner wa IMMMA advocates. Partners wa hio firm ni Ishengoma (aliteuliwa na JPM kuwa Jaji), Masha, Magai, Mujulizi (aliteuliwa kuwa jaji) na Fatma Karume.
 
Kwa hiyo huyu naye kaamua kujiweka hadharani kwamba ni moja ya watoa taarifa wa Kabendera?

I can smell a rat and blood-shedding incited across the country.
 
Umeelezea Vizuri ila hapo mwisho umepuyanga puyanga kama Panya Buku Wewe hayajakukuta ndugu yako auwawe na hata maiti msiione kama kina Ben Saa 8 Mambo mengine usi reasoning kihisia badala ya kutumia Akili yako
😅😅
 
Na wewe ficha upumbavu wako
 
Una IQ ya ngapi?
 
Wewe ungeweza kusema ?
 
Nafikiri ingefika mahali kila mMtanzania anayeipenda nchi yake akiona,akitambua mjinga au wajinga wanaolididimiza taifa letu kwa maslahi yao,mwendo uwe ni kuwapiga ban kila kona hadi akili zao zirudi kwenye mihimili yake.
 
Kwa maneno mengine, Askofu anatuthibitishia kwamba yaliyoandikwa katika kitabu cha Kabendera ni kweli kwani naye alipewa taarifa hizohizo ila hakuwahi kuzisema kokote.
Inashangaza sana, najiuliza nini kinaweza fanya mtu uamini hizi habari baada ya kusoma tu kitabu, na rejea ya Askofu?!

Vitu ambavyo hata source za taarifa ni siri? Na hakuna namna marehemu atakuwa hapa kusema otherwise.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…