Askofu Mwamakula: Sikutarajia yaliyoandikwa na Kabendera yangewekwa hadharani wakati wa uhai wangu

Askofu Mwamakula: Sikutarajia yaliyoandikwa na Kabendera yangewekwa hadharani wakati wa uhai wangu


View: https://youtu.be/HfQqupIGlKM?si=onGz-98ZMq-nvwC3

Kwenye hii video angalia kuanzia dakika ya 50 anasema alimpigia simu Generali mmoja wa JWTZ kwa simu inayoficha mawasiliano yao.

Generali akaenda chumbani kwake, akafunga kufuli, halafu akamwambia subiri kwanza mimi nina kitanda kikubwa hivi, akaingia uvunguni mwa kitanda chake kabla ya kuanza kuongea naye.

Huyu ni generali aliyekuwepo Uganda na kumuondoa Iddi Amin. Anasema ni shujaa.

Sikiliza mwenyewe halafu tumia akili kidogo kutafakari uongo wa kitoto wa aina hii anajaribu ku-mix ukweli na uongo awe na story ya kusisimua kama fiction yoyote.

Kwa msioamini unyama wa Magufuli shauri yenu. Ila tambua Tanzania ilikuwa inaongozwa na kichaa kuanzia 2015 hadi 2021.

Mwaka 2012, Magu akiwa Waziri alibaka binti yake na kisha binti aka commit suicide kuficha hiyo aibu
 

View: https://youtu.be/HfQqupIGlKM?si=onGz-98ZMq-nvwC3
Kuanzia dakika 55, Kabendera anasema inabidi kuondoa dhambi ya waasisi wa hii nchi kuanzisha mahakama kama ya Ujerumani iliyowahukumu nazi kule Nuremberg anasema Nyerere Waa wa hili taifa ndioa chanzo cha haya yote.

Kwahiyo wote waliosalia toka uhuru hadi sasa inabidi watafutwe, wafikishwe mahakamani na kuhukumiwa ili kuondoa mbegu mbovu. Kuponya Taifa.

Kuna uongouongo mwingi, inconsistents, anasema ukikaa barazani unasikia mengi.
 
Hawa hawa chadema ndo walikua hawataki covid19 waapishwe had magufuli akuombe weew uongee na mbowe?!!! Then imekuaje mbona wako upande wa mbowe had leo?!
Mbowevalijifanya kukataa kumbe gelesha. Eniwei, COVID19 walishafutwa uanachama.
 
Ukitoka maoni dhidi ya nchi badala ya kutoa maoni ya kujenga nchi Tena ukiwa kiongozi wa dini...lazima tujiulize maswali.
Ukweli huwa ni ukweli tu. Haupigiwi kura wala kufanyiwa make up. Kama uovu umefanyika katika nchi, ukweli kuhusu huo uovu na waovu husika hauwezi kufichwa ili kuficha aibu ya nchi. Ukweli unasemwa, uovu na waovu wajulikane na nchi ibadilike kwa serikali kushughulikia huo uovu au kujifunza namna ya kuushughulikia.
 
Bishop ndie aliekuwa central na kuna polisi alienda kumtisha ujumbe ssj

Bishop ndie alikuwa central na kuna polisi alitumwa aende kumpa vitusho ila sijajua ujumbe ulitoka kwa nani labda ujumbe ulitoka kwa mwendazake maana kwa hali ilivyo yeye ndio mtuhumiwa namba moja
Asante mkuu
 
Ukitaka kujua mtu muongo aliyekubuhu wana sifa moja za kufanana wawe maaskofu au yeyote utasikia marehemu aliniambia wakijua marehemu hawezi fufuka kujitetea au kusema muongo huyu Askofu

Askofu Mwamakula anaangukia kwenye hilo kundi la waongo wabobezi kwa nini hakusema hayo Magufuli akiwa hai?
Kumbe akisemwa mtu unayemuheshimu kwa mambo ambayo hayajathibitika inawauma.Mara kibao tu mnamsema mbowe uku mitandaoni kwa mambo mengi ambayo hamna ushahidi nayo ila mnayang'ang'ania kwasababu ya chuki zenu.sasa kaguswa wa kwenu mnatoa milio kila kona.
 
Haya uliyoondika hayaondoi hata chembe ya uovu aliowafanyia wakosoaji wake na wapinzani. Usitake kuchanganya wajibu wake aliokuwa analipwa mshahara, na maovu aliyokuwa anatenda.

Nani
Haya uliyoondika hayaondoi hata chembe ya uovu aliowafanyia wakosoaji wake na wapinzani. Usitake kuchanganya wajibu wake aliokuwa analipwa mshahara, na maovu aliyokuwa anatenda.

