Askofu Mwamakula sio mhuni, wahuni ni nyie mnaotetea maovu. Watanzania tunataka Katiba Mpya

Askofu Mwamakula sio mhuni, wahuni ni nyie mnaotetea maovu. Watanzania tunataka Katiba Mpya

Watanzania wanahitaji katiba mpya maana wanajua fika mwarobaini wa matatizo yao....
Kama watanzania mnataka katiba mpya mbona hamuandamani sasa? Achen unafiki mnaponza askofu,mwambieni ukweli aendelee na kazi yake ya kumtumikia Mungu.
 
Je, ni vitu hivyo tu abavyo mnataka katiba mpya ifanye? Inaonekana wengi hamjui maana ya katiba! Kufuatana na katiba ya sasa, vipengele vyote ulivyo vitaja ni uhalifu na kama ukimshitaki aliye tenda makosa hayo - kama una ushahidi wa kutosha, ataadhibiwa.
Hivyo kama unatetea kuwepo kwa katiba mpya jaribu kujua faida zake - ni nini ambazo mtanzania wa kawaida atapata.
Mbona faida zinajulikana tayari na mchakato ulishaanzana, Watanzania wakatoa mawazo yao kabla ukasimamishwa kinyemela na wajuaji wa awamu hii.
 
Anajua
Je, ni vitu hivyo tu abavyo mnataka katiba mpya ifanye? Inaonekana wengi hamjui maana ya katiba! Kufuatana na katiba ya sasa, vipengele vyote ulivyo vitaja ni uhalifu na kama ukimshitaki aliye tenda makosa hayo - kama una ushahidi wa kutosha, ataadhibiwa.
Hivyo kama unatetea kuwepo kwa katiba mpya jaribu kujua faida zake - ni nini ambazo mtanzania wa kawaida atapata.
Anajua zaidi ya ujuavyo hiyo short list ameiweka Kama kejeli kwa watawala na dola Pumbavu.
 
Tu
Msije na madai ya katiba kwa lengo la kuitoa ccm madarakani. Ainisheni faida za katiba mpya ili na wasio wanazi wa vyama waone watafaidikaje.

Lengo la katiba siyo kuitoa ccm madarakani kama mnavyoaminishana nyie.
Tunataka katiba itakayoruhusu matokeo ya urais yahojiwe mahakamani.
Tunataka katiba utakayotambua heshima ya utu na haki ya kuishi kutaka kuuwawa kwa lisu Ben na azory kumetufunza mengi.Pia tunataka katiba itakayotupa nguvu kumpinga chini rais na chama chake wakizingua bila kuleta fujo ndani ya nchi.
 
Chadema ni wajinga sana! Yani ukiwauliza mnataka katiba mpya ili iweje wanakwambia ili tuitoe ccm madarakani[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Jamani katiba ni karatasi tu, hazipigi kura wala kutangaza matokeo. Hivi kule ambako vyama tawala vimeondolewa kulianza na katiba mpya?
Katiba ni kwa watanzania wote, sio chama fulani
 
Huyo Askofu ana akili sana kizazi chake kitakumbukwa kwa kufanya Jambo jema kwenye utawala mgumu...
 
Wamkamate watahamasisha vurugu na hii ndiyo itageuka kuwa fimbo yao ya kujichapia
Mwamakula ana umuhimu na ushawishi mdogo kwa umma - na anachefusha umma anapo ingia siasa kwa mgongo wa dini! Angemuiga bosi wake Lissu, ambaye alijitahidi kwa akili zake ndogo eti ku-balance kura za waumini wote kwa kuvaa kanzu na balaghashia kila ijumaa ya kampeni zake! Kitendo cha kujitangaza yeye ni askofu wa dhehebu fulani atawapata wachache. Itakuwa ni vurugu!
 
Katiba mpya itapatikana soon, hapo ndipo impact yake utaiona.
Kila kitu kina wasaa wake. hata katiba mpya, muda ukiwadia itakuja. Sio kwa maandamano ya Askofu Mwamakula. He has got no influence on anything. Tusianze kudanganyana na kumdanganya mwenyewe akafikiri analofanya ni la maana
 
Back
Top Bottom