Askofu Mwamakula: Sikutarajia yaliyoandikwa na Kabendera yangewekwa hadharani wakati wa uhai wangu

Askofu Mwamakula: Sikutarajia yaliyoandikwa na Kabendera yangewekwa hadharani wakati wa uhai wangu

Mwishoni mwa mwaka 2020, nilipata ujumbe mzito kutoka kwa Rais Magufuli kupitia kwa mtu wake mmoja ambaye jina lake linatunzwa. Rais alimtuma kwangu akiniomba nishawishi Mhe. Freeman Mbowe na Mhe. Tundu Lissu waridhie wabunge wanawake 19 waapishwe kuwa Wabunge wa Viti Maalum.

Nilijitahidi kufurukuta kueleza Rais ajue kuwa sikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA wala mimi sikuwa na ushawishi wowote katika jambo lile. Lakini Rais aliamini kuwa Lissu na Mbowe watanisikiliza mimi.

Lilikuwa jambo gumu sana kwangu kumshawishi mtu yule aniamini mimi. Ahadi niliyoahidiwa na ambayo pia CHADEMA wangepewa kama 'dili' lile lingefanyika ingali katika kilindi cha moyo.

Nakiri kuwa baada ya ombi la Rais la kunitaka niwashawishi Lissu na Mbowe kushindikana, zoezi la uapishwaji liliendelea na mimi nikajua kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari. Lakini hoja la andiko hili sio jambo hili.

Mwezi Januari 2021, alitumwa tena kwangu mtu yule yule. Safari hii haikuwa kunishawishi ili niwashawishi Mbowe na Lissu, bali ilikuwa ni kunitisha niachane na harakati, la sivyo basi nilikuwa nachungulia mauti.

Nilikuwa nimetoka kuitangazia dunia kuwa maisha ya Mhe. Lissu yalikuwa hatarini na ndipo Ubalozi mmojawapo ukamchukua na kumpeleka nje ya nchi.

Kwa hiyo jibu langu kwake lilikuwa moja tu: "Mwambie Mheshimiwa kuwa akitaka aniue, lakini Askofu hatarudi nyuma"! Vitisho vya aina hiyo niliwahi kupewa na Polisi mmoja nikiwa Central Polisi, Dar es Salaam mwezi mmoja kabla Rais Magufuli hajafariki dunia.

Baada ya majibu yale, yule mtu alitetemeka na ikabidi aropoke mambo mengi sana ambayo sio sehemu ya andiko hili kwani kwa sasa Bado mambo yale ni 'classified information'! Baada ya hapo nikaanza kupata taarifa nyingi ambazo zilinitisha na kunipatia matumaini.

Siku moja nilitafutwa na mtu mmoja ambaye ni mzima na kada wa CCM. Kwa kuwa mtu huyo tunaheshimiana na kwa kuwa aliaminishwa ya kuwa mimi nilikuwa natumiwa na 'mabeberu'; ilibidi nimueleze pia baadhi ya mambo ambayo yalikuwa yanamzunguka Rais.

Nilifanya hivyo ikiwa kinga yangu kwani nilijua kuwa ataelewa mazingira yangu na hivyo ataweza kupangua hoja dhaifu dhidi yangu akiwa katika 'Pango la Wakilindi'. Aliishia kunikodolea macho na ndipo tukaagana akiwa kama mtu asiyeamini.

Lakini kabla mtu huyo hajaondoka, aliniuliza: "Wewe umejuaje habari hizi'? Nikamjibu kuwa: "Mimi ni mskofu wa mnyororo na pia mimi ni askofu wa kiapo"! Mambo haya yaliaminiwa pia kwangu chini ya kiapo kwa hiyo nisingeyasema hadharani wakati ule na hata sasa. Hapa sio mahali pake kuelezea kisa cha askari aliyeacha kufanya ibada baada ya kushiriki kuwaua watu na baadaye kumbukumbu za watu wale zikawa zinamjia na kuharibu akili yake.

Mambo haya ni ya kitubio na kwa hiyo mtu ye yote atakayemuendea Mchungaji (Padri) au Askofu kwa kitubio, jambo lile linabakia katika kifua cha mtubishaji, anayetubu na Mungu.