Tanzania hakuna upinzani, kuna kikundi cha wahuni nyuma ya upinzani, huko kikundi kina kazi mbili, kazi ya Kwanza ni kutumia upinzani kama bargain chip incase na kazi ya pili ni kumanipulate watu ili Tanzania kuonekana kuna upinzani.

Awamu ya tano, upinzani ulitumika kama bargaining chip dhidi ya JPM baada ya kupambana na kile kikundi cha walaji nchi, hapa walaji nchi walikaa nyuma ya upinzani lengo kumtingisha na kumlegeza JPM, hapo ndio shida ilipoanzia kwa wanaojiita upinzani na wakosoaji wa JPM awamu ya tano.
 
Ukitaka kujua mtu muongo aliyekubuhu wana sifa moja za kufanana wawe maaskofu au yeyote utasikia marehemu aliniambia wakijua marehemu hawezi fufuka kujitetea au kusema muongo huyu Askofu

Askofu Mwamakula anaangukia kwenye hilo kundi la waongo wabobezi kwa nini hakusema hayo Magufuli akiwa hai?
Swali la kipumbavu sana hili. Ni mara ngapi Mwamakula alisema mambo yanayohusu utawala wa JPM mkaishia kumbeza kama anavyofanya sasa hivi?

Lakini pia, walioishi wakati wa World War II hawaruhusiwi kusema lolote kuwahusu Mussolini na Hitler eti kwavile walishakufa na hawawezi kujitetea? Hizi akili sijui za wapi tuu?
 
Nani

Tanzania hakuna upinzani, kuna kikundi cha wahuni nyuma ya upinzani, huko kikundi kina kazi mbili, kazi ya Kwanza ni kutumia upinzani kama bargain chip incase na kazi ya pili ni kumanipulate watu ili Tanzania kuonekana kuna upinzani.

Awamu ya tano, upinzani ulitumika kama bargaining chip dhidi ya JPM baada ya kupambana na kile kikundi cha walaji nchi, hapa walaji nchi walikaa nyuma ya upinzani lengo kumtingisha na kumlegeza JPM, hapo ndio shida ilipoanzia kwa wanaojiita upinzani na wakosoaji wa JPM awamu ya tano.
We ni mwongo mbona jpm hakutumia kama ngao ikiwa upinzani uko mikononi mwa ccm
 
Sitakaa hata siku moja kupinga taarifa za mtu ikiwa Mimi Sina taarifa rasmi na za kweli.

Nachukia sana kupinga kitu kisa Nina mihemko.

Katika kila jambo ninalopata kulisoma kama Sina taarifa sahihi na za kweli ili kumpinga mtu Huwa ninanyamaza na kujifunza.

All in All ... Mungu ni mwema!
 
Nani

Tanzania hakuna upinzani, kuna kikundi cha wahuni nyuma ya upinzani, huko kikundi kina kazi mbili, kazi ya Kwanza ni kutumia upinzani kama bargain chip incase na kazi ya pili ni kumanipulate watu ili Tanzania kuonekana kuna upinzani.

Awamu ya tano, upinzani ulitumika kama bargaining chip dhidi ya JPM baada ya kupambana na kile kikundi cha walaji nchi, hapa walaji nchi walikaa nyuma ya upinzani lengo kumtingisha na kumlegeza JPM, hapo ndio shida ilipoanzia kwa wanaojiita upinzani na wakosoaji wa JPM awamu ya tano.
Ww utakuwa ni mzee lazima, maana wazee ndio huamini propaganda za aina hii. Nakushauri mzee wangu amka, kizazi hiki sio cha propaganda za aina hiyo.
 
Ww utakuwa ni mzee lazima, maana wazee ndio huamini propaganda za aina hii. Nakushauri mzee wangu amka, kizazi hiki sio cha propaganda za aina hiyo.
Huyo jamaa andiko la Kabender limemchanganya hadi amelose focus kwenye fikra zake
 
KABENDERA ANADAI BEN SANANE ALIUAWA NA 'BWANA MKUBWA'!

Mwishoni mwa mwaka 2020, nilipata ujumbe mzito kutoka kwa Rais Magufuli kupitia kwa mtu wake mmoja ambaye jina lake linatunzwa. Rais alimtuma kwangu akiniomba nishawishi Mhe. Freeman Mbowe na Mhe. Tundu Lissu waridhie wabunge wanawake 19 waapishwe kuwa Wabunge wa Viti Maalum.

Nilijitahidi kufurukuta kueleza Rais ajue kuwa sikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA wala mimi sikuwa na ushawishi wowote katika jambo lile. Lakini Rais aliamini kuwa Lissu na Mbowe watanisikiliza mimi. Lilikuwa jambo gumu sana kwangu kumshawishi mtu yule aniamini mimi. Ahadi niliyoahidiwa na ambayo pia CHADEMA wangepewa kama 'dili' lile lingefanyika ingali katika kilindi cha moyo.

Nakiri kuwa baada ya ombi la Rais la kunitaka niwashawishi Lissu na Mbowe kushindikana, zoezi la uapishwaji liliendelea na mimi nikajua kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari. Lakini hoja la andiko hili sio jambo hili.

Mwezi Januari 2021, alitumwa tena kwangu mtu yule yule. Safari hii haikuwa kunishawishi ili niwashawishi Mbowe na Lissu, bali ilikuwa ni kunitisha niachane na harakati, la sivyo basi nilikuwa nachungulia mauti. Nilikuwa nimetoka kuitangazia dunia kuwa maisha ya Mhe. Lissu yalikuwa hatarini na ndipo Ubalozi mmojawapo ukamchukua na kumpeleka nje ya nchi.

Kwa hiyo jibu langu kwake lilikuwa moja tu: "Mwambie Mheshimiwa kuwa akitaka aniue, lakini Askofu hatarudi nyuma"! Vitisho vya aina hiyo niliwahi kupewa na Polisi mmoja nikiwa Central Polisi, Dar es Salaam mwezi mmoja kabla Rais Magufuli hajafariki dunia.

Baada ya majibu yale, yule mtu alitetemeka na ikabidi aropoke mambo mengi sana ambayo sio sehemu ya andiko hili kwani kwa sasa Bado mambo yale ni 'classified information'! Baada ya hapo nikaanza kupata taarifa nyingi ambazo zilinitisha na kunipatia matumaini.

Siku moja nilitafutwa na mtu mmoja ambaye ni mzima na kada wa CCM. Kwa kuwa mtu huyo tunaheshimiana na kwa kuwa aliaminishwa ya kuwa mimi nilikuwa natumiwa na 'mabeberu'; ilibidi nimueleze pia baadhi ya mambo ambayo yalikuwa yanamzunguka Rais. Nilifanya hivyo ikiwa kinga yangu kwani nilijua kuwa ataelewa mazingira yangu na hivyo ataweza kupangua hoja dhaifu dhidi yangu akiwa katika 'Pango la Wakilindi'. Aliishia kunikodolea macho na ndipo tukaagana akiwa kama mtu asiyeamini.

Lakini kabla mtu huyo hajaondoka, aliniuliza: "Wewe umejuaje habari hizi'? Nikamjibu kuwa: "Mimi ni mskofu wa mnyororo na pia mimi ni askofu wa kiapo"! Mambo haya yaliaminiwa pia kwangu chini ya kiapo kwa hiyo nisingeyasema hadharani wakati ule na hata sasa. Hapa sio mahali pake kuelezea kisa cha askari aliyeacha kufanya ibada baada ya kushiriki kuwaua watu na baadaye kumbukumbu za watu wale zikawa zinamjia na kuharibu akili yake.

Mambo haya ni ya kitubio na kwa hiyo mtu ye yote atakayemuendea Mchungaji (Padri) au Askofu kwa kitubio, jambo lile linabakia katika kifua cha mtubishaji, anayetubu na Mungu.

Taarifa za kuchapishwa kwa kitabu cha Erick Kabendera zimeanza kusambaa kwa kasi sana mitandaoni siku ya leo tarehe 3 Januari 2025. Kitabu kinaitwa: 'In the Name of the President: Memoirs of a Jailed Journalist'. Nimesikiliza mahojiano ya Erick Kabendera kuhusu kitabu hicho. Nimeanza kufuatilia maudhui ya kitabu. Mengi ya mambo anayojadili ni sehemu ya yale niliyojulishwa kama 'sisi Askofu'! Ila sikutarajia mambo yale yangewekwa hadharani wakati wa uhai wangu. Ujasiri wa Kabendera unaivuka mipaka ya Nshamba na Kamachumu.

Ninaamini watu ambao walinishangaa kwa nini mimi nilijitoa muhanga kwa ajili ya kutetea haki nchini sasa wataanza kuelewa baada ya kuona na kusoma kitabu cha Erick Kabendera. Taarifa nyingi zilizofikishwa katika kilindi cha moyo wangu ziliishurutisha nafasi yangu kuchukua ili kupaza sauti na kutetea pale nilipoweza. Lakini pamoja na uropokaji wangu, mambo ambayo yalitiwa muhuri (sealed) katika moyo wangu yameamriwa na dhamiri iliyo kuu ili yasiyoke.