Taarifa za kuchapishwa kwa kitabu cha Erick Kabendera zimeanza kusambaa kwa kasi sana mitandaoni siku ya leo tarehe 3 Januari 2025. Kitabu kinaitwa: 'In the Name of the President: Memoirs of a Jailed Journalist'. Nimesikiliza mahojiano ya Erick Kabendera kuhusu kitabu hicho. Nimeanza kufuatilia maudhui ya kitabu. Mengi ya mambo anayojadili ni sehemu ya yale niliyojulishwa kama 'sisi Askofu'! Ila sikutarajia mambo yale yangewekwa hadharani wakati wa uhai wangu. Ujasiri wa Kabendera unaivuka mipaka ya Nshamba na Kamachumu.

Ninaamini watu ambao walinishangaa kwa nini mimi nilijitoa muhanga kwa ajili ya kutetea haki nchini sasa wataanza kuelewa baada ya kuona na kusoma kitabu cha Erick Kabendera. Taarifa nyingi zilizofikishwa katika kilindi cha moyo wangu ziliishurutisha nafasi yangu kuchukua ili kupaza sauti na kutetea pale nilipoweza. Lakini pamoja na uropokaji wangu, mambo ambayo yalitiwa muhuri (sealed) katika moyo wangu yameamriwa na dhamiri iliyo kuu ili yasiyoke.

Kitabu cha Kabendera kitasaidia katika mambo muhimu. Kwamba tukisome na kumjua Rais Magufuli nje ya uelewa uliojulikana. Baada ya hapo, tuone kuwa alikuwa binadamu kama sisi na mwenye mapungufu na kisha tumsamehe. Kikubwa, kama jamii tutafute njia ya kuponya ikiwemo kuondoa vimelea au masalia ya yale aliyoayaasisi ambayo hayakuwa mazuri na hili itawezekana kama tutasoma na kuielewa sura ya mwisho ya Kitabu cha Kabendera.

Kitabu hiki kinaposambazwa na kusomwa ni vizuri tujue kuwa kinayahusu maisha fichika ya Rais Magufuli na sio maisha ya familia na ukoo wake. Hatuhitaji kwa namna yeyote kuwaona ndugu hata familia kama sehemu ya mambo aliyoyafanya kama Rais kwani nao walikuwa ni washangaaji kama sisi.

Mwisho, natoa wito kwa viongozi wa dini walio karibu na familia ya Ben Sanane na familia ya Azorly Gwanda kuzifikia kwa ajili ya huduma ya kiroho. Kupitia kitabu cha Erick Kabendera na mahojiano yake ni rasmi sasa ya kuwa umma umejulishwa kuwa watu hao hawapo pamoja nasi katika maisha haya.

Hekima iliyo ndani ya kilindi cha moyo wa Rais Samia inaweza kumsaidia afanye nini kwa ajili ya familia hizo. Bila shaka, CHADEMA itatafuta namna njema ya kuhitimisha kwa heshima kwa kumkumbuka Ben, mwanachama na Msaidizi maalum wa Mhe. Mbowe.

Kadhalika, Gazeti la Mwananchi litaona pia namna ya kulihitimisha l kwa heshima ya Azorly, aliyekuwa mtumishi.
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 3 Januari 2025; saa 2:00 usiku
Hadithi hadithi njoo, utamu kolea
 
Ukitaka kujua mtu muongo aliyekubuhu wana sifa moja za kufanana wawe maaskofu au yeyote utasikia marehemu aliniambia wakijua marehemu hawezi fufuka kujitetea au kusema muongo huyu Askofu

Askofu Mwamakula anaangukia kwenye hilo kundi la waongo wabobezi kwa nini hakusema hayo Magufuli akiwa hai?
Wapelekwe mahakamani wakatoe ushahidi.
 
Hivi unajuaje kama mtu katumwa na Rais kuja kwako? Yaani ni kigezo kipi kinakuonesha ni kweli huyu mtu kaagizwa na Rais au wanakujaga na barua?. Maana nijuavyo mimi afisa yeyote kwa utashi wake anaweza akawa hapendi wewe unachokifanya cha kuchafua image ya serikali au ya nchi hivyo ili akunyamazishe itabidi aje akutishe kidogo. All in all JPM hawezi chafuka kwa hadithi za kutunga sababu kazi zake na wema wake kwa taifa bado vinaishi na kila unaposafiri nchii hii kazi zake nzuri zinaonekana na zinamtetea.
Kwani yeye alikuwa mtakatifu, yaani hana dhambi?.
 
Because it takes a month to write, publish a book and get Amazon to distribute it.
You are missing a point, I guess! With Deepseek, Germini, ChatGPT and the like, if you are serious with "hash money" a week is too long ! However, after Kibanda, Meena et al. book failure, I presume Kabe saw the 'evil chance'!
 