Kitabu cha Kabendera kitasaidia katika mambo muhimu. Kwamba tukisome na kumjua Rais Magufuli nje ya uelewa uliojulikana. Baada ya hapo, tuone kuwa alikuwa binadamu kama sisi na mwenye mapungufu na kisha tumsamehe. Kikubwa, kama jamii tutafute njia ya kuponya ikiwemo kuondoa vimelea au masalia ya yale aliyoayaasisi ambayo hayakuwa mazuri na hili itawezekana kama tutasoma na kuielewa sura ya mwisho ya Kitabu cha Kabendera.

Kitabu hiki kinaposambazwa na kusomwa ni vizuri tujue kuwa kinayahusu maisha fichika ya Rais Magufuli na sio maisha ya familia na ukoo wake. Hatuhitaji kwa namna yeyote kuwaona ndugu hata familia kama sehemu ya mambo aliyoyafanya kama Rais kwani nao walikuwa ni washangaaji kama sisi.

Mwisho, natoa wito kwa viongozi wa dini walio karibu na familia ya Ben Sanane na familia ya Azorly Gwanda kuzifikia kwa ajili ya huduma ya kiroho. Kupitia kitabu cha Erick Kabendera na mahojiano yake ni rasmi sasa ya kuwa umma umejulishwa kuwa watu hao hawapo pamoja nasi katika maisha haya.

Hekima iliyo ndani ya kilindi cha moyo wa Rais Samia inaweza kumsaidia afanye nini kwa ajili ya familia hizo. Bila shaka, CHADEMA itatafuta namna njema ya kuhitimisha kwa heshima kwa kumkumbuka Ben, mwanachama na Msaidizi maalum wa Mhe. Mbowe. Kadhalika, Gazeti la Mwananchi litaona pia namna ya kulihitimisha l kwa heshima ya Azorly, aliyekuwa mtumishi.
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 3 Januari 2025; saa 2:00 usiku
Nasi Tuseme Ameeeen. Ila JIWE ukawe MAKAA ya Kubandikia chakula cha Shetani Kubabako Ulale pabaya Peponi
 
Tangu hizi habari zianze kusambaa hatujaona uthibitisho hata mmoja. Ni hearsays, speculations na personal opionions tu zinatawala. What a crap kutoka kwa a self-declared bishop.

Na bahati nzuri zinatoka kwa walewale vibaraka wa mabeberu. Hatushangai kama ambavyo hatushangai panya kumchukia paka.

It changes nothing especially kazi kubwa aliyolifanyia taifa hili Rais bora kabisa kuwahi kutokea.
Wewe nawe kaliwe na PopoBawa na Huyo marehemu wenu
 
Sina mashaka na andiko la askofu Mwamakula. Mashaka yangu ni kuwa aliye achiwa kiti lazima alikuwa anayajua yote haya na yale asiyoyajua wakati ule sasa ameyajua kutokana na source mbalimbali alizo nazo.
Lakini kutamka "mimi na yule ni kitu kimoja" inaacha maswali! Jee aliropoka au ni kweli yuko hivyo?
Najua sio rahisi naye kumpiga za kichwa asiyempenda, lakini jee hawezi kuagiza bila moyo kustuka?
Acha niendelee kujiuliza!
Wale wale tu sema na yeye siku zake zinahesabika
 
JPM alitufunulia na kutuonyesha namna mambo mengi mazuri yanaweza kufanyika katika nchi hii na nchi ikaenda mbele kwa haraka.

Taifa hili hela nyingi inapotea mikononi mwa watu wasiowaaminifu kuanzia watumishi, wafanyabiashara na makampuni ya nje yaliyojikita kwenye fraud kwa kushirikiana na watumishi na viongozi.

Kupitia JPM watu wengi walijua shida ya nchi hii ni ombwe la uongozi na kukiwa na kiongozi shupavu basi mambo yanaweza kwenda kwa kasi.

Mapenzi ya wananchi mitaani dhidi ya JPM ni makubwa sana na ukweli uliowazi, WANANCHI WANAHITAJI JPM mwingine.

Binafsi kwangu JPM alikuwa na huruma sana, alipaswa kuua wapumbavu na wajinga weeengi sana katika nchi hii ambao wanaua watu kila siku kupitia upumbavu wao.
Umeelezea Vizuri ila hapo mwisho umepuyanga puyanga kama Panya Buku Wewe hayajakukuta ndugu yako auwawe na hata maiti msiione kama kina Ben Saa 8 Mambo mengine usi reasoning kihisia badala ya kutumia Akili yako
 
Back
Top Bottom