Ndugu Kifo si Adhabu ni Mlango kila Mtu atapita kwa Wakati wake hata hivyo Mungu wetu ni mwema kwa wasioshukrani na wenye shukran wapo watakatifu waliokufa wakiwa na umri mdogo na wapo watenda zambi waliokufa wakiwa na umri mkubwa Mungu Hapangiwi
Hakika umenena vema. Utawala wa JPM ulisababisha maumivu makubwa kwa watu wengi, nao wakamlilia Mungu mioyoni mwao. Mungu akasikia kilio chao na kumwondoa mtesi juu yao. Mungu anazo njia nyingi za kukomesha udhalimu kwa watu wake maana uwezo wote upo mikononi mwake.
 
Kumtuhumu mtualiekufa ni hadisi zakijingatu ambazo wajinga ndio wanawezakuamini.

Mnaandika yotehayo kwasababu mnajua muhusika hayupo,hawezi kukubali wala kukanusha.

Wapumbavu tu ndio watakao amini huo upuuzi.

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
 
Andika na wewe kitabu kupinga hizo uziitazo stori zetu dhidi ya huyo DHALIMU MKUU Mwendazake
Hakuna kinachotisha hapo, mauaji yameanza leo? Kwa Nini yawe hadharani wakati huu? Kwani unataka kusema waliouawa awamu nyingine wao sio binadamu? Mbona hayafufuliwi?
 
Waliohudumu katika top positions kwa wamu ya 5 have to be accountable for the deeds of their boss as in one way or another they aided the killer!.........IGP, RCs, RCOs, and the like!
 
You are missing a point, I guess! With Deepseek, Germini, ChatGPT and the like, if you are serious with "hash money" a week is too long ! However, after Kibanda, Meena et al. book failure, I presume Kabe saw the 'evil chance'!
Yeah, very sensible, the magic of AI. Never mind the fact that he's made it known that he's been working on a book for a long time. Make up your mind, is it about countering CDM's infighting or books about a subject you don't like that supposed failed by your standards?

The meat gobbling isn't helping your thinking
 
COVID 19 ni dili ya Mbowe sasa sijui Askofu anataka kutuambia nini.

JPM alikuwa na nia ya dhati kabisa na nchi hii, kuitoa ilipo na kuipeleka mahala.
Wapumbavu wengi walitumia mbinu mbalimbali kumkwamisha katika nia yake hii na hapo ndio shida ilipoanzia.

JPM alipigana vita zote, za ndani ya chama chake CCM, nje ya chama chake wapinzania feki waliozoea kula kwa mongo wa siasa, wapinzania wa nje ya mipaka ya Tanzania waliozoea kuwaibia Watanzania na kula pamoja na Watanzania wenzetu ndani ya nchi.
Hizi vita alizopigana JPM ndio zimeleta uadui wote huu dhidi yake.

Leo CDM tunaona wanavyoshutumiana dhidi ya masuala ya rushwa, rushwa kutoka CCM, watu hawa hawa leo watamsema JPM, ugomvi wao na JPM nikuwakatia mirija na mafungu waliyokuwa wanapewa kuendesha upinzani feki.

JPM kuwakatia watu mirija ya hela za kuchezea ndani ya mifumo na kuwanyima watu fursa za kijingajinga kupeanapeana ajira, kuendesha semina na masafari ya nje pamoja na kufirisi baadhi ya watumishi na wafanyabiashara walioihujumu nchi NDIO KUMELETA NA KUZAA YOTE HAYA.

Wivu Kwa mageuzi aliyoyafanya JPM ambayo wengine yamewashinda mpaka Leo watu wamebaki na kinyongo na marehemu.
Mazishi ya kitaifa na response ya wananchi dhidi ya marehemu JPM imesababisha wivu kwa marehemu mpaka leo.

JPM alithubutu hata kureview mikataba ya Makampuni ya madini kwa manufaa ya Watanzania na sio wachache waliokuwa wanajichotea tu kupitia hizi kampuni kupitia vijana wao waliowapandikiza kila mahala.
Alichokifanya JPM ndio Leo hii tunaona kinatokea Mali, Niger,Burkina Faso nk.

JPM pamoja na mapungufu yake, ataendelea kuwa shujaa katika nchi hii na hawezi kufananishwa na Rais yeyote yule ukimtoa Nyerere.
 
Back
Top Bottom